Salaams JF,
Nilipata wazo la kuanzisha bakery maeneo ya sinza. Products ni ; Mikate, Maandazi na cakes aina mbalimbali. Sikuomba au kutafuta ushauri kwa mtu yeyote. Pia sijafanya research ya uhakika kuhusu mahitaji halisi ya hizo bidhaa ninazotaka kuingiza sokoni. Pia sijafanya utafiti kuhusu ushindani wa hii biashara. Nimeamua kuchukua RISK 100% katika kuwekeza huko kwenye bakery. Kwahiyo bado sijaelewa / sijajua kama nipo njia sahihi au nimekosea. Naomba ushauri na uelewa wenu kwenu hii biashara.
Hadi sasa nimefanikiwa kupata vitu vifuatavyo;
- Machines- 3 Ovens ( moja kubwa inaingiza paltes 6 na nyingine mbili ni ndogo zinaingiza plates 2 kila moja); 1 Mixer aina ya B30; Shelf; 30 Oven Plates,
-Nimepanga Jengo na kulifanyia ukarabati kulingana na mahitaji ya kazi.
-Nimesajili jina la biashara
-Nimeshapata na TIN
-Nimeshapata leseni
Vitu vinavyohitajika kwa sasa ni;
-Connecting service line ( electricity) kwenye jengo ambalo nimeshafanya wiring
-TFDA authorization
-Source of more finance
-Hard working, knowledgeable and skilled person ( Baker) ambaye ataweza kutengeneza bidhaa mbalimbali
-Bread slicer
-Manager and cashier
-Marketing and sales person
-Distributor
Je mnaonaje wakuu? Je nipo sahihi? Nawakilisha
===========
SIMILAR CASES:
===========
Jan 19, 2012: