Bibi Aondoka Baada ya Siku 30, Mume Adai Refund ya Sh1.16M ya Mahari, Mbuzi, Chakula na Pombe

Bibi Aondoka Baada ya Siku 30, Mume Adai Refund ya Sh1.16M ya Mahari, Mbuzi, Chakula na Pombe

Omu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
469
Reaction score
95
Mwanaume mmoja wa Machakos aliingia kwenye ndoa ya Kamba customary akiwa ametumia zaidi ya Sh1.16 milioni, lakini ndani ya mwezi mmoja, ndoa ilikuwa imevunjika.

Alienda mahakamani akitaka si tu divorce, bali pia refund ya Sh1,169,650 aliyosema alitumia kwa mahari, mifugo, chakula, sherehe, mavazi na transport.

Lakini Wamunyu Law Courts ikasema: si kila kitu kilichotumika kwenye harusi kinaweza kurudishwa.

Court records zinaonyesha SWM na MNS walifanya Ntheo na Ngasya ceremonies Novemba 7, 2025. Takriban mwezi mmoja baadaye, mke alikata mawasiliano na kusema hataki kuendelea na ndoa. Attempts za familia kuwapatanisha hazikufaulu.

Magistrate Pascal Nabwana alikubali kuwa ndoa ilikuwa irretrievably broken down na akaivunja.

Lakini refund? Hapana.

Among the items SWM alitaka kulipwa ni goats zilizochinjwa kwenye sherehe, beer, soda na chakula kilicholiwa na wageni. Court ilisema hizo zilikuwa customary gifts na entertainment expenses—si returnable dowry.

Pia alidai Sh80,000 ya PA system, Sh180,000 catering, Sh100,000 mavazi na Sh300,000 transport na fuel. Court ilisema hizo ni logistical choices za kufanya sherehe, si mahari chini ya Kamba customary law.

Zaidi, mahakama ilisema dowry disputes hazipaswi kuanza moja kwa moja kortini. Kwa Akamba tradition, kwanza kuna clan elders, auditing ya gifts na customary return processes.

Kwa hiyo baada ya ndoa ya siku 30, SWM alipata divorce-lakini si Sh1.16M yake.

Na hili linaibua swali:

Ndoa ikivunjika muda mfupi baada ya customary marriage, ni sehemu gani ya mahari inapaswa kurudishwa, na ni gharama gani mtu anapaswa kukubali zimekwisha mara sherehe inapomalizika?

tKPkl_tf.jpg
 
Back
Top Bottom