Wengi hapo hawajui mkuu, kuanzia huyo aliesema inalipa sana.
Kwa haraka mkuu ni biashara ambayo inahitaji kujituma sana ili ufikie mafanikio.Youtube malipo yao ni kidogo na inategemea idadi ya matangazo ambayo yameonekana au kutangazwa katika video yako.Kwa maana nyingine kwa mfano kama una views 1M na hakuna tangazo limetazamwa probably hautalipwa kabisa(huu ni mfano).
Pia kuna ka shughuli ka kufikia vigezo; subscribers 1000 na kuendelea pia masaa 4000 ya channel kutazamwa katika miezi 12 iliyopita.
USHAURI: Usitarajie pesa ya haraka, ila kama ukifanikiwa kuna malipo mazuri...na kuna mambo kama ya affiliate marketing unaweza kuyatangaza ukapata pesa nzuri.