Biashara yangu inaniingizia faida ya Tsh. 200,000 kila mwezi; Je, Niiache niende chuo?

Mkuu samahan kama nitakukwaza ila napenda kusema kuwa " Hela ndio kila kitu *

Sent From My Nokia Ya Tochi
 
Kwa kweli title yako na unachomaanisha haviendani.
Unataka upewe ushauri wakat hujaweka waz ni biashara gan unafanya, pengine wadau wangekwambia namna bora ya kufanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ulofa, Ushenzi Na Upuuzi kuacha hela na kufuata upuuzi

Sent From My Nokia Ya Tochi
 
Mimi sionagi nilifata nini University...
Tuko mpamoja mkuu...elimu ya form 6 inatosha sana......ila walitutangulia ndio wametudaganya......Maamuzi ya elimu yako wanamuachia mtu mmoja akitaka anakufelisha...
 
Mimi nimesoma chuo mwaka wa kwanza, ilibidi mwezi wa 10 niingie mwaka wa pili lakini nimekimbia chuo kwanza baada ya kuona ni ujinga nilichotarajia kukipata chuo ni tofauti kabisa, yaani nilijikuta nakariri tu, maana niliyosoma semester iliyopita siyakumbuki ila ukiangalia matokeo nimeperform vizuri, nikakaa nikatafakari nikaona kwa elimu niliyofikia inanitosha kabisa, na nikiendelea na chuo nitakua ni mjinga wa mwisho.

Nimeamua nitafute mil 2 niingie porini kulima lakini sio kupoteza Muda wangu na pesa chuo, mimi mzazi wangu ana uwezo wa kunilipia kila kitu chuo kwa wakati na boom nimepata lakini Nimeamua kuachana na chuo,

Nakushauri fanya biashara ukienda chuo baadae utakuja kujuta sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijana shida yako si elimu bali vyeti....Kitendo cha kuanzisha biashara tu una elimu zaidi ya Phd....mkumbuke yule mkuu wa Mlkoa ana Phd alilia baada ya kutumbuliwa....
Kijana elimu ni muhimu lakini si muhimu zaid ya pesa....Elimu ya kibongo ukienda huko chuo watakurudisha nyuma kimawazo......Mfumo mzima wa kielimu umeandaliwa kuwa mwajiriwa na sio kukiajiri......Huyo mhadhiri unafundisha soma la ujasiliamali hafanyi biashara nae mwajiriwa tu......Panua biashara yako weka mazingira mazuri ......tengeza network halafu nenda chuo kwa luxury ......
 
Aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Enedelea kukuza hiyo biashara yako... usikubali ife.. kama umeweza kutengeneza laki 2 kila mwez means utaweza tengeneza mpaka milion nyingi kila mwez... achana na chuo kwa sasa.. utasoma tu hata miaka ijayo once biashara yako imesimama vizur.


Elimu yetu inatudumaza sana asikwambie mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Elimu Ni Mbegu Na Maua ya Mafanikio!", Maadam una ndoto ya kuwa mchumi basi soma mkuu kwani hilo Ni somo rafiki Na kujiajiri/biashara yako, lakini kwa mazingira uliyopo nakushauri soma Open University kwa maana ya unafuu wa ada na muda WA kusimamia biashara yako. Nina uhakika baada ya kumaliza kozi yako utajiona ulivyo Na upeo mkubwa wa ku-utilize fursa na pia utaliona deni lililopo mbele yako kwa kufanya biashara ndogo wakati huo huo unafikra kubwa Sana kuhusu fursa za biashara zilizokizunguka. Na hiyo (elimu) ndio itakuwa driving force yako!. Amen!
 
Huwezi linganisha elimu na hela...ukifanya hivyo utakuwa kichaaa....nenda shule elimu ni Mali kuliko hiyo laki 2 kwa siku
Elimu sio kufika chuo kikuu mkubwa, unaweza usiwe na cheti hata kimoja lakini ukawa na elimu nzuri na kubwa kuliko mwenye cheti cha PhD inategemea wewe unaitafsiri vipi Elimu
 
Chuo unafuata nini? Mademu,modules,birthday party,bash au unawaza itakuwa rahisi kuajiriwa? Mi nadhani kiasi ulichonacho ndio PHD ya kukufanya uwe na maisha mazuri! Kuza mtaji wako na ongeza thamani katika biashara yako mkuu! Chuo kipo tu! utasoma kwa amani pale maisha yako yatakapokuwa stable! Huko chuo kwenyewe kila siku wanatoa seminars kuhusu kujiajiri! Fanya biashara! Nimepita chuo na nimeona chuo ni kupoteza muda tu! Sababu elimu yetu haipo katika misingi ya kutufanya tujitegemee baada ya kuhitimu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…