Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
Amini usiamini habari ndiyo hiyo tajwa hapo juu.
Biashara nyingi zina changamoto kubwa sana kutokana na mfumuko wa bei pamoja na kushuka kwa kiwango cha manunuzi "Purchasing Power katika jamii"
Lakini biashara ya umaarufu ni moja kati ya biashara zinazokua kwa kasi sana na mahitaji ya watu maarufu ni makubwa sana nchini Tanzania.
Mabadiliko makubwa yamejitokeza katika sekta ya mawasiliano na matangazo ya kibiashara jambo lililopelekea kuwepo kwa aina mpya ya uhitaji wa huduma za mawasiliano baina ya watoa huduma na wapokea huduma.
Mfano, watu binafsi waliofanikiwa kuutumia umaarufu kujiingizia kipato kutokana na huduma ya matangazo, ambassadors na posting ni Maulid Kitenge, Eddo Kumwembe, Idris Sultan, Harmorapa na MC PILIPILI.
Pia wasanii wengi hutumia umaarufu wao kujiingizia kipato nje ya kazi zao rasmi.
Mtu mwelewa na mwenye elimu nzuri ana nafasi nzuri ya kuingiza kipato kupitia mitandao ya kijamii.
Ieleweke kwamba, makampuni mengi ya kibiashara na kijamii hukwepa gharama za kutangaza kupitia runinga na redio hivyo hutumia mitandao ya kijamii na kuwatumia watu maarufu kufikisha jumbe zao.
Ndugu yangu, kama una chochote halali kinachoweza kukufanya uwe maarufu tafadhari itumie nafasi hiyo kukifanya hicho kitu maana utavuna zaidi ya unavyotarajia.
Taifa linahitaji watu maarufu watakaobeba majukumu ya kutangaza huduma na bidhaa mbalimbali mfano, sigara, bia, nguo, vifaa vya ujenzi, usafirishaji, mawasiliano na ubalozi mbalimbali hususani katika masuala ya mazingira, demokrasia, kilimo, masuala ya kijinsia na imani za kidini.
Just guess, Dr.Shika aliweza kuingiza chochote kitu kupitia 900 ITAPENDEZA.
Hivi wewe huna kipaji chochote kinachoweza kukufanya ukawa maarufu na kuanza kupiga mpunga taratibu.
Binafsi ukiacha masuala yangu ya kazi na shughuli zangu ndogo ndogo nimegundua kuna hela yangu sehemu sijaanza kuichuma.
Nipo kwenye mpango wa kuwa maarufu katika jambo fulani linalohusiana na Show Off.
Kuna mama anapiga danadana na anaizunguka dunia kupitia umaarufu alioupata kupitia danadana.
Ikumbukwe kwamba kuwa na kipaji kigezo cha umaarufu lakini kukijua kipaji cha
Ko ni mwanzo wa umaarufu.
Karibuni tujuzane fursa za umaarufu na mikakati ya kuwa maarufu.
KAZI NI MOYO!