Biashara za kifamilia ni ngumu na zinaweza kusambaratisha familia nzima

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Posts
5,107
Reaction score
10,969
Sehemu ninayofanya kazi tuliwahi kufanya kazi na kampuni fulani ya usafirishaji na utoaji mizigo bandarini, kampuni hii ilikuwa ikiendeshwa kifamilia..yaani unakuta Mmiliki ni babu, Meneja Mkuu ni baba, Rasilimali Watu ni shangazi, Mhasibu ni mpwa, Mkuu wa Madereva ni binamu n.k

Kampuni hii ilinivutia maana inaiweka familia karibu, mnakuwa mpo pamoja muda wote na pia inatoa ajira kwa wanafamilia na kutunza legacy ya mzee kama ikiendelea vizuri baada ya yeye kufariki.

Ila baadae nikaja kugundua biashara hii ina changamoto nyingi sana ukiacha changamoto za kawaida za biashara kama mabadiliko ya kiuchumi na ushindani wa soko

1. Kwanza hii biashara inakuweka njia panda mara nyingi.. Kuna mahusiano ya kibinadamu kati ya wanafamilia, mahusiano haya yanakuwa kikwazo kwa wanafamilia ku maintain mahusiano ya kikazi (professional relationship) ama ukiendekeza professionalism sana utakuta mahusiano yako na familia yanadorora, mfano kama mtu wa chini yako akifanya kosa unakuwa ngumu kumchukulia hatua sahihi za kumuwajibisha

2. Kingine wafanyakazi wengi ambao sio wanafamilia watakua wakitafuta kazi sehemu nyingine sababu wanaona kampunibni ya familia na hawana nafasi kubwa sana ya kufanikiwa wakiwa hapo

3. Ila kama wewe ni mwanafamilia inakua ngumu kuondoka kutafuta kazi sehemu nyingine na kuiacha kampuni ya familia, hasa inapokuwa matatizoni..Utaonekana ni msaliti

4. Kunakuwa na kufanya kazi kwa mazoea na kunakuwa hakuna mawazo mapya kwani wanafamilia huwa wana "take for granted" fursa wanazopewa hasa ukizingatia hawawajibishwi ipasavyo wanapokosea

5. Pia ikitokea mmiliki akifariki ghafla na hakuandaa mrithi kabla, kumtafuta mrithi wake inaweza ikaleta tabu kwani siasa za kifamilia kwenye mbio za urithi zinaweza kupelekea vita na familia kuvurugika

6. Kunakuwa pia na shinikizo la kuwaajiri wanafamilia wengine zaidi hata kama hawana vigezo bora kuliko ambavyo ungevipata ungeajiri mtu mwingine

Hivyo biashara hizi ni ngumu mno hasa ukiwa na wanafamilia ambao sio waelewa, ni bora kuwatafutia ajira kwingine kuliko kuwaleta kwenye biashara yako
 
Ukitaka kuielewa kwa undani biashara ya familia na kuiendesha bila matatizo makubwa kifamilia kwanza onana na mabaniani wakupe ideas.

Halafu isajili biashara kama kampuni kisheria wahusika wote waainishwe kwa details kabisa ubia wao ukoje kama vile utavyofanya na watu baki. Hata iwe ni ndugu baba mmoja mama mmoja, sheria na kanuni za biashara zifatwe to the dot.
 
Shughuli sana, ndugu nao usipowapachika kwenye Biashara utakuta wanakusimanga vibaya tena. Kwenye mambo ya pesa tafrani mwanzo mwisho
 
Mbona imekaa kama kaujinga fulani hivi
kakujitakia, kampuni nzima ndugu tena waafrika unategemea nini
 
Hata ukifanya hivyo, hamuwezi kuwa robot..undugu lazima utaathiri biashara kwa kiasi fulani
 
Mbona wahindi na waarabu wanaweza! Hao akina MO siyo waanzilishi ni wajukuu.
 
Mkuu mimi naleta wazo mbadala.
1.Misingi ya utendaji iwe wazi.usuluhishi ni mikutano ya kifamilia.
2.watumishi wa nje walindwe kwa mishahara Mizuri iliyo zaidi ya mishahara ya Soko.
3.Uhamaji unaingiza maarifa mapya.hasa unapoajiri watu wajuzi.
4.wizi unadhibitiwa na mikutano ya Kifamilia.
5..Hili linawezekana tuelimishane faida ya kuandika warithi kibiashara
6.Hili nalikubali ni tatizo kubwa.
Wahindi wanafanikiwa kwa nini sisi tuu Waswahili?Tufunguke macho.Faida ni nyingi kama tutakuwa flexible,Faida kama ya kuchangiana mtaji ili kuweza pata mkopo mkubwa.Kuleta mahusiano karibu yanayosimamiwa na katiba na taratibu nzuri ukoo uliojiwekea..
Wataalam wanasema Survival for the fittest.Kama tutabaki Rigid hatutaweza kushindana,Daima tutakuwa mkia.
 
Kabla hta hamjasajili kampuni mnapaswa kusain form za (mou) mkae na muelewane jinsi mtakavyoendesha kampuni, kila mtu apewe role yake na akizembea awajibishwe

Undugu ubaki nyumbani mkiwa kazini mnapaswa mmeoprate km kampuni nyingine. Msiulete undugu kazini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji2][emoji2] siasa za kifamilia.. kumbe siasa kila mahali!!

Niliwahi fanya kazi kwenye biashara ya familia, na mmiliki alishafariki... yote uliyoandika ni kweli tupu!!

Wale jamaa mwisho wa mwaka walikuwa wanagawana familia kila mtu anasepa... toka mzee wao afariki hawakuongeza chochote tangible!
 
Mtia mada ninakupinga ninao mfano hai wa biashara ya familia issue Ni organisation structure na majukum
Mfano. Standard oil ya David na Albert rockerfellar American
Gsm group Africa ya gharib na said Saad Mohammed Tanzania
Motisun group ya shubhash na jitu Patel Tanzania
Bakhresa group of companies Salim bakhresa and sons Tanzania
METL YA Mohammed and his father's ghulam and azim dewj
Hao hawajui management useme hvyo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni mtihani sana. Ila hayo magumu siyo kwamba waarabu, wachina, wahindi na wasomali hayawakuti. Ni namna tu wanapambana nayo. Na kingine wenzetu watoto wao huwafunza biashara kwa kuambatana nao hata wakiwa wadogo. Nafikiri na ule mfumo wao wa familia kubwa kuishi pamoja unawasaidia.
Huwezi leo ukachukua tu kijana wa 24 ukamuingiza kwenye family business. Hana uchungu nayo, hajui kipi ni kipi wala hajui magumu yake. Anachojua ni faida tu na kugawiwa hela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…