Biashara zinazofanyika Mkuranga

Biashara zinazofanyika Mkuranga

Juan-Gonzalez

New Member
Joined
Sep 15, 2022
Posts
2
Reaction score
2
Wana JF,

Naomba kuuliza shughuli zinazofanywa kwenye wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani. Ni miji ipi ipo kwenye hiyo wilaya, utamaduni wa watu wa huko ni upi na ni watu wa kabila gani wanapatikana katika wilaya hiyo.

Nataka niende huko nikafanye maisha naombeni msaada kwa wenye taarifa kuihusu Mkuranga.
 
Huko wamakonde, wangindo, wazaramo, wamakua ... kiufupi wote wa kusini na Pwani wapo huko.

Wengi hawapendi kulima, uvivu wa pwani so kama wewe ni mkulima ukienda utafaidika zaidi, ardhi nzuri mno na ni karibu sana na Dar.

-Mkaa
-Mihogo ni mingi
 
Kwasasa katika Nchi yetu Viwanda viiiiiiiiingi vya Vifaa vya Ujenzi ka Tiles, Mabomba, Cement, Mabati, White Cement, Azam Juice, Yebo Yebo, Ndarra nk nk vipo na vinaendelea kujengwa Wilaya ya Mkuranga na Mkoa wa Pwani kwa ujumla.

So utapata kazi za Vibarua Viwandani, Kwenye Site za Ujenzi wa Viwanda kuna Vibarua vya Ujenzi. Lkn nje ya hapo Wenye Uwezo wengi na wanaomiliki mashamba kutokea Dsm mashamba yao yapo Mkuranga wakilima Mihogo, Minazi, Nanasi na Tikitimaji, hivyo endapo wewe ni mwaminifu utapata kazi za Shamba Boy kwa urahisi.

Makabila ni Wazaramo, Wakwere, Wandengereko nk
 
Pwani yote ni oya oya tu..mana ni lango la dsm..chamsingi fika explore hizo fursa kwa macho yako.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom