Pia nimegundua watu wengi huwa hawafanyi analysis kabla ya kuingia kwenye business, wengi huiga tu kwa kuona fulani anafanya.
Mfano, watu wengi anapotoa pesa kama mteja kwenye let's say M-pesa kiasi cha laki 1 na kukatwa 3,650/= anahisi pesa yote ile inaenda kwa wakala, kisha anaangalia movement ya wateja... anaona jamaa anapiga pesa hatari [emoji23][emoji23]
Ila kiuhalisia katika ile 3,650/= ya kutolea, wakala anabaki na tshs. 460/= na hapo bado haijakatwa kodi 10%. Sasa ndio hizo uzidundulize hadi mwisho wa mwezi uje utoe gharama ya kulipa operator(s), hujalipa kodi ya pango, umeme, ulinzi nk. unabaki na kiasi kidogo sana kwa kweli.