JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Katika Jiji la Dar es Salaam ambalo kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi wapo wakazi zaidi ya Milioni sita, shughuli mbalimbali za kibiashara zimekuwa zikifanyika kama sehemu ya Watu kujipatia kipato.
Hata hivyo, miongoni mwa biashara ambazo zimekuwa zikifanyika nyingine uibua wasiwasi na maswali juu ya usalama wake kwa walaji licha ya kuwaongezea watu kipato.
Udadisi maalumu nilioufanyaka katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam unabaini kumekuwepo na ongezeko la biashara ya kuku hasa wa kisasa, jambo ambalo limeonekana kuwa fursa kwa wafugaji na kutanua wigo wa fursa kwa baadhi ya Wafanyabiashara wadogo wadogo kuanza kuuza utumbo pamoja na vitu vingine vya ndani.
Licha ya kuwaingizia kipato, udadisi unabaini baadhi ya Watu wamekuwa wakichinjia Kuku katika mazingira yasiyo salama na kupeleka bidhaa hizo sokoni kulingana na uhitaji.
Lakini mashaka zaidi yanaibuka katika uchinjaji huo, ambapo wahusika wamekuwa wakitunza utumbo na vitu vingine vya ndani katika mazingira yasiyo salama kwa ajili ya kuwauzia wateja wao ambao wamekuwa wakikaanga kwa ajili ya biashara katika maeneo mbalimbali, huku wengine wakizunguka na ndoo mitaani wakiuza ambao haujakaangwa.
Udadisi katika maeneo mbalimbali ya Dar unabaini baadhi ya Wafanyabiashara wa utumbo wengine huweka oda kwa wauzaji wa kuku kwenye masoko na mabanda ya kibiashara ambayo uuza kuku na kutoa huduma ya kuchinjiwa, lakini uchunguzi unabaini utumbo huo umekuwa ukihifadhiwa katika mazingira ambayo sio salama kabla ya kuchukuliwa hata baada.
Kutokana na hali ya maisha kiuchumi hasa kwa baadhi ya Wananchi ikiwemo Watoto wamekuwa sehemu ya walaji wa utumbo ambao mara nyingi uonekana sio salama kutokana na kutoandaliwa katika mazingira rafiki, huku wauzaji wengine wakitembeza kwenye ndoo kuanzia asubuhi hadi jioni na ikitokea soko limeenda vibaya ulazimika kuukaanga kwa ajili ya kuuza.
Wapo baadhi ya wananchi ambao wanakili wazi kuumwa matumbo kutokana na ulaji wa utumbo ambao uhisiwa kuandaliwa katika mazingira yasiyo salama hususani maeneo ya 'uswahilini'.
Wito wangu kwa mamlaka ni muhimu wakafuatilia kiundani suala hilo na hususani maafisa afya uenda kukawepo watu wengi ambao wamepata changamoto kutokana na biashara hiyo, lakini ni muhimu kuhamasisha utaratibu salama wa uchinjaji au kama biashara hiyo tumeamua kuihalalisha basi wahusika wasisitizwe kuzingatia usalama wa walaji.