Biashara ya Uokaji (Bakery): Mbinu, Ushauri na Changamoto Zake

Biashara ya Uokaji (Bakery): Mbinu, Ushauri na Changamoto Zake

Naked truth...ila kwa pm umeharibu,
Usije enda mwambia kuwa huwa mna kanda unga
Kwa visigino na jasho likiwatoka kama waona mikate ya kukanda.


Hii biashara kama ndo unaanza kabisa ni kazi kidogo kwa upande wa vifaa ila ukisha kua navyo ni mwendo wa kuingiza pesa tuu. Vifaa utakavyohitaj vya muhim
*Mixer
*Oven
*Masufuria
*Mabomba au karatas za kudecorate
*Nozzles

Hapo hujawek mazaga yanayotumik kutengenezea keki kama ngano, sukar n.k

Changamoto zilizokuepo kwenye hii biashara n wateja kukuzoea au kukuamini! Watu wenye jina ndio wanapata fursa nyingi tofauti na wasio na jina, so kama unaanza hakikisha unatengeneza vitu high quality, pesa utakuj piga mbele huko! Niko Dar, ukitak tukutane nkuwek waz zaid ni pm!
 
Hii biashara kama ndo unaanza kabisa ni kazi kidogo kwa upande wa vifaa ila ukisha kua navyo ni mwendo wa kuingiza pesa tuu. Vifaa utakavyohitaj vya muhim
*Mixer
*Oven
*Masufuria
*Mabomba au karatas za kudecorate
*Nozzles

Hapo hujawek mazaga yanayotumik kutengenezea keki kama ngano, sukar n.k

Changamoto zilizokuepo kwenye hii biashara n wateja kukuzoea au kukuamini! Watu wenye jina ndio wanapata fursa nyingi tofauti na wasio na jina, so kama unaanza hakikisha unatengeneza vitu high quality, pesa utakuj piga mbele huko! Niko Dar, ukitak tukutane nkuwek waz zaid ni pm!
Inahitaji mtaji kiasi gani ndo uweze kununua hivyo vifaa vyote?
 
Kama milion moj na nusu hv, ila ukipata oda za harus kama nne, pesa yako inarud!
 
Vp kuhusu vifaa vya kutengeneza half cake za kuuza mtaani navyo vinagarimu kuasi gani
Hapo inabd uwe na jiko kubwa ili upike kwa trei(kama n za kukata) au upike cup cake nying kwa wakt mmoja! Hayo majiko yapo kuanzia milion moja na nusu had milioni nne! Mixer inabd uwe nayo ya milioni moja na nusu, so ukiwa na milioni tatu inatosha!
 
Hapo inabd uwe na jiko kubwa ili upike kwa trei(kama n za kukata) au upike cup cake nying kwa wakt mmoja! Hayo majiko yapo kuanzia milion moja na nusu had milioni nne! Mixer inabd uwe nayo ya milioni moja na nusu, so ukiwa na milioni tatu inatosha!
Asante mkuu
 
Tatizo watengeza keki hawana ubunifu kabisa ni kuigana tuu.....ladha ile ile wanatofautiana decorations tuu.... akitokea mwenye ubunifu na aliye tayari kujaribu atapata mafanikio sana.
 
Kama milion moj na nusu hv, ila ukipata oda za harus kama nne, pesa yako inarud!
Millioni 1 na nusu haiwezi tosha. hiyo labda just kwa matumizi ya nyumbani. ila kwa biashara inaweza chukua mpaka 12Million
 
Amani iwe kwenu wanaJF

Kama heading inavosomeka katika safari ya kutaka kujikomboa na umasikini nimetokea sana kuipendenda hii business ya Uokaji mikate, na catering kwa ujumla

Mwenye ujuzi wa hii biashara naomba msaada ina changamoto ipi, Mtaji kiasi gani unahitajika.

Upatikanaji wa viafaa bei yake ikoje ni aina gani ambavyo ni vizuri n.k

Nini cha kufanya ili kuifanya biashara iwe bora na ikue kwa haraka.

Natumai nitapata muongozo mzuri kutoka kwa wazoefu

Nawasilisha

BM
 
Salute wakuu..
Natumaini wote mko poa.. Leo naomba ni-shee na nyie huu mradi mdogo kama jinsi watu wanavyoweza kuuona lkn kwa kiasi fulani unawaingizia watu mkwanja wa nguvu na wanalisha familia kama kawaida, sio lazima wewe uufanye huu mradi, la hashaa......!!

Ila unaweza kumshauri mtu akaufanya kupitia mawazo haya ama na wewe ukaboresha zaidi... {mwisho wa huu uzi nimekuwekea file unaweza kulipakua na kujisomea ama kumuonesha mtu unayetaka afanye huu mradi} haya twende sasa

MRADI WA KUTENGENEZA MAANDAZI.
Mradi huu utahusisha utengenezaji wa vitafunwa aina ya maandazi na kuyasambaza maduka mbali mbali kwa ajili ya kununuliwa na wateja. Hivi ni vitafunwa vinavyojulikana na wengi mijini na vijijni.

Vitafunwa hivi hutengenezwa na ngano inayouzwa madukani pamoja na mchangavyiko wa viungo vingine mahsusi. Ni mradi mdogo sana kwa kuutizama lakini kama ukifanywa kwa umakini unafaida kubwa na inaweza hata kumpatia mtengenezaji pesa nyingi.

Usambazaji
Kama nilivyoainisha awali kuwa hii biashara itafanyika kwa kuweka maandazi haya madukani {maduka ya kawaida kwa kuwaomba marafiki na hata kuwa na makubaliano fulani}. Kwa mfano hapa mtengenezaji atakuwa na madeli {makontena} madogo kumi {10 ama pungufu} ambayo kila moja wapo litakuwa na maadazi 100.

Yote haya yata wekwa maduka tofauti tofauti kwa makubaliano Fulani Fulani na muuzaji. Hapa ujanja wa kuweka maandazi ma2 ama ma3 kwa kila deli ili kumpatia muuzani nae atafute kama ujira wake. 🙂🙂 ama unaweza kutafuta watu/madogo wakawa wanakuuzia mashuleni hasa shule za msingi... n.k

Utengenezaji
Maandazi yatatengenezwa na msambazaji mwenyewe kwa mikono yake ili kuepuka gharama kubwa za uwekezaji huu. Vifaa vitanunuliwa humu humu ndani ya masoko yetu ili kuepuka gharama za uzalishaji na kujihakikishia faida kubwa.

Mbinu za kuyafanya yauzike.

Kwa sababu huu ni ujasiriamali makini, sasa ili kuifanya hii bidhaa iuzike ni muhimu kuwa mbunifu. Nazani inaeleweka kuwa vipo aina nyingi ya vitafunwa madukani vizuri tuu lakini ni vema kuyafanya maandazi haya yakauzika mapema na haraka ili kuufanya mzunguko wa biashara uwe mzuri na wa haraka zaidi.

Kwa mfano size ya andazi iwe ya kuridhisha kulingana na gharama za ununuzi wa bidhaa {kuepuka tamaa}, kuweka viungo ili angalau andazi liwe na harufu na radha ya kuvutia, kuweka tui la nazi, maandazi yakae katika hali ya usafi yaani yakae ndani ya deli linalo yaonesha {transparent} lililofunikwa na pia ili kuepuka mandazi yasiwe na unyevu nyevu ni vema deli likatobolewa matundu kiasi ili kupitisha hewa.

Ifutayo ni mchanganuo wa bajeti na mambo mengineyo ya jinsi ya kuifanya hii biashara kuwa na faida kubwa.
Gharama za awali,mchanganuo, faida na changamoto

{WAKUU HAPA NAOMBA M-DOWNLOAD FILE NIMELIWEKA HAPO CIINI NAONA HAPA MAJEDWALI HAYAKAI VEMA}

Changamoto.
Bithaa hii ikiwa sokoni itakutana na bidhaa nyingine kama hizi, kwa hiyo ni vema ubunifu wa hali ya juu ukatumia ili kuifanya biashara hii kuwa ya kipekee na kupendwa na watu.

Mpango na idadi ya mauzo kwa siku,mwezi,mwaka na FAIDA katika mradi.
{WAKUU HAPA NAOMBA M-DOWNLOAD FILE NIMELIWEKA HAPO CHINI NAONA HAPA MAJEDWALI HAYAKAI VEMA}

MWISHO
Uzuri wa biashara hii ni kuwa haiitaji mtaji mkubwa saaaana yani hata laki nne haifiki kwa kuanzia. lakini pia unaweza kubuni mbinu ya kuyaweka maandazi yako mashuleni ambapo kama yakopoa madogo janja lazima wayanunue sana.

MWISHO KABISA
Ukiangalia kwenye hilo file labda kuna hesabu zimekosewa kwa njia moja ama nyingine lkn napenda kuwafungua macho watu waliokuwa wanaichukulia poa hii biashara, labda niwaambie mama yangu mzazi mimi kwa % Fulani kanilea mimi na ndugu zangu wengine kwa biashara ya maandazi.

Sasa wewe mdau ni kazi yako wewe kusuka ama kunyoa. Ikumbukwe huu mradi unaweza kuufaya na vijana wako home hata kama unafanya kazi kwa {DEREVA WA ROLI} ˂≈≈ Usini-quote tafadhali.

Nakaribisha
*maoni
*marekebisho
*matusi hapana {Sikaribishi}
*chochote

Salute Wakuu
 

Attachments

Samahani hivi mashine (local) ya kukandia unga wa ngano naweza ipata wapi ?
 
Nilishawahi kuwaza plan kama hii, ni plan nzuri yenye return kubwa. Big up sana kwa kuliona hilo
 
Nzuri.. Tho kuna competition na yale maandazi fulani makubwa hivi sijui ya azam yale..
 
Back
Top Bottom