Biashara ya ukopeshaji pesa kwa riba

Biashara ya ukopeshaji pesa kwa riba

Kwanza hii biashara hutakiwi kuwa na roho ya huruma Nina dada angu anaifanya mwaka wa nane na ndio biashara inayomuweka mjini

Anakopesha kuanzia 10000 mwisho laki tatu. Riba anafanya asilimia 50 ndani ya mwezi mmoja. Anayekopesha lazima aweke kitu na hicho kitu analetewa sio abaki nacho mkopaji , vitu anavyopokea vifaa vya umeme mfano TV, radio , pasi nk.

Vito vya thamani dhahabu , silver , tanzanite nk kabla ya kumpa mteja pesa anaenda kuvipima kujua thamani yake ana sonara yake maalum.

Hapokei kiwanja Wala hati ya nyumba, anayeleta pikipiki au gari anaacha na kadi.

Anavyokopesha mfano mtu akiwa shida na laki , anatakiwa aweke vitu vyenye thamani ya laki na nusu pamoja anajumlishia na thamani ya riba. Anamletea ikifika muda wa malipo asipoliopa anaweza akamletea faida 50000 Deni Lina baki palepale, mkopaji akikaa kimya mfano miezi miwili anampigia simu muhsika kumuuliza vp akiwa Hana jibu anamwambia tumemalizana Basi vitu vyako nauza Mimi na wewe tumemalizana.

Unakuta mtu labda kamuachia flat screen nch 32 kapewa laki moja so hata akiuza laki nanusu yeye faida yake ipo

Kikubwa uwe makini na vitu wanavyoleta wateja ni biashara nzuri ila yahitaji umakini wa Hali ya juu.
Ndugu mleta mada tulia bana.
Halafu ujue wenzako wengi wamesitisha kukopesha hata zile giant companies zimesitisha.
 
Siku hizi biashara hii haifanywi holela kama zamani.

Ni lazima usajiliwe na utimize vigezo vyote vilivyoanishwa.

Utapewa licence ndipo utakapoweza kuifanya kwa mujibu wa sheria.

Hii inakupa ulinzi hata wewe mwenyewe mtu akikudhulumu utakuwa na uwezo wa kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hebu nipe muongozo wa hili suala.Nianzie wapi?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom