Biashara ya upepo, pancha, na kubadlisha tairi za gari

Rene Jr.

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2014
Posts
3,714
Reaction score
2,376
Salaam wakuu,

Kadri unavyotembea ukakutana na changamoto ndivyo kichwa kinavyofikirishwa. Last week nilikuwa sehem flan nikafikwa na changamoto iliyonifanya niwaze kitu kilichonifanya nianze kusaka majibu.

Ni vifaa gani vinavyohitajika kuanzisha biashara ya kuziba pancha za magari, kujaza upepo, kubadlisha tairi, na pengine kupima alignemnt?

Ningependa kupata orodha ya vifaa na gharama zake, pengine na mahala vinakopatikana. Napenda kujifunza kwa wanaofanya biashara hii pia, ina changamoto zipi?

ASANTENI
 
Asante, mtizamo wako ni mzuri sana, kabla ya yote fanya savei kwenye vituo husika ujionee aina gani ya mitambo inayotumika, hii itakusaidia kuchagua vifaa vip imara na vyenye bei linganifu na uchumi wako, nasemea hivo kwa sababu kuna biashara kama hizi zinafanyika kwa vifaa makini na mahili na wengine tu ni vijiwe vya kazi, vingine ni ofisi ya kazi.
 
Wazo zuri sana mkuu.
Lakini nakumbuka huu uzi upo na ulichangiwa vizuri saana.
Jaribu ku search utaupata
 
Maeneo nayosemea mimi hakuna kabisa huduma hizo, nilifikwa na majanga maeneo hayo nikasumbuka sana kwa hiyo nataka vifaa vya kawaida tu, anayefanya biashara hii akitusaidia itakuwa vizuri.
 
Huu uzi vp tena' mbona upo slow'mo na huku 2nackilizia wataalam wa hz mambo!
 
Inategemea na mtaji wako ukoje

Hapo kuna compressor sijajua utahitaji ya ukubwa gani na ya nchi gani
Mashine za kuvulia tyre pia bei zake inategemea na made in wapi
Eneo zuri ni kama ulilosema huduma hiyo ni ya tabu
Mashine nzuri ni za kiitaliano kwenye biashara hii
Nimepoteza contact za jamaa wa dukani wanapouza hizi mashine
Ila nikipata muda nitakupa contact zao
 

around 6m. nitashukuru.
 
Maeneo nayosemea mimi hakuna kabisa huduma hizo, nilifikwa na majanga maeneo hayo nikasumbuka sana kwa hiyo nataka vifaa vya kawaida tu, anayefanya biashara hii akitusaidia itakuwa vizuri.
Mkuu ulifanikiwa kupata msaada WA vifaa na bei?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…