Biashara ya Uokaji (Bakery): Mbinu, Ushauri na Changamoto Zake

Biashara ya Uokaji (Bakery): Mbinu, Ushauri na Changamoto Zake

Imekaa poowah sana.

All the best ndugu.
Salute wakuu..
Natumaini wote mko poa.. Leo naomba ni-shee na nyie huu mradi mdogo kama jinsi watu wanavyoweza kuuona lkn kwa kiasi fulani unawaingizia watu mkwanja wa nguvu na wanalisha familia kama kawaida, sio lazima wewe uufanye huu mradi, la hashaa......!!

Ila unaweza kumshauri mtu akaufanya kupitia mawazo haya ama na wewe ukaboresha zaidi... {mwisho wa huu uzi nimekuwekea file unaweza kulipakua na kujisomea ama kumuonesha mtu unayetaka afanye huu mradi} haya twende sasa

MRADI WA KUTENGENEZA MAANDAZI.
Mradi huu utahusisha utengenezaji wa vitafunwa aina ya maandazi na kuyasambaza maduka mbali mbali kwa ajili ya kununuliwa na wateja. Hivi ni vitafunwa vinavyojulikana na wengi mijini na vijijni.

Vitafunwa hivi hutengenezwa na ngano inayouzwa madukani pamoja na mchangavyiko wa viungo vingine mahsusi. Ni mradi mdogo sana kwa kuutizama lakini kama ukifanywa kwa umakini unafaida kubwa na inaweza hata kumpatia mtengenezaji pesa nyingi.

Usambazaji
Kama nilivyoainisha awali kuwa hii biashara itafanyika kwa kuweka maandazi haya madukani {maduka ya kawaida kwa kuwaomba marafiki na hata kuwa na makubaliano fulani}. Kwa mfano hapa mtengenezaji atakuwa na madeli {makontena} madogo kumi {10 ama pungufu} ambayo kila moja wapo litakuwa na maadazi 100.

Yote haya yata wekwa maduka tofauti tofauti kwa makubaliano Fulani Fulani na muuzaji. Hapa ujanja wa kuweka maandazi ma2 ama ma3 kwa kila deli ili kumpatia muuzani nae atafute kama ujira wake. 🙂🙂 ama unaweza kutafuta watu/madogo wakawa wanakuuzia mashuleni hasa shule za msingi... n.k

Utengenezaji
Maandazi yatatengenezwa na msambazaji mwenyewe kwa mikono yake ili kuepuka gharama kubwa za uwekezaji huu. Vifaa vitanunuliwa humu humu ndani ya masoko yetu ili kuepuka gharama za uzalishaji na kujihakikishia faida kubwa.

Mbinu za kuyafanya yauzike.

Kwa sababu huu ni ujasiriamali makini, sasa ili kuifanya hii bidhaa iuzike ni muhimu kuwa mbunifu. Nazani inaeleweka kuwa vipo aina nyingi ya vitafunwa madukani vizuri tuu lakini ni vema kuyafanya maandazi haya yakauzika mapema na haraka ili kuufanya mzunguko wa biashara uwe mzuri na wa haraka zaidi.

Kwa mfano size ya andazi iwe ya kuridhisha kulingana na gharama za ununuzi wa bidhaa {kuepuka tamaa}, kuweka viungo ili angalau andazi liwe na harufu na radha ya kuvutia, kuweka tui la nazi, maandazi yakae katika hali ya usafi yaani yakae ndani ya deli linalo yaonesha {transparent} lililofunikwa na pia ili kuepuka mandazi yasiwe na unyevu nyevu ni vema deli likatobolewa matundu kiasi ili kupitisha hewa.

Ifutayo ni mchanganuo wa bajeti na mambo mengineyo ya jinsi ya kuifanya hii biashara kuwa na faida kubwa.
Gharama za awali,mchanganuo, faida na changamoto

{WAKUU HAPA NAOMBA M-DOWNLOAD FILE NIMELIWEKA HAPO CIINI NAONA HAPA MAJEDWALI HAYAKAI VEMA}

Changamoto.
Bithaa hii ikiwa sokoni itakutana na bidhaa nyingine kama hizi, kwa hiyo ni vema ubunifu wa hali ya juu ukatumia ili kuifanya biashara hii kuwa ya kipekee na kupendwa na watu.

Mpango na idadi ya mauzo kwa siku,mwezi,mwaka na FAIDA katika mradi.
{WAKUU HAPA NAOMBA M-DOWNLOAD FILE NIMELIWEKA HAPO CHINI NAONA HAPA MAJEDWALI HAYAKAI VEMA}

MWISHO
Uzuri wa biashara hii ni kuwa haiitaji mtaji mkubwa saaaana yani hata laki nne haifiki kwa kuanzia. lakini pia unaweza kubuni mbinu ya kuyaweka maandazi yako mashuleni ambapo kama yakopoa madogo janja lazima wayanunue sana.

MWISHO KABISA
Ukiangalia kwenye hilo file labda kuna hesabu zimekosewa kwa njia moja ama nyingine lkn napenda kuwafungua macho watu waliokuwa wanaichukulia poa hii biashara, labda niwaambie mama yangu mzazi mimi kwa % Fulani kanilea mimi na ndugu zangu wengine kwa biashara ya maandazi.

Sasa wewe mdau ni kazi yako wewe kusuka ama kunyoa. Ikumbukwe huu mradi unaweza kuufaya na vijana wako home hata kama unafanya kazi kwa {DEREVA WA ROLI} ˂≈≈ Usini-quote tafadhali.

Nakaribisha
*maoni
*marekebisho
*matusi hapana {Sikaribishi}
*chochote

Salute Wakuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimejaribu kutafuta threads zinazozungumzia hizo biashara mbili sijaziona,hebu wazoefu njooni tujadili hizo biashara hasa tukiangalia kiasi cha mtaji cha kuanza nacho na changamoto zake.

Kwa mfano ukataka kuanzisha dodoma,je ushindani uko vp huko!?je ni biashara inayokutaka muda wote uwepo sehem husika!?
Biashara ipi mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amani iwe kwenu wanaJF

Kama heading inavosomeka katika safari ya kutaka kujikomboa na umasikini nimetokea sana kuipendenda hii business ya Uokaji mikate, na catering kwa ujumla

Mwenye ujuzi wa hii biashara naomba msaada ina changamoto ipi, Mtaji kiasi gani unahitajika.

Upatikanaji wa viafaa bei yake ikoje ni aina gani ambavyo ni vizuri n.k

Nini cha kufanya ili kuifanya biashara iwe bora na ikue kwa haraka.

Natumai nitapata muongozo mzuri kutoka kwa wazoefu

Nawasilisha

BM
Vipi ndugu ushafungua au bado

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila shaka biashara ya shule inahitaji mtaji mkubwa sana ili kuleta ufanisi maana utahitaji majengo, vifaa vya kufundishia na kujifunzia, rasilimali watu n.k
Lakini pia kiasi cha mtaji kitategemea unataka kuanzisha shule ya level(pre/primary/secondary) ipi na yenye ukubwa gani (idadi ya wanafunzi)


Anza na DAY care, Panga nyumba then kuwa mdogo mdogo then utafika huko kwenye International school.
 
Nimejaribu kutafuta threads zinazozungumzia hizo biashara mbili sijaziona,hebu wazoefu njooni tujadili hizo biashara hasa tukiangalia kiasi cha mtaji cha kuanza nacho na changamoto zake.

Kwa mfano ukataka kuanzisha dodoma,je ushindani uko vp huko!?je ni biashara inayokutaka muda wote uwepo sehem husika!?

Bishaara gani hizo mbili ?
 
Mm nafanya hiyo kazi
Ujue nishaumiza kichwa sana kufikiria kuajiriwa sema nin yatosha sasa

Nafikiria kuuza maandazi chapati na keki

Nakaribisha mawazo yenu.mtaji mpaka sasa sijapata ila ujuzi ninao hata kama sio mkali kiivyo.Nina imani wateja sikosi profit per day 7000 target ya kuanzia,location kigamboni.

Kama kuna mtu humu ashafanya hii biashara msaada wako tafadhali kabla sijala loss.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu habari,

Habari za mchana naomba kupewa ufafanuzi juu ya gharama, na vigezo ili uanze kuanzisha kiwanda cha mikate na changamoto zake kwa mwenye uelewa na hii biashara.

Naomba kuwasilisha.
 
Nipo siti ya mbele kabisa

Hii kitu ipo kweny mipango yngu!
 
Wakuu habari,

Habari za mchana naomba kupewa ufafanuzi juu ya gharama, na vigezo ili uanze kuanzisha kiwanda cha mikate na changamoto zake kwa mwenye uelewa na hii biashara.

Naomba kuwasilisha.
10million for starting sio mbaya, na one VAN for physical distribution itafaa itakua vizuri zaidi
 
Jamaa yangu hapo jirani aliwahi kufunga veranda yake kwa tofali...akamodifai akaichanganya na sebule akafungua bekari. Akaingiza majiko akawa anatengeneza mikate keki n.k

Biashara haikufikisha miezi 6 akaachana nayo.
 
Jamaa yangu hapo jirani aliwahi kufunga veranda yake kwa tofali...akamodifai akaichanganya na sebule akafungua bekari. Akaingiza majiko akawa anatengeneza mikate keki n.k

Biashara haikufikisha miezi 6 akaachana nayo.
Huyo ni yeye na muomba ushauri ni mtu mwingi, watu hawafanani nyota za kibiashara, hii ni njia ya kujikatisha tamaa.
 
Huyo ni yeye na muomba ushauri ni mtu mwingi, watu hawafanani nyota za kibiashara, hii ni njia ya kujikatisha tamaa
Sasa angekua anaulizia nyota yake ya biashara si angetafuta Wanajimu asingekuja JF?

Mimi nimempa scenario inayolenga kumpa angalizo kwamba afanye utafti wa kutosha kuhusu biashara hiyo.

Kwa akili yako hiyo iliyobireshwa na elimu ya kiwango hicho unaweza kweli ukasema "biashara ni nyota"? Au unaona raha mwenzio aingie kichwakichwa afilisike ?
 
Biashara ya bakery haina faida ni biashara kichaa,Faida ya mkate mmoja ni shilingi 50/= tu ya Tanzania kama ukipata sana.Mkuu fanya ishu nyingine maana Mtaji ni mkubwa faida ni kidogo ndio maana kuna mdau kasema kuna mtu kafanya kwa miezi 6 kaifunga.

Sipo kukukatisha tamaa mtaji wa ziaidi ya milioni kumi utauhitaji,maoven,dough mixer,brade slicer,Cake mixer,Bread and cake tins,racks za kuwekea,then twende kwenye kusajili kampuni,kodi ya pango na Raw materials then gari la kusambaza then petrol then kodi ya mapato,kwa kitu gani?50/=?Kuna biashara nyingi za kufanya mkuu achana na hiyo kazi.
 
Sasa angekua anaulizia nyota yake ya biashara si angetafuta Wanajimu asingekuja JF?

Mimi nimempa scenario inayolenga kumpa angalizo kwamba afanye utafti wa kutosha kuhusu biashara hiyo.

Kwa akili yako hiyo iliyobireshwa na elimu ya kiwango hicho unaweza kweli ukasema "biashara ni nyota"? Au unaona raha mwenzio aingie kichwakichwa afilisike ?
Hujanielewa wewe, nakueleza kama alifeli huyo sio lazima kila mtu afeli, kila mtu ana ujuzi wake wa kukuza biashara, umesema tu mtu hakufika miezi 6 akafunga biashara hujaeleza kilichofanya afunge biashara ni kama umekurupuka tu kunijibu kiholela
 
Back
Top Bottom