Biashara za Online Zimejaa Matapeli

Biashara za Online Zimejaa Matapeli

King Loto

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2018
Posts
1,581
Reaction score
1,357
Habarini wanandugu wa JF na poleni na majukumu ya kila siku.

Leo hii nimeona nije na hii threadπŸ“œπŸ“œπŸ“œπŸ“œπŸ“œ angalau tutoe tongo tongo machoni mwetu.
Huu UZI utaweza kukusaidia Wewe na Mimi tuepukane na hili janga la kuaminishwa kuwa fursa za makampuni ya online businesses yanaweza kututoa kimasomaso kwenye wimbi la umaskini na kuwa na kipato cha kumudu maisha au kuongeza mianya ya kipato.

Kama kichwa cha habari kinavyoeleza hapo juu, Siku hizi kumekuwa na upotoshaji wa baadhi ya watu wanaotushawishi kuingia kwenye biashara za online wakijiita ni makampuni yanayojihusisha na online money, wengi wao wakiwa wanadai wanadeal na currencies hususani virtual currencies kama bitcoins, etherum, zcash, ripple na digital currencies zinazoendana na hizo ambapo platform yake inafahamika kwa jina la crypto currency exchange trade ya digital coin.

kumbuka pia biashara ya sarafu za kidigitali mfano bitcoins ni virtual currencies huwa haina any stakeholders au third parties kulingana na teknolojia yake ilivo kuwa discovered na Nakamoto, hivyo siyo sawa na legal currencies kama USD, EURO, AUD, JPY, TSH n.k. legal currencies zimebeba third parties ikiwemo World Bank ambao ni wadau wakubwa hivyo trust and credibility is inhand ndio maana forex trade is on fire πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯ sasa crypto currency trade inakosa hii sifa alafu bado watu wanaamini makampuni ya kitapeli badala ya kutrade wenyewe au kununua Bitcoin na kuuza wenyewe, ndio maana inadeal na virtual currencies na ukitapeliwa au kampuni ikafall definitely unakuwa hunapaku claim au kudai wala pakufia yaani ni maumivu tu πŸ˜₯πŸ˜₯πŸ˜₯πŸ˜₯πŸ˜₯

Hivyo basi uweza kuwashawishi wengi wa watanzaniaπŸ‡ΉπŸ‡Ώ na hata nimeona nchi nyingi za africa mashariki na hata Congo au niseme Africa kiujumla especially third countries wameona ndio chance ipo vile elimu yao haijapanuka kuhusu information system globally hivyo wameona kuna mapopo wengi wakuwachota pesa fasta na kusepa.

Hivyo waafrika wengi wameingia kwenye huu upepo mchafu wa kitapeli kwa kudanganywa waekeze pesa kwa kuwa part of the company na wanunue shares, wao wanaita packages au vifurushi ambavyo wameeka ununue kwa gharama tofauti tofauti na mwisho wa siku unalipwa kwa percent kadiri ulivowekeza kwa gawio la faida, kitu ambacho Mara nyingi kimekuwa ni udanganyifu na kuwatapeli pesa, wanaodanganywa hutoa pesa eti wawekeze watalipwa na hatimaye mwisho wa siku wanaingizwa mjini live live!!!!!!!!!!!

Hawa Matapeli wengi wao wamekuwa white men kutoka mataifa ya Brazil, Ureno na Mexico na hata Marekani, na uazishwaji wa hizi scam businesses zimekuja baada ya trusted network businesses kuanza Kama forever living company, super life nakadhalika, pia forex trade kushamiri zaidi mtandaoni na kupata influencies za watu ndipo hawa scammer waka anzaa kuwa wengi,

Njia wanazotumia kupata watu na kuwashawishi ni pamoja na social medias Kama whatsup, fb, na Instagram, mfano utaniamini kama umewahi kuona messages za magroup ya whatsup zikitumwa kila mara zikieleza kuna fursa mpya ya biashara, wanajiita majina kama hutley investment, bitclub advantage, vortex, mcc n.k,

Pia njia nyingine ni pale mwenzako aliyeingia anaweza kukushawishi na wewe kiurahisi ukaona ni sahihi ukaingia na wewe pia ukamshirikisha mwingine maana wanawapa hamasa ya kulipwa pale unavyo mshirikisha mtu japo malipo yako unapewa indirectly kwenye account utakayo kuwa nayo, hivyo kutokana na kushirikishana chain itaendelea kuwa kubwa na mwisho mnatapeliwa wote kwa pamoja.

Gear wanayoingia nayo huwa wanakuambia tunadeal na fursa za kuchenjua coin za kidigitali Kama bitcoin, etherum, ripple n.k pia wanadanganyaga sana wanafanya biashara za mafuta, Gold, na hata real estate businesses kitu ambacho ni uongo wa kuingiza watu mjini ili muwaone matajiri na watu wenye basement kubwa kifedha isiyo weza kufilisika kirahisi na mwisho wa siku mwaamini mwekeze kweli kumbe ni trick tu ya kuwapiga pesa.

Sasa wanashawishi unapoekeza unalipwa daily, weekly hata monthly kwa mfano unaambiwa wekeza laki 7 kila siku watukupa elfu 4 na kwa wiki labda elfu 50 na mnalipwa in terms of dollars,

Sasa ni kweli watanzania wamekuwa wakiweka pesa na uki open account unafurahi mpunga unaingia kwa dola au watu wa Arusha tunasemaga kibunda inasoma πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ na hata unaweza kulipwa kweli ukawithdraw pesa kwa baadhi ya hayo wanaojiita makampuni lakini sasa huo ni mtego wanawalipa kiaina muje wengi maana huu mfumo pia wanawaambia ni wa network market hivo unaweza pia mshirikisha mwingine ukalipwa, wao wanaita mfumo wa referral bonuses pale utakapoleta mwenzako utapewa hiyo bonus kwa hiyo mtashirikishana mtakuwa wengi oviusly na mukisha jazana kuwekeza ela wanawapiga mapema wanasepa zao wanawaacha kwenye mataa.

Kimsingi hizi kampuni ziko kiupigaji na wanaosema wanawin ni kama 1 kati ya 100 ambao wanajitoa na kutoendelea kuwekeza ila wengi wametapeliwa sana sana.

Kwani nini watu tuendelee kuumizwa kwa kutaka mteremko, nadhani ni muda wa kufanya vitu productive Kama ni Online businesses fanya mwenyewe Kama either utatrade forex ingia sokoni mwenyewe uza na ununue currencies mwenyewe kuliko kuamini mtu.

Amna kitu kibaya kinacho leta umaskini Kama kuwa tegemezi, Hawa jamaa wanataka kusema wao wana skills za kutrade sijui technical skills, lakini hata sisi tukijifunza hatushindwi kufanya wenyewe.
Upo msemo unasema jiamini believe in yourself pia Go confidently in the direction of your dreams, & live the life you have imagine.

Ushauri wangu tuepuke hizi mambo na tufanye vitu productive vya kuonekana tusipende mteremko, pesa zipo Kama tutaamua kuzitafuta mbona riziki mafungu saba.
Yupo jamaa aliwahi sema kuna watu they have rated five star πŸ’ŽπŸ’ŽπŸ’ŽπŸ’ŽπŸ’Ž but they just have one star πŸ’Ž because of their greed, wapo wanaojaliwa talanta tano ila wanapata talanta moja sababu ya tamaa zao.

Wakuu mi sina mengi naamini ni wengi wameshatapeliwa na wengine bado wanarudia makosa na kuendelea kutapeliwa kwa sababu ya kuwa na tamaa kuwa greed na amini wapo watakao niunga mkono kukubaliana na Mimi na watakaopinga wapo pia ambao wengi wapo kwenye hizo mambo.

πŸ”¨πŸ”¨πŸ”¨πŸ”¨πŸ”¨πŸ”πŸ”πŸ”πŸ”πŸ”πŸ”πŸ”πŸ”Mwisho kabisa amna kampuni ya bitcoin inayouza share ambayo ni trusted, 100% ya hizi ni scammers 🚫🚫🚫🚫🚫

Mi nasemaga ukiona fursa inakufuata jua wewe ndio fursa yenyewe kivyovyote jiandae kupigwa. Kwani nini wewe usifuate fursa, mpaka fursa ikufuate.
Nawasilisha wana JF.
 
Habarini wanandugu wa JF na poleni na majukumu ya kila siku.

Leo hii nimeona nije na hii thread itakayoweza kukusaidia Wewe na Mimi tuepukane na hili janga la kuaminishwa kuwa fursa za makampuni ya online businesses yanaweza kututoa kimasomaso kwenye wimbi la umaskini na kuwa na kipato cha kumudu maisha au kuongeza mianya ya kipato.

Kama kichwa cha habari kinavyooleza hapo juu, Siku hizi kumekuwa na upotoshaji wa baadhi ya watu wanaotushawishi kuingia kwenye biashara za online wakijiita ni makampuni yanayojiusisha na online money, wengi wao wakiwa wanadai wanadeal na currencies hususani virtual currencies kama bitcoins, etherum, zcash, ripple na digital currencies zinazoendana na hizo ambapo platform yake inafahamika kwa jina la crypto currencies ya digital market,

Hivyo basi huweza kuwashawishi wengi wa watanzania na hata nimeona nchi nyingi za africa mashariki na hata Congo wameingia kwenye hizi biashara za kitapeli kwa kudanganywa waekeze pesa kwa kuwa part of the company na wanunue shares, wao wanaita packages au vifurushi ambavyo wameeka ununue kwa gharama tofauti tofauti na mwisho wa siku unalipwa kwa percent kadiri ulivowekeza kwa gawio la faida, kitu ambacho Mara nyingi kimekuwa ni udanganyifu na kuwatapeli pesa wanaodanganywa kutoa pesa eti wawekeze watalipwa na hatimaye mwisho wa siku wanaingizwa mjini live live!!!!!!!!!!!

Hawa Matapeli wengi wao wamekuwa white men kutoka mataifa ya Brazil, Ureno na Mexico na hata Marekani, na uazishwaji wa hizi scam businesses zimekuja baada ya trusted network businesses kuanza Kama forever living company, super life nakadhalika, pia forex trade kushamiri zaidi mtandaoni na kupata influencies za watu ndipo hawa scammer waka anzaa kuwa wengi,

Njia wanazotumia kupata watu na kuwashawishi ni pamoja na social medias Kama whatsup, fb, na Instagram, mfano utaniamini kama umewahi kuona messages za magroup ya whatsup zikitumwa kila mara zikieleza kuna fursa mpya ya biashara, wanajiita majina kama hutley investment, bitclub advantage, vortex, mcc n.k

Gear wanayoingia nayo huwa wanakuambia tunadeal na fursa za kuchenjua coin za kidigitali Kama bitcoin, etherum, ripple n.k pia wanadanganyaga sana wanafanya biashara za mafuta, Gold, na hata real estate businesses kitu ambacho ni uongo wa kuingiza watu mjini.

Sasa wanashawishi unapoekeza unalipwa daily, weekly hata monthly kwa mfano unaambiwa wekeza laki 7 kila siku watukupa elfu 4 na kwa wiki labda elfu 50 in terms of dollars, sasa ni kweli watanzania wamekuwa wakiweka pesa na uki open account unafurahi mpungu unaingia kwa dola na hata unaweza kulipwa kweli ukawithdraw pesa kwa baadhi ya hayo wanaojiita makampuni lakini sasa huo wanawalipa kiaina Kama mtego muje wengi na mukisha jazana kuwekeza ela wanawapiga mapema wanasepa zao wanawaacha kwenye mataa.

Kimsingi hizi kampuni ziko kiupigaji na wanaosema wanawin ni kama 1 kati ya 100 ambao wanajitoa na kutoendelea kuwekeza ila wengi wametapeliwa sana sana.

Kwani nini watu tuendelee kuumizwa kwa kutaka mteremko, nadhani ni muda wa kufanya vitu productive Kama ni Online businesses fanya mwenyewe Kama either utatrade forex ingia sokoni mwenyewe uza na ununue currencies mwenyewe kuliko kuamini mtu.

Amna kitu kibaya kinacho leta umaskini Kama kuwa tegemezi, Hawa jamaa wanataka kusema wao wana skills za kutrade sijui technical skills, lakini hata sisi tukijifunza hatushindwi kufanya wenyewe.
Upo msemo wanasema jiamini believe in yourself pia Go confidently in the direction of your dreams, & live the life you have imagine.

Wakuu mi sina mengi naamini ni wengi wameshatapeliwa na wengine bado wanarudia makosa na kuendelea kutapeliwa kwa sababu ya kuwa na tamaa kuwa greed na amini wapo watakao niunga mkono kukubaliana na Mimi na watakaopinga wapo pia ambao wengi wapo kwenye hizo mambo.

Ushauri wangu tuepuke hizi mambo na tufanye vitu productive vya kuonekana tusipende mteremko, pesa zipo Kama tutaamua kuzitafuta.

Mi nasemaga ukiona fursa inakufuata jua wewe ndio fursa kivyovyote jiandae kupigwa. Kwani nini wewe usifuate fursa.
Nawasilisha wana JF.
Wasiwasi wako tu?Mbona hela zipo?
 
Well said mkuu, wa kusoma na asome na ujumbe umfikie...na siku hizi zimeshamiri kweli yaani...Ponzi schemes na network marketing ndio kabisaa..hawa Bitcoin na wenzao ndio sitaki kuwasikia kabisa...

Wasitumie kigezo cha udigitali kuwa kama mgongo wa kuwaibia na kutapeli pesa za watu
 
Watu wamekuwa wakipenda mteremko wakati mambo sivyo ya livyo na ukifuatilia hawa wanatapeli watu kirahisi sana sana.
 
Watu wamekuwa wakipenda mteremko wakati mambo sivyo ya livyo na ukifuatilia hawa wanatapeli watu kirahisi sana sana.
Uko sahihi mkuu, na cha kushangaza wengine kwa kujua au kutokujua wanaingia katika mkumbo huu...cha ziada ni kwamva ni watu walioelimika na elimu zao wanapigwa mchana kweupee...Unawekeza hela pasipo kujua misingi yake, mtu humjui hakujui unamuamini akutunzie hela zako...daaah tuna safari ndefu kufika

Hizi tamaa ndizo zinazotuponza mara nyingi na yote ni katika kusaka shortcut/njia fupi ya mafanikio

Mtu yuko amekaa tu huko anasema 'hela zangu zipo kwenye mzunguko, nikiamka asubuhi nazidownload'

Tofauti kati ya ndoto na mafanikio ipo hivi, ndoto utaipata ukilala, mafanikio utayapata kwa jitihada na sio kulala..
 
Umelenga point ya msingi sana hapa mkuu, ni wachache sana wanaelewaga hivi, Pia kuna hiki kitabia siku hizi wamekuja nacho hawa jamaa na wale wanaojiita motivational speaker wanawaambia watu eti usipo tafuta njia ya kupata pesa ukiwa umelala utafanya kazi mpaka unakufa, hivi ni tajiri yupi ambaye hafanyi kazi na amelala? hii kitu nayo ni gear wanatumia kuambia watu waekeze ela kwa hiyo zitaingia wakiwa wamelala. Wanachosema ni kinyume chake kabisa, Sasa umekuwa msemo wa vijana wa siku hizi
 
Kuna rafiki yangu kanisani alinishawishi kujiunga na bitcoin.. lakini shida nikaona jinsi alivyoniambia ni tofauti na muonekano wake.. sasa mwenyekiti wa vijana alimkopesha 200000. Cha ajabu yule kaka alipotea kanisani hadi leo
 
Take Risks if you want make it.Take calculated Risks
Let me tell you something my friend risk taking isn't to trust someone that even you don't know him do the real business that you always understand it, incase you get loss you may either findout what has come over that loss, risk taking = sacrifices, so if you give money to someone what do you think will be the sacrifices, just be logical you will understand what do I talk about.
 
Kuna rafiki yangu kanisani alinishawishi kujiunga na bitcoin.. lakini shida nikaona jinsi alivyoniambia ni tofauti na muonekano wake.. sasa mwenyekiti wa vijana alimkopesha 200000. Cha ajabu yule kaka alipotea kanisani hadi leo
Ndugu kama uelewi kitu tafuta kwanza uelewa wake ndio ufanye usikae uige kwa kuona kumbe na fulani anafanya utapoteana sana, ila hongera kwa kushutuka kwa hilo, soma vizuri hapo juu kwenye thread utaelewa.
 
Kwa hiyo bwana ubongokid hiyo unayosema ni risk taking definitely sio kweli na umeongezea neno calculated risk kama unajua maana ya hii calculated risk ulicho sema basi ni ushahidi unaokufunga maana calculated risk should be studied and computed sasa hii kampuni za kitapeli zishawahi kukuita physically mkakaa mkajadili risk emerged from investing
 
tatizo wabongo elimu muliitoa zandakarawe we kweli kampuni ina wiki mbili unaiamini unaiachia vipesa vyako vya korosho unategemea nini
 
Let me tell you something my friend risk taking isn't to trust someone that even you don't know him do the real business that you always understand it, incase you get loss you may either findout what has come over that loss, risk taking = sacrifices, so if you give money to someone what do you think will be the sacrifices, just be logical you will understand what do I talk about.
Watu walionunua bitcoin wakati ipo 200$ saivi ipo worth tens of thousands. High risk high reward. Calculated risks are part of the game.

Matapeli wanajulikana tu cha msingi ni mtu kufanya research kabla ya kukurupuka lakini ukisema fursa zote za online ni scam kisa huoni mtu mhusika unakua unakosea sana.
 
Kwa hiyo bwana ubongokid hiyo unayosema ni risk taking definitely sio kweli na umeongezea neno calculated risk kama unajua maana ya hii calculated risk ulicho sema basi ni ushahidi unaokufunga maana calculated risk should be studied and computed sasa hii kampuni za kitapeli zishawahi kukuita physically mkakaa mkajadili risk emerged from investing
Kukaa physically sio enough proof.. In fact unaweza ukakutana na mtu physically akawa amekushawishi virahisi kuliko ata online...

Mi nadhani cha msingi ni kujielimisha, kujua what you're dealing with na kufanya maamuzi baada ya kufanya research ya kutosha.

Dunia ya sasa ni Dunia ya online, whether we like it or not. Sasa ukimwambia mtu online hakuna cha kweli kwa sababu mtu haonekani.. Yani unakua umempoteza sana hasa kwenye Tanzania kama hii yenye ajira chache.

Vijana wenzangu cha msingi ni kujielimisha tu. Soma vitabu, articles pata ujuzi.. Hutowai kuingia kwenye mitego kama hii ya ponzi schemes.
 
Ukiona fursa inakufuata ujue wewe ndiyo fursa jiandae kupigwa yaani kuwa makini πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Wewe ndiyo unatakiwa ufuate fursa.
Asantevsana,Mungu akubariki,kwa kuwashtuwa watu,na utapeli,unaofanywa na watu wa sio waaminifu.
 
Nawaona vijana hasa wa chuo wanavyopapalikia huu utapeli.
Kuna hii inaitwa global health alliance wanawadanganya eti kuna ujiunge kwa tsh 500,000 halafu na wewe utafute watu wawili uwashawishi wajiunge.

Unakuta kijana mzazi wake kajichanga ili amlipie ada mtoto , mtoto naye anaona ngoja aiongezee hiyo hela kwa kuamini kuna siku kweli atatoboa.
 
Back
Top Bottom