Biashara ya Uchawi Tanzania

Wafanya biashara wa maduka ya rejareja, akija mama/baba na chupa iliyofungwa, akakupatia umpimie mafuta ya kula, usiifungue hiyo chupa, mrudishie huyo mama/baba aifungue yeye mwenyewe. Ukimrudishia hiyo chupa kama ni salama ataifungua, la sivyo atalalamika sana, mara hoo vijana wa siku hizi heshima hawana, mara hili na lile, ukweli ni kuwa hawezi kabisa kuifungua hiyo chupa, akianza kulalamika atakuwa anaondoka akisema maduka yapo mengi unafikiri ni wewe peke yako tu mwenye duka. Kumbuka siyo aina yoyote ya chupa, lazima iwe chupa ya kioo yenye mfuniko wa kujizungusha kama chupa zinazowekwa pombe kali.

Chupa za plastiki hizo hazina matatizo. Wachawi wa nchi wanatumia uchawi wao kupata pesa kwa njia za wizi, aina hii ya wizi wa kutumia majini huitwa chuma ulete. Majini haya huyatengeneza wao wenyewe, zipo aina ya majani na vitu vingi huchanganya pamoja na damu ya mnyama, huo mchanganyiko ukifikia hali fulani husomwa dua mbalimbali na machangiko huo hupatiwa jina kama Jumatatu, na kila siku mchawi anaita jina hilo mara tatu au nne akiwa karibu na huo mchanganyiko.

Baadaye hutumika aina mbalimbali za ubani na dua na ule mchanganyiko huwa ni pepo kamili, pepo hilo huingizwa ndani ya chupa kama moshi, ambao siyo rahisi kuona. Anapokupa hiyo chupa kuifungua, kawaida unapofungua chupa, unaiweka mbele karibu na uso wako, hivyo ule moshi ulio ndani ya chupa hutoka na kuingia ndani ya mwili wako.

Jumatatu akishaingia ndani ya mwili wako, mchawi akitaka kitu chochote dukani kwako atakichukua kirahisi sana. Anachofanya akifika dukani anaita tu jina la Jumatatu, lile pepo aliloliweka ndani yako huitika na kupanda, pepo likipanda wewe mwenye duka fahamu zinakutoka, analiangiza sasa nipimie mchele kilo 4, sukari kilo 1, unga kilo 5 akishapimiwa huondoka, na wewe mwenye duka huzinduka bila kujua chochote kilichofanyika, mara nyingine anaweza kuja na kuita Jumatatu nipe shilingi alfu ishirini, Jumatatu hupanda na kumpatia hizo pesa.

Hilo pepo linapanda linapoitwa na mchawi aliyelitengeneza peke yake, akija mtu mwingine na kuita Jumatatu pepo hilo halipandi kwani halimtambui.
 
Sasa ina maana ulaya /marekani hakuna uchawi?au kama upo huo uchawi wao ni wa kimaendeleo zaidi kuliko Afrika/Tanzania?
 
Sasa ina maana ulaya /marekani hakuna uchawi?au kama upo huo uchawi wao ni wa kimaendeleo zaidi kuliko Afrika/Tanzania?

Uchawi upo na wachawi wa kukata na shoka wapo, tofauti ni jinsi ya utendeji kazi, ulaya wanavaa suti, wanatumia ofisi zenye vitendea kazi vya kisasa, kama freemasons, Tanzania uchawi unafanyika kwenye mikeka ndani ya vibanda vya nyasi, tunaloga kila kitu, hadi mpapai.
 

Kazi ipo!!!
 
Hapo ndo nakupa big up Majimoto. Tengeneza pdf tafadhari ya part I ili tudownload. Najua hii haina mwisho kwani mambo haya ni mengi na yamefichika sana. Then partII, III, etc
 
 
Hapo ndo nakupa big up Majimoto. Tengeneza pdf tafadhari ya part I ili tudownload. Najua hii haina mwisho kwani mambo haya ni mengi na yamefichika sana. Then partII, III, etc

Mbona hata "Thanks" hamumugongei jamani?
 

Ooooooh YAHWE have mercy on us. Tusamehe maovu yetu Watanzania na uliponye taifa letu.

“Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na KUOMBA, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na KUIPONYA NCHI YAO” (2 Mambo ya Nyakati 7:14).
 

nilishawahi kusikia kitu kama hiki,ila chura huwa anatumika na pia wanafanyia ktk mazingira ya maji ya kutiririka mtoni etc wakati wanaandaa hiyo chuma ulete.
 
Majimoto unasema vitu vingi vya kimaendeleo tunavyotumia vinatokana na ujuzi wa kuzimu. na komputa? Kwa hiyo sisi wote tunaotumia ukiwemo na wewe huoni kwamba nia mawakala wa kuzimu hapa dunia?
Vipi kuhusu ushoga kwani sku hizi nchi nying za Ulaya na Marekani wanaupigia kelele. Hauna uhusiano wowote na kuzimu au ushetani?
 
Vipi kuhusu wachawi wanaofanya watu wa kawaida kuwa invisible? yeye anajiona kawaida kumbe watu wanaomzunguka hawamuoni?
 
maji moto vipi mama ntilie kupakua chakula na mkono wa mtu ukitumika kama kijiko, hii ni kweli?
 
jamani hata singida? dah, mbeya nimeishi sana, wanakaba usiku ukilala si mchezo, ukifunga ndoa jiandae vimbwanga watakavyokuonea wivu...
 
Vipi kuwa na laki moja halafu unaitumia yote lakini kiukweli umetumia elfu 40 the rest zimetambaa kwa mtu mwingine. lakini calcualtion zako zinabalance ktk ulimwengu wa kawaida.
 
Majimoto bado upo maktaba nini? Au maswali ni magumu? Nimepita kuchungulia tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…