Biashara ya umaarufu "fame" inalipa zaidi nyakati hizi

Mwabhleja

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2016
Posts
1,351
Reaction score
2,061
Amini usiamini habari ndiyo hiyo tajwa hapo juu.
Biashara nyingi zina changamoto kubwa sana kutokana na mfumuko wa bei pamoja na kushuka kwa kiwango cha manunuzi "Purchasing Power katika jamii"

Lakini biashara ya umaarufu ni moja kati ya biashara zinazokua kwa kasi sana na mahitaji ya watu maarufu ni makubwa sana nchini Tanzania.

Mabadiliko makubwa yamejitokeza katika sekta ya mawasiliano na matangazo ya kibiashara jambo lililopelekea kuwepo kwa aina mpya ya uhitaji wa huduma za mawasiliano baina ya watoa huduma na wapokea huduma.

Mfano, watu binafsi waliofanikiwa kuutumia umaarufu kujiingizia kipato kutokana na huduma ya matangazo, ambassadors na posting ni Maulid Kitenge, Eddo Kumwembe, Idris Sultan, Harmorapa na MC PILIPILI.

Pia wasanii wengi hutumia umaarufu wao kujiingizia kipato nje ya kazi zao rasmi.
Mtu mwelewa na mwenye elimu nzuri ana nafasi nzuri ya kuingiza kipato kupitia mitandao ya kijamii.

Ieleweke kwamba, makampuni mengi ya kibiashara na kijamii hukwepa gharama za kutangaza kupitia runinga na redio hivyo hutumia mitandao ya kijamii na kuwatumia watu maarufu kufikisha jumbe zao.

Ndugu yangu, kama una chochote halali kinachoweza kukufanya uwe maarufu tafadhari itumie nafasi hiyo kukifanya hicho kitu maana utavuna zaidi ya unavyotarajia.

Taifa linahitaji watu maarufu watakaobeba majukumu ya kutangaza huduma na bidhaa mbalimbali mfano, sigara, bia, nguo, vifaa vya ujenzi, usafirishaji, mawasiliano na ubalozi mbalimbali hususani katika masuala ya mazingira, demokrasia, kilimo, masuala ya kijinsia na imani za kidini.

Just guess, Dr.Shika aliweza kuingiza chochote kitu kupitia 900 ITAPENDEZA.
Hivi wewe huna kipaji chochote kinachoweza kukufanya ukawa maarufu na kuanza kupiga mpunga taratibu.

Binafsi ukiacha masuala yangu ya kazi na shughuli zangu ndogo ndogo nimegundua kuna hela yangu sehemu sijaanza kuichuma.
Nipo kwenye mpango wa kuwa maarufu katika jambo fulani linalohusiana na Show Off.
Kuna mama anapiga danadana na anaizunguka dunia kupitia umaarufu alioupata kupitia danadana.
Ikumbukwe kwamba kuwa na kipaji kigezo cha umaarufu lakini kukijua kipaji cha
Ko ni mwanzo wa umaarufu.

Karibuni tujuzane fursa za umaarufu na mikakati ya kuwa maarufu.
KAZI NI MOYO!
 
Yes you can,
Hii nchi ina watu wengi wanaohitaji huduma yako. Bila shaka mimi nitakuwa wa kwanza kukupa support!
Hata mimi nauona u-fame ndani yangu[emoji41][emoji41]lazima nifanye jambo hata ubalozi wa diapers jomonii kama sio mambo ya maakuli[emoji4][emoji4]Ila kwa hivyo ulivyovitaja nimetamani ubalozi wa sigara[emoji854]
 
Bado haiwalipi kihivyo mana wasanii wenyewe wanapenda kuishi maish ya gharama wewe angalia mtu kama hamisa tangazo moja anaweza akapewa hadi mil 5 lakini matumizi ni makubwa kuliko anachopata
kodi ya nyumba,mavazi,kukodi magari
 
Suala la matumizi linatokana na anaingiza ngapi maana huwezi tumia mia tano kama unaingiza mia mbili.
Pia wengi wana biashara mtambuka. Ukiacha hilo kuna issue ya personal brand management ni moja kati ya mambo ya msingi kuanzia kwenye mavazi, lugha, makazi na mwonekano wa sura ya mtu mashuhuri.
Mtu kama Dr.Shika hakuwa na personal brand manager mzuri wa kuendeleza alipofikia kitu kilichosababisha umaarufu wake kushuka.
Vile vile umaarufu unaweza kushuka kutokana na kiwango kidogo cha ufahamu kukuhusu wewe mwenyewe hivyo kujikuta hujielewi ufanye nini na umaarufu ulio nao.
Kwahiyo, fursa hii isiachwe ikaenda bure!
Bado haiwalipi kihivyo mana wasanii wenyewe wanapenda kuishi maish ya gharama wewe angalia mtu kama hamisa tangazo moja anaweza akapewa hadi mil 5 lakini matumizi ni makubwa kuliko anachopata
kodi ya nyumba,mavazi,kukodi magari
 
Mkuu upo sahihi kwa kiwango fulani.
Kazi yoyote au biashara yoyote inayohusu umaarufu huwa si ya kudumu bali ni ya msimu tu.
Kwa hyo usikosoe kuhusu umaarufu wa Dr. Shika kwamba uliisha kwa kukosa brand manager bali muda wake tu wa umaarufu umekwisha.
Dr Shika Kuna kipindi alikuwa akiitwa kwenye event yoyote alikuwa anapelekwa na managers wanaomsimamia.
Ila shuda ilipo ni kwamba hao brand managers wa wasanii unaowaongelea kazi yao pia hufanywa hvyo hvyo kisanii.
Kazi yao huwa ni kufanya timing mahali ambapo wanaona Kuna fursa ya kupiga pesa then ukichuja wanapotea yaani kiufupi hakuna mtu atakusapoti moja kwa moja miaka yote.
Kwa hyo wale mameneja wa Dr. Shika Sasa hv wanadili na Pierre Liquid huyo Shika washamsahau.
 
Nimekuelewa vema mkuu!
 
Kutengeneza jina ni safari ndefu,ukiwaangalia kina mpoki walipotoka mpaka Leo hii taiga linatambua uwepo wao hakika wamekwepa mishale mingi
 
Kutengeneza jina ni safari ndefu,ukiwaangalia kina mpoki walipotoka mpaka Leo hii taiga linatambua uwepo wao hakika wamekwepa mishale mingi
Ni kweli mkuu,sio kitu Cha kukurupuka tu eti useme kuanzia leo mm nakuwa maarufu.
Otherwise labda umaarufu wako uwe wa kipumbavu na kujitoa ufaham Kama akina Maryam biriani,Pierre Liquid,Amber ruty.
 
Ni kweli mkuu,sio kitu Cha kukurupuka
tu eti useme kuanzia leo mm nakuwa maarufu.

Otherwise labda umaarufu wako uwe
wa kipumbavu na kujitoa ufaham Kama akina Maryam biriani,Pierre
Liquid,Amber ruty.
Sahihi mkuu.
 
Sahihi mkuu.
Ww angalia wakina mpoki walihustle miaka Zaid ya 10.
Na wakat huo walionekana Kama wanacheza tu au walionekana wamekosa kazi ya kufanya au kituko ktk jamii.
Lakini leo hii wanatamba na kuonekana matajiri.
Sasa mwingine asiyejua anafikir walikurupuka tu na kuibuka na umaarufu.
 
Kuwa maarufu sometimes ni vigumu,lkn kwanini MTU usitumie watu maarufu kupata pesa!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…