Kwasasa katika Nchi yetu Viwanda viiiiiiiiingi vya Vifaa vya Ujenzi ka Tiles, Mabomba, Cement, Mabati, White Cement, Azam Juice, Yebo Yebo, Ndarra nk nk vipo na vinaendelea kujengwa Wilaya ya Mkuranga na Mkoa wa Pwani kwa ujumla.
So utapata kazi za Vibarua Viwandani, Kwenye Site za Ujenzi wa Viwanda kuna Vibarua vya Ujenzi. Lkn nje ya hapo Wenye Uwezo wengi na wanaomiliki mashamba kutokea Dsm mashamba yao yapo Mkuranga wakilima Mihogo, Minazi, Nanasi na Tikitimaji, hivyo endapo wewe ni mwaminifu utapata kazi za Shamba Boy kwa urahisi.
Makabila ni Wazaramo, Wakwere, Wandengereko nk