Biashara yangu inaniingizia faida ya Tsh. 200,000 kila mwezi; Je, Niiache niende chuo?

Biashara yangu inaniingizia faida ya Tsh. 200,000 kila mwezi; Je, Niiache niende chuo?

Haya mambo ya kuwaza kuwa ukitoka chuo basi unaanza kupata mshahara mkubwa au lazima uanzishe biashara kubwa inayokulipa mil 10 nk ndo inawafanya graduates wanakuwa maskini wa kutupwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mara nyingine tena nimechaguliwa
Kusoma
bachelor of arts in economics pale UDSM.

Wakati naomba ushauri nilikuwa tayari nimeshatuma maombi ya kujiunga university.

SASA kulingana na ushauri wa walio wengi najiuliza hii chance ni ipige chini tena?
 
Kama una ndogo za kuajiriwa rudi shule


Kama una ndoto za kuwa mfanyabiashara pga chin shule
 
Kwa mara nyingine tena nimechaguliwa
Kusoma
bachelor of arts in economics pale UDSM.

Wakati naomba ushauri nilikuwa tayari nimeshatuma maombi ya kujiunga university.

SASA kulingana na ushauri wa walio wengi najiuliza hii chance ni ipige chini tena?

Rudi shule kaka, trust me moyo wako uko shule.
Kama ushauri umetolewa mwingi namna ile wa kukushauri uendelee kufanya ukifanyacho lkn bado unawaza shule,
Formal education is the best for you
 

Rudi shule kaka, trust me moyo wako uko shule.
Kama ushauri umetolewa mwingi namna ile wa kukushauri uendelee kufanya ukifanyacho lkn bado unawaza shule,
Formal education is the best for you
Asante kwa ushauri wako..
 
Wakuu habari zenu,. Mwaka 2014 nilihitimu kidato ya sita shule mojawapo nchini, nikafanya application kuingia chuo kikuu nikachaguliwa kwenda kusoma course ya uchumi pale udsm.

Kwa bahati mbaya sikupata mkopo kutoka HESLB kwa ajili ya kuniwezesha kupata elimu hiyo ya juu,

Nikatazama nyuma na mbele nikagundua sina support kutokana na umasikini uliokithili ndani ya familia yangu,

Baada ya hapo nikachukua maamzi magum, nikasafiri kutoka mkoani mpaka jijini na nikafuta na kufuta kabisa mawazo ya hiyo elimu ya chuo kikuu kwanza kwenye ubongo wangu.

Mawazo yangu na bongo langu nikahamishia kwenye neno "ajira" nikaanza kutembeza bahasha la vyeti vyangu ya secondary kutafuta ajira hapa mjini, hata hivyo sikuweze kupata ajira baada ya kuzunguka sana na bahasha hapa jijini,. Baada ya changamoto hiyo ikanifundisha tena kubadili mawazo kutoka kutafuta ajira mpaka kutafuta "mtaji" ili nijiajiri, nikiwaza ni jinsi gani niachane na suala la kutembeza bahasha kila ofisi naonekana kama bango,

nikaamua kukusanya kamtaji kwa kuanzia na kale kale ambako nilikuwa nazunguka nako kutafuta ajira nikapiga vibarua vya hapa na pale, nikasaidia sana mafundi site mbalimbali, nikapata kamtaji, nikaachana kwanza na vibarua nikaanzisha biashara fulani.

kwa sasa biashara yangu hiyo inanilipa faida tasilimu ya shilingi laki mbili kila mwezi, na mpaka dakika hii nimeweza kukusanya ada ya kuweza kujilipia university nchini.,

Je niende chuo au niendelee na biashara yangu hii.

NB nikimuachia mtu kuisimamia hii business lazima ife ndani ya muda mfupi sana maana inahitaji kujitoa sana. Japo kulingana na hela niliyonayo cash lazima chuo nimalize bila wasiwasi kabisa..

Naombeni ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu jiunge na FOREX hiii biashara ni kiboko. Hio 200K unapiga kwa siku
8c2b5bdba8ca793d286aa753fc2214be.jpg
 
Kuna kitabu kinaitwa Rich Dad poor Dad...kwa kusummary n hiv hakikisha hiyo biashara unayoifanya inabadilisha kipato chako Kama kiwe kinasoma Kama no ya simu Alf ndipo utaamua kusoma au uendelee kufurah maisha.
 
Back
Top Bottom