biashara ya taxi

biashara ya taxi

i411

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
906
Reaction score
293
Nina kacorola kangu nakataka nikafanye taxi. hivi mahesabu nitegemeaje kwa siku nzuri na kwa wiki. Nataka jua hili nione kama naweza jipatia kaela ka mboga au nikauzie tu nduguzangu.
 
Nina kacorola kangu nakataka nikafanye taxi. hivi mahesabu nitegemeaje kwa siku nzuri na kwa wiki. Nataka jua hili nione kama naweza jipatia kaela ka mboga au nikauzie tu nduguzangu.
uko wapi..yaani pande zipi?
 
Nina kacorola kangu nakataka nikafanye taxi. hivi mahesabu nitegemeaje kwa siku nzuri na kwa wiki. Nataka jua hili nione kama naweza jipatia kaela ka mboga au nikauzie tu nduguzangu.
Mimi hii biashara ndio naonaga ni biashara kichaa,unaenda kununua gari kwa sh million 8 mpaka 10 unampa dereva anakuletea husabu ya elfu 10 mpaka 15,mimi ntafungua genge nimeweka hela nyingi sana laki 3 ntapata faida ya 15 mpaka 30000,sifanyi service,genge halichakai,risk ya ajali hamna,kwa ujumla kama una gari yako usijeifanya taxi kabisa,haina faida manake hesabu yake ni ndogo sana hesabu ya elfu 15,000 haitakulipa itaishia kwenye service,achana nayo hiyi biashara kwa ushauri wangu.
 
hata kwa walewanaofanya hapo airport mambo yao ni hivi au wananafuukidogo
 
Nina kacorola kangu nakataka nikafanye taxi. hivi mahesabu nitegemeaje kwa siku nzuri na kwa wiki. Nataka jua hili nione kama naweza jipatia kaela ka mboga au nikauzie tu nduguzangu.
labda uendeshe mwenyewe lakini ukimpa dereva ni biashara ya hovyo sana hiyo.
 
Mimi hii biashara ndio naonaga ni biashara kichaa,unaenda kununua gari kwa sh million 8 mpaka 10 unampa dereva anakuletea husabu ya elfu 10 mpaka 15,mimi ntafungua genge nimeweka hela nyingi sana laki 3 ntapata faida ya 15 mpaka 30000,sifanyi service,genge halichakai,risk ya ajali hamna,kwa ujumla kama una gari yako usijeifanya taxi kabisa,haina faida manake hesabu yake ni ndogo sana hesabu ya elfu 15,000 haitakulipa itaishia kwenye service,achana nayo hiyi biashara kwa ushauri wangu.

ureni

hilo jina lako au la eneo!
pili mi nilikuwa na tax 2 niliamua kuziuza zote, hakuna hesabu ni longo longo tu.
 
Nina kacorola kangu nakataka nikafanye taxi. hivi mahesabu nitegemeaje kwa siku nzuri na kwa wiki. Nataka jua hili nione kama naweza jipatia kaela ka mboga au nikauzie tu nduguzangu.

Muulize mbunge wa Nzega, H. Kingwangala amefanya sana hiyo (As per his own admission) biashara na ni memba humu.
 
Nina kacorola kangu nakataka nikafanye taxi. hivi mahesabu nitegemeaje kwa siku nzuri na kwa wiki. Nataka jua hili nione kama naweza jipatia kaela ka mboga au nikauzie tu nduguzangu.

Hakuna kinachonikuna kama kumuona mtu akitaka kuboresha maisha yake kwa rasilimali alizonazo.
Boss ni swala zuri kutaka kufanya txi io gari yako lakini ebu kumbuka umeinunua kwa sho ngapi na ungependa iwe imerudisha baada ya muda gani?
Kasheshe inakuja sema umempa kazi huyo dereva atafute chochote.
kwa siku 15,000 x 28(wiki 4) = 420,000/=. x 12 (mwaka) = 5m/-
Kasheshe hapo bado mahesabu ya service, kubadilisha vifaa vya gari, na mengineo.
Italipa kama gari yako iko bomba, ila kama ndio imeanza kuchoka mkuu, naona wewe tafuta business nyingine tu.

Na nashauri usiogope kuchekwa, fanya biashara yoyote ile so long as iwe inaingiza kuanzia alfu 15,000/- na kuendelea kwa siku.
Kila la heri.
Kwa idea, jiulize je ni kitu gani ambacho kila kukicha wewe au familia zingine kila kukicha ni lazima wanunue.
Hapo utapata jibu boss
 
mimi nilikuwa nazania ningeweza pata kama 50,000 kwa airport daaa kumbe ni hali ngumu
 
mimi nilikuwa nazania ningeweza pata kama 50,000 kwa airport daaa kumbe ni hali ngumu

Kama utakua unaganga wewe mweyewe mkuu labda kwa kweli unaweza kupata hio alf 50.

Swala uko tarayi kuchukua likizo au kuacha kazi kabisa halafu nguvu zote ukapeleka hapo?

Wewe ndio muamuzi, ukiifanya wewe mwenyewe 30 mpaka hio 50 utapata, ila sio kila siku.

Endelea kufanya research.
 
Wahindi wako very successful kwenye hili eneo kwa vile wako strict na makusanyo. Asubuhi dreva anapochukua taxi kwa Mhindi anamkabidhi fedha in advance kwanza ndipo anapewa funguo. So ni juu yake kuhangaika kuhakikisha anaipata hiyo fedha barabarani.
 
Kaka biashara kichaa hiyo.
Sikukatishi tamaa ila mimi ni mbishi lakini nilinyoosha mikono.
Uza fanya biashara nyingine,hii nchi inaangalia mapato yake kutoka sehemu moja bila kuamgalia kipato cha eneo hilo.
 
Hii biashara ni nzuri kama wewe ni mjasiriamali,ambaye uko tayari kuchukua "risk".Huyu jamaa anayesema genge,kwani nyanya haziozi,kwa hiyo mwenye uamuzi wa mwisho ni wew binafsi,mbona kuna wanafunzi wanapata sifuri kwenye mitihani lakini watoto hawaachi kusoma.Mimi ninaTEKSI na inalipa kweli,kuwa na dereva mwaminifu
 
HAPO NILIPO-BOLD NA KU-HIGLIGHT IN BLUE "NDIO PENYE UTATA KUHUSU BIASHARA HIYO NA NYINGI TUU ZA MAGARI KWA DAR ES SALAAM"...mara dereva akuambie gari imenock chasis mara block ni ya kubadilisha ukiwa hujui mambo ya magari ndio unampa makusanyo yote ya mwezi akatengeneze gari kisha anakuletea michuma mibovu anakubwagia hapo home unaona kweli kafanya kazi....TAX BUSINESS= UPUUZI MTUPU
 
taxi hailipi.miundombinu mibovu dar,ajali nje nje.halafu tax ni nyingi,kuna upinzani wa bajaj na pikipiki.so kwa dar bajaj ingefaa ukaipaki zako pale mwenge au bamaga usiku unapaki zako maisha club,sansiro,masai au bill's.ni ushauli tu.coz taxi ikihalibika kupata wa kukusukuma ni hela tofauti na bajaj.mia
 
Tujaribu kubuni biashara nyingine ambazo wengi hawajaingiza pua na kushika kazi ya ushindani. Kama nafasi inaruhusu mtaji wa gari ulilo nalo unaweza nunua mtumba wa mtambo wa kuchuja mafuta, kubangua na kuzindika karanga na korosho na kufanya packaging kwa mauzo yenye uhakika kiafya, na mengine mengi tu.
 
Tujaribu kubuni biashara nyingine ambazo wengi hawajaingiza pua na kushika kazi a ushindani. Kama nafasi inaruhusu mtaji wa gari ulilo nalo unaweza nunua mtumba wa mtambo wa kuchuja mafuta, kubangua na kuzindika karanga na korosho na kufanya packaging kwa mauzo yenye uhakika kiafya, na mengine mengi tu.
YES! Huu ushauri wa kuwekeza ktk mitambo ya kutengeneza mafuta naukubali sasa hebu tujuze zaidi- iko wapi, bei zikoje, installation charges, power, labour, etc. I AM INTERESTED.
 
YES! Huu ushauri wa kuwekeza ktk mitambo ya kutengeneza mafuta naukubali sasa hebu tujuze zaidi- iko wapi, bei zikoje, installation charges, power, labour, etc. I AM INTERESTED.

Mitambo kama hiyo inapatikana kwa gharama nafuu kutoka visiwa vya Indonesia, Malasya na Singapore, na hata Korea. ila makampuni yanayouza sijafanya utafiti nakujusudia kufanya karibuni. Si lazima kuanza na mitambo mikubwa ya bei mbaya, bora kuwa na mitambo midogo ya kawaida tu ambayo gharama yake inaweza kuwa kati ya $1000-2500 hii ikiwa ni pamoja na gharama za shipping. Sidhani kama installation charges ni kitu cha kutisha kwa vile ni mtambo mdogo tu wa kuanzia, labda tatizo umeme wetu, inabidi uwe na standby generator.

Kadiri unavyofanikiwa ndivyo utakavyoona hitaji la kuongeza kipaato na huduma kwa kununua mtambo mkubwa zaidi kutokana na uzoefu wa uendeshaji na mafanikio ya biashara yako.

Napenda kushauri kwamba wengi tusifikirie tu retail tu, tufikirie uzindikaji wa vyakula ambavyo vimekuwa processed ndiyo njia ya kuingia kwenye ulimwengu wa Industrialized. Kama badala ya kuuza mchele kwenye meza bora kufanya packaging zenye lable zilizohakikiwa na idara ya viwango na kama biashara imeshamizi kuna uwezekano wa export.

Labor charges siona kama kitu cha kutisha Tanzania tukitilia maanani kuwa kima cha chini cha mshahara sekta binafsi ni kiwango cha kufikiwa na wengi kama umejiandaa vizuri, bora kufikiria zaidi upatikanaji wa mitambo na namna ya kuiendesha. Unaweza kufunzwa namna ya kuiendesha kabla hujaileta ndivyo wauzaji wengi wa kimataifa wanavyofanya.
 
Back
Top Bottom