Kwa maana ya kutaka kukidhi mahitaji ya soko (demand and supply), eneo unalofanyia biashara ndilo haswa hukupa mwanga wa mahitaji ya mtaji halisi wa biashara kwa kuzingatia mzunguko wa eneo husika.
Ila kwa kuanzia kama una mtaji wa 10M ni nzuri then unaweza kuongeza kulingana na mahitaji ya eneo, kiwango cha usimamizi na uwezo wako binafsi.
Changamoto:
Kwa upande wa changamoto ni nyingi kwa kweli, sisemi hivi kukukatisha tamaa bali ujiandae kuzikabili maana ukiteleza kidogo 'umepigwa'.
Kuna hasara zinazotokana na uzembe wa operator, uwezo mdogo wa mahesabu ya fasta fasta na utambuzi wa tarakimu na kiasi cha fedha, utapeli na ushirikina ni mwingi sana kwenye mambo ya fedha.
Kwa maoni yangu, kama huna operator mzuri ( ni vigumu kuwapata) na uwezo wako wa kumonitor business hii ni mdogo achana nayo.
Ukipunguza pesa kidogo kwenye mtaji unafeel lile gap (panayumba), kwa hiyo pesa unayoi dedicate pale kwa kiasi kikubwa huwezi kuichomoa kufanya jambo jingine kama ilivyo kwa biashara zingine.
Kwa uzoefu, ukizingatia commission ya mwezi na mtaji kwa eneo lililo busy sana, wastani wa profit ni 15% (gross).
Kama kuna fursa nyingine inayoweza kukupa profit hiyo kwa mtaji mdogo zaidi huku ina risk chache na pengine inahitaji minimum supervision ningekushauri uchague hiyo dhidi ya hii.
Benefits:
Ni biashara ambayo inaweza kukupa faida ambayo ni predictable almost kwa kipindi chote cha mwaka, mara nyingi miamala ya fedha ina wateja wengi fixed na wanakuwa ni regular customers, ni mara chache kwa siku kupata wateja wapya kabisa.
Kama uko eneo ambalo ni remote, biashara hii itaku connect na fursa nyingi sana kwa kuwa watu wengi wanaamini (actually wanaziona) pesa ulizo nazo, hivyo wengi watakuletea fursa.
Pia kwa remote areas inakupa dhamana kubwa ya kuaminika, kukopesheka na kudhaminika kwa mambo mengi sana kitu ambacho ni muhimu sn kwenye maisha kumiliki 'ghost capital'.