Habari Wadau,
Mimi nina mtaji wa 40m ninataka kufanya biashara ya kutengeze mafuta ya kula kutokana na mawese.
Nimejaribu kufanya utafiti wa malighafi Kigoma na Urambo tabora ipo ya kutosha.Eneo ya kiji-kiwanda nataka kuweka eneo la Kasulu Kigoma.
Pia nimekutana na wadau tofauti toka wizara ya kilimo,biashara na viwanda na watafiti na lishe bora
Target yangu kubwa nikusambaza mafuta mazuri kwa bei rahisi kwa wakaanga chips mijini.
Naombeni maoni yenu nini kifanyike zaidi.