Biashara za Online, Zinaibuka gafla na kufa gafla

gkasekwa

Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
41
Reaction score
2
Wadau mpo powa!

Hivi karibuni kumeibuka biashara nyingi sana za mitandaoni ambazo zimekuwa zikivutia sana kwa kujinadi kwao. Mfano wa biashara hizo ni D9, Amazon traders, Elnet Africa, Helping hand,rifaro africa, dollarplane, bitclub advantage etc.

Kwa kifupi zimekuwa ni biashara zenye ushawishi mkubwa sana kiasi kwamba watanzania wengi wamekuwa wakijiunga nikiwepo mimi. Shida iliyopo biashara hizo zimekuwa zikiibuka na kufa haraka sana kabla ya kukamilisha mafanikio unayoaidiwa muda wa kujiunga.

Kibaya zaidi zimekuwa zikitumia sana pesa ya nje yaani dollar na bitcoin. Je huu sio utakatishaji wa pesa ya Tanzania? Kuna watu wameuza hadi nyumba na kujiunga na mwisho wa siku wameambiwa network imehakiwa je huu sio uharamia mwingine kwa watz? Ni kweli kwamba serikali haiwezi kuingilia kati kwenye hizi biashara?

Wadau nawakilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nafkir ni watu wenyew kujiongeza,kwanza unaambiwa dont invest what you can't afford to Lose

Ukiliwa ni wewe mwenyew tu,serkal itapewa kaz bure tu..
By the way...wapo wanao liwa na wapo wanao kula...kikubwa ni kupambana na hali yako tu..

All men are self made [emoji123]
 
We umejiunga na biashara Gan Kati ya hizo, umepata faida au umeliwa??, tuanzie apo kwnz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani serikali izuie bitcoin unaota eeh?? USA wenyewe wameshindwa... Kama hujui one bitcoin kwa sasa ni dola 4400 sawa na 8mil za kibongo!! Na inapanda kila siku...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani serikali izuie bitcoin unaota eeh?? USA wenyewe wameshindwa... Kama hujui one bitcoin kwa sasa ni dola 4400 sawa na 8mil za kibongo!! Na inapanda kila siku...

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza nikwambie bitcoin haitaweza kamwe kuhalalishwa sababu haiko controled kama normal currency mtaendelea kuuziana na kununua hivo hivo ki bubu bubu


Afu soma vizuri maada husika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…