stickvibration
JF-Expert Member
- Feb 7, 2017
- 3,226
- 5,147
EFD Machine
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu, nimekuwa na utamaduni wa kujisomea vitabu kadhaa kila mwaka, Japo kuwa mwaka huu nimebanwa ila mpaka sasa nimesoma vitabu vitatu
Sent using Jamii Forums mobile app
biashara gan mkuuWakuu habari zenu,. Mwaka 2014 nilihitimu kidato ya sita shule mojawapo nchini, nikafanya application kuingia chuo kikuu nikachaguliwa kwenda kusoma course ya uchumi pale udsm.
Kwa bahati mbaya sikupata mkopo kutoka HESLB kwa ajili ya kuniwezesha kupata elimu hiyo ya juu,
Nikatazama nyuma na mbele nikagundua sina support kutokana na umasikini uliokithili ndani ya familia yangu,
Baada ya hapo nikachukua maamzi magum, nikasafiri kutoka mkoani mpaka jijini na nikafuta na kufuta kabisa mawazo ya hiyo elimu ya chuo kikuu kwanza kwenye ubongo wangu.
Mawazo yangu na bongo langu nikahamishia kwenye neno "ajira" nikaanza kutembeza bahasha la vyeti vyangu ya secondary kutafuta ajira hapa mjini, hata hivyo sikuweze kupata ajira baada ya kuzunguka sana na bahasha hapa jijini,. Baada ya changamoto hiyo ikanifundisha tena kubadili mawazo kutoka kutafuta ajira mpaka kutafuta "mtaji" ili nijiajiri, nikiwaza ni jinsi gani niachane na suala la kutembeza bahasha kila ofisi naonekana kama bango,
nikaamua kukusanya kamtaji kwa kuanzia na kale kale ambako nilikuwa nazunguka nako kutafuta ajira nikapiga vibarua vya hapa na pale, nikasaidia sana mafundi site mbalimbali, nikapata kamtaji, nikaachana kwanza na vibarua nikaanzisha biashara fulani.
kwa sasa biashara yangu hiyo inanilipa faida tasilimu ya shilingi laki mbili kila mwezi, na mpaka dakika hii nimeweza kukusanya ada ya kuweza kujilipia university nchini.,
Je niende chuo au niendelee na biashara yangu hii.
NB nikimuachia mtu kuisimamia hii business lazima ife ndani ya muda mfupi sana maana inahitaji kujitoa sana. Japo kulingana na hela niliyonayo cash lazima chuo nimalize bila wasiwasi kabisa..
Naombeni ushauri
Sent using Jamii Forums mobile app
University ni hiyo biashara yako dont get twisted,hiyo ada ulinayo igeuze mtaji kisha fungua project nyingine...chuoni hamna kitu kule...kama ni kupata elimu utakua unasoma online ukiwa kwenye mambo yako,vitabu vyote vinavyotumika vyuoni viko kwenye mtandao tena bure.
Ni biashara gani mkuu?Nakushauri tafuta kozi usome lakini kozi ambayo itakusaidia kujiajiri baada ya shule somea kitu unachotaka kufanya ikiwezekana. Kwa mtu anae angalia mbali faida ya laki 2 kwa mwezi ni ndogo sana kukufanya kuachana na elimu. Kumbuka pia kuna umri wa kusoma kirahisi japo chuo kipo tu ukikaa miaka 5/6 mtaani kusoma tena itakuwia ngumu sana maana utajiona nje ya mazingira (hauto fit in). Muda ni sasa fuata moyo wako, never give up on your dream.
Ukienda shule tayari ukiwa na malengo yakujiajiri utafanikiwa sana utaacha kuwaza biashara ya kutembeza maji (no disrespect ni mfano tu) na utawaza kufungua kampuni ya kuingizia mil 15 kwa mwezi (mfano). Utaona laki 2 kwa mwezi ni pesa ndogo sana ukiwa unaangalia bigger picture.
Walio wengi wanasoma kwa kufuata ajira na kwa kozi ipi ina mkopo ndio maana wanapata taabu baada ya kumaliza.
Nakushauri fanya biashara mpaka pale utakapoona IPO stable ata kumwachia mtu,. Swala kusoma limebaki kwenye vitabu, application yake ni kama tu utaiweka kweny kujiajiri lakini kam utatumia nguvu nying kusoma sasa kuna uwezekano ukapoteza vyote ukarudi kweny msoto, ur still young kama umeweza kujiingiza kweny biashara ukafanika, elimu unayoitaj apo ni ndogo sana,.. So jitaidi biashara iwe stable kwanza then ujipe majukumu mengine,
University ni hiyo biashara yako dont get twisted,hiyo ada ulinayo igeuze mtaji kisha fungua project nyingine...chuoni hamna kitu kule...kama ni kupata elimu utakua unasoma online ukiwa kwenye mambo yako,vitabu vyote vinavyotumika vyuoni viko kwenye mtandao tena bure.
Okay, ASANTE kwa ushauri ngoja tusubiri mawazo ya wengine pia tuamue kwa pamoja.
Sent using Jamii Forums mobile app
Labda ungeuliza ufanye biashara gani,(kama hufanyi lakini) inayoendana na mazingira unayoishi na kiwango chako cha mtaji pesa.kijana tuambie basi biashara gani wafanya weye?
true say,ila watanzania tulio wengi ubongo wetu unachelewa kukua,hivi haya uliyoyaandika mtu anayetaka kwenda kusoma sasahivi hayaelewi kabisa,ila baada ya miaka 4-10 ndo atayaelewa!Depend na wewe una malengo gani na chuo unataka ukasomee nini na ni biashara gani unaifanya so far.
Niliacha kazi ya sales kwenye kampuni kubwa tu yenye salary nzuri na commission kubwa tu nikaenda kusoma kitu ambacho kitanifanya niajiliwe na nijiajiri. Mpaka muda huu nashukuru kwenda kusoma maana ninachoingiza kwa mwezi ni zaidi ya mara tatu ya kabla sijaenda kusoma na bado sijaridhika soon kabla huu mwaka haujaisha nitaanza kuingiza mara sita ya nilichokua nalipwa.
Fuata moyo wako soma ambacho kwako unaona kina faida wengi wanaolia walisomea vitu kufuata mkumbo bila kusoma hata ramani ya ajira au kujiajiri akimaliza chuo itakuaje (samahani kwa nitakaowakwaza ila ukweli ndio umuweka mtu huru).
Ukienda kusoma ikiwa unajua unataka kufanya nini baada ya kuhitimu basi utafanya vizuri sana chuoni na utafaulu vyema sana huenda leo unapata hiyo laki mbili faida baada ya kusumbuka sana ila ukaenda chuo ukapata milioni faida ya bila kuumiza kichwa sana.
Jiandae tu chuoni kuna mateso na kuna kuvumilia kunahitajika sana maana kuna muda unaweza jisikia kuacha chuo but komaa mpaka lengo litimie
true say,ila watanzania tulio wengi ubongo wetu unachelewa kukua,hivi haya uliyoyaandika mtu anayetaka kwenda kusoma sasahivi hayaelewi kabisa,ila baada ya miaka 4-10 ndo atayaelewa!
Uko vizuri sana,Hakika mimi nilipomaliza form six kwakweli sikua na hamu ya kusoma nikatafuta kwanza ajira nikafanya kwa miaka kama mitano,nikajifunza mengi nilipokwenda chuoni nikajua nafuata nini na kipi kipo mtaani.
Nimefundisha,nimeongoza taasisi binafsi na nikafanya sales zote zikanijenga na nikaenda kusomea kilimo. So kutazama unataka kufanya nini ukitoka chuo ni muhimu zaidi,kama uko A level muda wa likizo tafiti sana kuliko kujiona uko juu sababu u mwanafunzi na wengine wa mtaani hawana akili.
Labda ungeuliza ufanye biashara gani,(kama hufanyi lakini) inayoendana na mazingira unayoishi na kiwango chako cha mtaji pesa.
....great great thinking!Pamoja na gharama Za manunuzi Au siyo ? Je biashara hiyo inamuda gani ianze? Na hicho kiwango cha faida Kwa mwezi umekuwa ukikipata Kwa miezi mingapi mfululizo? What is the nature of your business ? Je unalipa kodi stahiki Kwa kila mamlaka husika Kwa wakati ? Je mtaji wa biashara yako ni kiasi gani ? (Net wealth) , Je una mkopo wowote? Je unajaribu kuona uwezekano wa biashara yako kuwa endelevu? Je hakuna viashiria / dalili ambazo zaweza Shaka uwezekano wa biashara yako kuendelea? (Going concern symptoms ) , Je Kwenye hiyo faida umejilipa Mshahara Kwa ku assume kuwa Kama ungeajiri Mtu ungepaswa kulipa? Naomba ujibu hayo machache kwanza Kisha ndo nitakushauri uende Chuo Au usiende Kwa sasa Au ufanye vyote viwili.
Hyo hela ndogo hata muuza maji ya mkokoteni chanika anaipata Mara tatu ya hyo kwa mwez,,