Biashara zangu zimegeuzwa kuwa za ukoo

Cheka cheka na nyani utavuna
mabua.
*Umemuingiza mama kwenye biashara akichota noti kumpa mwanae akale bata utamfanya nini?
*Business is a separate entity, huwezi toka nyumbani na kwenda kwenye biashara yako kuchukua pesa itakavyo,
* Kinachotoka kwenye biashara kwenda kwa mwenye biashara ni faida sio mauzo,
*Tengeneza mfumo madhubuti wa udhibiti (strong internal control mechanism) utakao ondoa mianya yote ya kukomba pesa toka kwenye biashara.....
* Acha kucheka cheka na nyani... Watu wanahangaika kupata mitaji miaka nenda rudi wewe unauchezea utakuja JUTA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hutokuja kuendelea kwa mentality hiyo. Nenda kwenye biashara zako zote sema anayeruhusiwa kutoa hela ni wewe au mke wako full stop. Huu undugu mkiuendekeza sana mtaishia kufa masikini, ndugu hawaishiwi shida alafu wengi wao wavivu hua hawajishughulishi. Tatizo lako unawabembeleza ndugu, wamekukosea heshima waweke kwenye mstari waache ujinga.
 
Hii nakumbuka wakati napitia nyaraka za kihasibu ilikuwa inajulikana kama "Entity Concept"

Hii kitu ina apply katika uhalisia na kiukweli ukikiuka hio kanuni ujue umevunja miiko ya kihasibu na biashara lazma itayumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…