Biashara ya Bajaj ni nzuri kama utaendesha wewe mwenyewe.
Tena ndani ya muda mfupi utarudisha fedha zako, lakini bajaj za hesabu ni pasua kichwa maana kuna madereva ni mchwa hatari.
Yaani hesabu iwe kubwa au ndogo mambo ni yaleyale.
Wengine watakuja kuamsha asubuhi akipiga round 2 za mwanzo then anampa Nyoka wake (deiwaka) anaipiga hadi saa usiku then dereva wako ndio anairudisha.
Na ubaya kila dereva ana mkono wake so mwisho wa siku utasikia Clutch inasumbua mara Block imetanuka mara hiki mara kile.
Bora hiyo ela ya Kununua Bajaj ufungulie duka la kuuza Spare za Bajaj na Pikipiki maana utapata Return ya Maana ambayo ni zaidi ya 20,000 ya hesabu ya Bajaj kwa siku.
Chamsingi weka vitu vinavyouzika haraka kama Filter Oil, Rubber, Seal, taa, shock ups, urembo urembo, valve nali, plug, betri, matairi na tube zake, compressor ya upepo.
Utaiona hela na utashangaa kikubwa upate Location ya Maana yenye vyombo hivyo vingi..
Chukua hiyo.
Sent using
Jamii Forums mobile app