Biashara ya toothpick, namna ambavyo charles forster aliweza kuwa millionaire

Biashara ya toothpick, namna ambavyo charles forster aliweza kuwa millionaire

Lasway.Jr

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2015
Posts
233
Reaction score
413
BIASHARA YA TOOTHPICK , Namna ambavyo Charles Forster aliweza kuwa millionaire .
Kutoka kwenye mji wa Boston Marekani mwaka 1826 alizaliwa kijana Charles Forster ambae alikuwa na kuanza kufanya Kazi na mjomba wake aliekuwa aagiza na kuuza mizigo Brazil kutokea marekani

Miaka ya 1700's watawa wanawawake kutoka ureno walikuwa wakitengeneza vijiti mithili ya toothpick na kuviuza Brazili kwa ajili ya kuondoa vitu kwenye meno wakati wa chakula , Charles alipoenda Brazil na kuona vijiti hivyo aliona ni fursa na alianza kuwaza kibiashara zaidi

Alirudi US na kuanza kuwaza namna ambavyo angetengeneza mashine ya kuchonga toothpick na kwenda kuziuza Brazil, hakuwa Mech Engineer lakini alipata idea na kumshikirisha jamaa yake mmoja Charles Freeman ambae alimsaidia kwenye kutengeneza mashine na kuchagua miti mizuri

Kwa ajili ya kutengeneza , na mwaka 1887 wakafanikiwa kutengeneza kiwanda kikubwa cha toothpick na kuanza uzalishaji , uzalishaji ulikuwa mkubwa na issue kubwa ikawa namna ya kuuza au masoko , jamaa alijaribu kwenda kwenye maduka na migahawa lakini hakuna aliemuelewa

Ilikuwa Changamoto kubwa sana kuuza product yake mpya , alichofanya ni kuitafutia product yake mpya patent right na mwaka 1891 aliweza kuipata na mwamba akaamua kuingia sokoni kwa njia ya kipekee kabisaa , unajua alichofanya ? Unaambiwa biashara ni ujanja sio akili bhnaa

Kwanza alizalisha mzgo wa kutosha akawa anapita kwenye maduka na store kuuza mzgo wake na alikataliwa , baada ya muda akawa anatuma watu kwenye maduka aliyopita kuuzia kwa kutaka kununua toothpick na walipokosa walikasirika sana na kuwaambia wenye maduka ni aibu kukosa bidhaa

Hiyo ya fahari kwenye maduka yao , baada ya muda jamaa anapita tena na wenye maduka wananunua bidhaa yake , baada ya muda alituma tena watu kwenda kwenye yale maduka na kununua zile toothpick na kumletea tena yeye na waliponunua wenye maduka walimwongezea order kubwa zaidi

Baadae akaanza kupita kwenye migahawa na kutangaza bidhaa yake na hawakununua , aliwachukua watu mashuhuri na kwenda nao kula kwenye migahawa mikubwa na walipomaliza kula waliuliza toothpick na walipokosa walikasirika sana na hii ikapelekea wenye migahawa kuagiza bidhaa kwa
Haraka na jamaa akauza sana ,

Next aliwatumia wanafunzi wa harvard university ambao walionekana watasha sana , baada ya kula kwenye migahawa waliulizia toothpick na zilipokosekana Basi walipiga kelele na kutukana huku wakisema hawatakuja tena kwenye hiyo migahawa kama hakuna

Toothpick, jamaa aliuza sana na kufikia kuzalisha toothpick elfu 70 kwa siku , kupitia watu maarufu akaanzisha mtindo wa kuweka toothpick mdomoni , kwa hiyo watu maarufu na vijana wakawa wanapiga picha nje ya hotel kubwa na kuweka toothpick mdomoni kuashiria wamekula kwenye

Hoteli hizo , lakini ushindani ulikuwa mkubwa bidhaa kutoka China na matumizi ya toothpick za plastic kutoka China basi kiwanda kikazota na kikafungwa mwaka 2003 kutoka mwaka 1870's

HALI YA SASA KWA TANZANIA
Sidhani kama Kuna kiwanda cha kutengeneza toothpick hapa tz japokuwa tunazitumia kila siku , kulikuwa na kiwanda kimoja cha KIJITI LTD sijui Kama sasa kinazalisha toothpick tena , karibia 80% ya toothpick tunazotunia zinatoka China or Imported

Toothpick nyingi hutengenezwa kwa miti hasa Mianzi "Bamboo" ambayo ipo mingi sana hapa kwetu tz na demand ya toothpick ni kubwa sana kwa sababu Zina matumizi kila siku , kidogo nisahau pia vijiti vingi vya kuchoma mishikaki na nyama huwa tuna import pia kutoka China[emoji1]



2006BB2609_charles_dickens_photograph.jpg
image%20(2).jpg
images%20(26).jpg
IMG_-s1br5m.jpg
download%20(4).jpg
download%20(5).jpg
 
BIASHARA YA TOOTHPICK , Namna ambavyo Charles Forster aliweza kuwa millionaire .
Kutoka kwenye mji wa Boston Marekani mwaka 1826 alizaliwa kijana Charles Forster ambae alikuwa na kuanza kufanya Kazi na mjomba wake muda alituma tena watu kwenda kwenye yale maduka na kununua zile toothpick na kumletea tena yeye na waliponunua wenye maduka walimwongezea order kubwa zaidi
Mpaka leo tunaagiza toothpick China, hii nchi imekuwa haina tofauti na kisiwa cha Comoro
 
Hapa Tanzania bamboo unazipata wapi!!! Kwanza hakuna watu wanaootesha bamboo kibiashara. China.....bamboo ni biashara kubwa, watu wanaotesha kibiashara kabisa.
Jaribu kufungua hicho kiwanda baada ya muda utakosa malighafi
Pia China kuna misitu mikubwa sana ya mianzi na mianzi yao ni mikubwa tofauti na yetu. Ila uzuri wa mianzi yetu ni kuwa inastahimili ukame na inatoa bidhaa nyingine, pombe.
Kupanda mianzi inawezekana kabisa. Kwanza duniani hakuna zao linakua haraka kama mianzi. Ni basi tu hatuna maarifa na mitaji.
 
Back
Top Bottom