Mkuu si kwamba nakukatisha tamaa, Ila hii biashara ni ngumu kuliko, ingawa hakuna biashara rahisi wala ngumu, ila kwa hii kuna utofauti kidogo na sababu kubwa ni hii
1. Umonopoly unaofanywa na kampuni kubwa
2. Pesa
3. Mtandao
- Makampuni mengi na makubwa ni ya wazungu na wahindi, na wana mitaji mikubwa balaa na wana Maagent huku Majuu mfano Marekani, Ulaya na Asia, so wao kupata watalii si ishu kwa sababu wana ofisi huku huko majuu na ukijumlisha na mitaji yao ilivyo mikubwa ndo maana wana weza kumonopolaize soko,
- Kwa kampuni za wazawa ni chache sana zinazo fanya vizuri na kwa Arusha na Moshi hata sita hazifiki, nyingi za kampuni za wazawa zinasubiria wale wageni walio jijia wenyewe ndo wanawakamata hao, au wale choka mbaya kutoka huko,
- Na tambua kwamba hata kataika watalii kuna Madaraja, kuna wale wenye pesa na kuana ambao hawa tofauti sana na wabongo, Mfano watalii kutoka USA, CANADA hao ndo wenye pesa na ni kampuni chache zinazo weza kuwapata hao na hata gharama za kukodisha magari kwa hao ziko juu balaa
PROPAGANDA
- Hii ishu niliwahi kuambiwa kwamba kampuni nyingi za Wazungu zilizoko huku huwa zinafanya propaganda ya kuwaaminisha watalii kwamba kampuni za wabongo haziamnini na zinazo aminika ni za kwao tu
So mkuu ili ufanikiwe ni lazima uwe na wazungu huko juu tena wazungu wa maana, la sivyo utaishia kuvizia wazungu walio kuja na Mabasi kutoka Nairobi kenya ambao unakuta ni choka Mbaya tu na ni mabairi sana,
Na unaweza cheki nyanja zingine za utalii, mfano cultre tourism kidogo haina mizengwe sana,