Salute wakuu..
Natumaini wote mko poa.. Leo naomba ni-shee na nyie huu mradi mdogo kama jinsi watu wanavyoweza kuuona lkn kwa kiasi fulani unawaingizia watu mkwanja wa nguvu na wanalisha familia kama kawaida, sio lazima wewe uufanye huu mradi, la hashaa......!!
Ila unaweza kumshauri mtu akaufanya kupitia mawazo haya ama na wewe ukaboresha zaidi... {mwisho wa huu uzi nimekuwekea file unaweza kulipakua na kujisomea ama kumuonesha mtu unayetaka afanye huu mradi} haya twende sasa
MRADI WA KUTENGENEZA MAANDAZI.
Mradi huu utahusisha utengenezaji wa vitafunwa aina ya maandazi na kuyasambaza maduka mbali mbali kwa ajili ya kununuliwa na wateja. Hivi ni vitafunwa vinavyojulikana na wengi mijini na vijijni.
Vitafunwa hivi hutengenezwa na ngano inayouzwa madukani pamoja na mchangavyiko wa viungo vingine mahsusi. Ni mradi mdogo sana kwa kuutizama lakini kama ukifanywa kwa umakini unafaida kubwa na inaweza hata kumpatia mtengenezaji pesa nyingi.
Usambazaji
Kama nilivyoainisha awali kuwa hii biashara itafanyika kwa kuweka maandazi haya madukani {maduka ya kawaida kwa kuwaomba marafiki na hata kuwa na makubaliano fulani}. Kwa mfano hapa mtengenezaji atakuwa na madeli {makontena} madogo kumi {10 ama pungufu} ambayo kila moja wapo litakuwa na maadazi 100.
Yote haya yata wekwa maduka tofauti tofauti kwa makubaliano Fulani Fulani na muuzaji. Hapa ujanja wa kuweka maandazi ma2 ama ma3 kwa kila deli ili kumpatia muuzani nae atafute kama ujira wake. ππ ama unaweza kutafuta watu/madogo wakawa wanakuuzia mashuleni hasa shule za msingi... n.k
Utengenezaji
Maandazi yatatengenezwa na msambazaji mwenyewe kwa mikono yake ili kuepuka gharama kubwa za uwekezaji huu. Vifaa vitanunuliwa humu humu ndani ya masoko yetu ili kuepuka gharama za uzalishaji na kujihakikishia faida kubwa.
Mbinu za kuyafanya yauzike.
Kwa sababu huu ni ujasiriamali makini, sasa ili kuifanya hii bidhaa iuzike ni muhimu kuwa mbunifu. Nazani inaeleweka kuwa vipo aina nyingi ya vitafunwa madukani vizuri tuu lakini ni vema kuyafanya maandazi haya yakauzika mapema na haraka ili kuufanya mzunguko wa biashara uwe mzuri na wa haraka zaidi.
Kwa mfano size ya andazi iwe ya kuridhisha kulingana na gharama za ununuzi wa bidhaa {kuepuka tamaa}, kuweka viungo ili angalau andazi liwe na harufu na radha ya kuvutia, kuweka tui la nazi, maandazi yakae katika hali ya usafi yaani yakae ndani ya deli linalo yaonesha {transparent} lililofunikwa na pia ili kuepuka mandazi yasiwe na unyevu nyevu ni vema deli likatobolewa matundu kiasi ili kupitisha hewa.
Ifutayo ni mchanganuo wa bajeti na mambo mengineyo ya jinsi ya kuifanya hii biashara kuwa na faida kubwa.
Gharama za awali,mchanganuo, faida na changamoto
{WAKUU HAPA NAOMBA M-DOWNLOAD FILE NIMELIWEKA HAPO CIINI NAONA HAPA MAJEDWALI HAYAKAI VEMA}
Changamoto.
Bithaa hii ikiwa sokoni itakutana na bidhaa nyingine kama hizi, kwa hiyo ni vema ubunifu wa hali ya juu ukatumia ili kuifanya biashara hii kuwa ya kipekee na kupendwa na watu.
Mpango na idadi ya mauzo kwa siku,mwezi,mwaka na FAIDA katika mradi.
{WAKUU HAPA NAOMBA M-DOWNLOAD FILE NIMELIWEKA HAPO CHINI NAONA HAPA MAJEDWALI HAYAKAI VEMA}
MWISHO
Uzuri wa biashara hii ni kuwa haiitaji mtaji mkubwa saaaana yani hata laki nne haifiki kwa kuanzia. lakini pia unaweza kubuni mbinu ya kuyaweka maandazi yako mashuleni ambapo kama yakopoa madogo janja lazima wayanunue sana.
MWISHO KABISA
Ukiangalia kwenye hilo file labda kuna hesabu zimekosewa kwa njia moja ama nyingine lkn napenda kuwafungua macho watu waliokuwa wanaichukulia poa hii biashara, labda niwaambie mama yangu mzazi mimi kwa % Fulani kanilea mimi na ndugu zangu wengine kwa biashara ya maandazi.
Sasa wewe mdau ni kazi yako wewe kusuka ama kunyoa. Ikumbukwe huu mradi unaweza kuufaya na vijana wako home hata kama unafanya kazi kwa {DEREVA WA ROLI} Λββ Usini-quote tafadhali.
Nakaribisha
*maoni
*marekebisho
*matusi hapana {Sikaribishi}
*chochote
Salute Wakuu