Nabii koko
Member
- Aug 16, 2022
- 21
- 15
Ukizungumzia mavazi ya kisasa ya wanawake, basi DELA ama kama wengine wanavyoliita DILA halibaki nyuma, na lenyewe utaliona kimbelembele kuliko hata mbele yenyewe. Vazi hili limejizolea wafuasi lukuki katika siku za hivi karibuni Tanzania hususani mwambao wa pwani na hasa mikoa ya Tanga, Dar es Salaam Pwani na viunga vyake na baadaye kushika kasi maeneo mengine ya nchi kama vile Morogoro, Iringa na Mbeya.
Usiulize kwanini dela na sio 'vijora' vingine? Jibu ni kwamba dela ni dela na litabiki kuwa hivyo kutokana na sifa zake. Yapo madela membamba na manene kama mfuko wa mashineni. Yapo yaliyonyooka mithiri ya bomba la maji na yaliyokatika kiuno kama nyigu. Yapo ya kola na yasiyonalo, ya maua maua na ya rangi moja mfano wa kanzu. Mengine, hata rangi nishidwa kuielezea: kipepeo si kipepeo, kiwavi si kiwavi. Aidha, dela linaweza kunyumbuliwa nyumbuliwa kuchukua kila sura na bado likakukaa kutegemeana na matumizi yako kama kwa wajawazito, ibadani, harusini, mitaani na maeneo mengine chungu mzima.
Lakini... licha ya sifa ambazo dela limejaaliwa, nina imani utakubaliana na ukweli kwamba DELA LINA WATU WAKE...watu wenye mwendo na 'shape' zao. Ndiyo maana wakunena walinena: UZURI WA DELA... TAKO. Hii ni katika kuthibitisha kwamba matumizi yake yazingatie 'muktadha'. Ukikurupuka ukajitupia tu bila kusema na kioo kikakwambia ukweli unaouma kwamba linanipwaya, utaonekana kituko. Unaweza ukalazimisha kuvaa halafu mtaani kila jicho linakufuta akadhani wanastaajabia, kumbe wanasemezana "Mh, huyu naye!"
Hivi ndivyo ninavyojiona pindi nitokeapo dela lako bibi, dela la kuazima lisilositili makalio yangu kwa kila namna. Je, ni furaha yako kuniona nikiogelea na kutapatapa ndani mithili ya njiti ya kiberiti katika kasha? Ama n'navyoenda nikielea utadhani boya juu ya bahari, vazi likin'tepeta kama sanamu ya kufukuzia ndege majarubani hiyo ndiyo burudani yako? Sasa nasema hivi, BIBI EE, DELA KAKO LINAN'PWAYA!
Hivi, tuanatambua kuwa mfumo wa Sasa wa elimu yetu ni zao la wakoloni? Tumeiga!Tumeiga bila kuzingatia kuwa malengo ya elimu yao yalikuwa ni kuwanufaisha wenyewe. Mfano, Wajerumani ililenga kuwaandaa watumishi wa ngazi za chini za serikali na wahitimu waweze kuzalisha kwaajili ya uchumi wa Wajerumani. (https://kaskazitz.blogspot.com/2018/06/1)
Sisemi ni vibaya kuiga, lakini tuige vile vizuri vinavyotekelezeka kulingana na uwezo na sifa zetu Kama Watanzania. Tunawezaje kumfanya mwanafunzi wa kileo aweze kujitegemea, kuwa mzalendo, mwenye kudumisha maadili na utamaduni wa mtanzania pindi anapohitimu masomo ilihali tunaendelea kumrithisha mizimu ya wazungu kupita masomo yetu?
(1)Mfano mzuri, kidato Cha kwanza katika Soma la historia wanasoma mada ndogo "Contacts with Europe" kutoka mada "3.AFRICA AND THE EXTERNAL WORLD". Mada hii inamtaka mwanafunzi kutambua bidhaa zillizobadilishwa katika biashara Kati ya Wareno na Waafrika. Je inamsaidia nini mwanafunzi katika kukabiliana na changamoto za Maisha katika mazingira yake hususani kiuchumi kwa sasa?
(2)Kidato Cha tatu mada ndogo (Historia) "Sectors of colonial economy" kutoka mada kubwa "COLONIAL ECONOMY" Inamtaka mwanafunzi atambue sekta mbalimbali za uchumi wa kokoloni mathalani, viwanda, kilimo, biashara, uchimbaji madini, mawasiliano na uchukuzi na kadharika. Swali ni je, uchumi huu anaojifunza ni wake, wetu ama wa kikoloni? Ili iweje? Mwanafunzi wetu, anabeba mambo mengi wakati anayotumia ni kiasi. (Tazama viambatanisho kutoka katika muhtasari wa sekondari mwisho>>)
Labda tujiulize, tunakumbuka kabla ya ujio wa wakoloni ni aina gani ya elimu mababu zetu waliirithisha kwa vizazi vyao? Inawezakana umesahau kuwa mababu zetu watufundisha elimu kwa vitendo, elimu iliyosawiri mazingira halisi waliyoishi. Mfano mzuri ni Wasani, Wasandawe, Wairaq, Wamasai na wengineo walijihusisha na shughuli za uwindaji, ukusanyaji na baadaye uhunzi, ufugaji, uvuvi na kilimo. Mababu hawa hawakubakiza ujuzi wao kichwani mwao, bali walirithishana vizazi na vizazi kwa mafanikio. Hii ni kwa sababu walifundishwa stadi zinazoshabihiana na mazingira yao.
Hapa nisinukuliwe vibaya, simaanishi turudi kwenye enzi za wimbombo na ulindi, la hasha. Ninachotaka, elimu ya Tanzania izingatie mazingira tunayoishi, wakati pamoja na uwezo na mahitaji yetu. Kama ni elimu ya ufugaji imlenge zaidi mfugaji kuliko mimi ambaye ukanda wangu ni wa kilimo. Mikoa inayozunguka maeneo ya Mito, maziwa, na bahari Kama vile Tanga, Mwanza, Kigoma, Rukwa, Lindi na Mtwara Wafundishwe darasani na kwa vitendo kwenye Mito, maziwa na bahari. Mwanafunzi yangu utotoni amjue samaki, aina za samaki, maisha ya samaki, chakula cha samaki, faida na changamoto za shughuli zinazohusu samaki, namna ya ufugaji binafsi wa samaki. Wajue njia bora na salama za uvuvi na mwisho wapewe nyenzo bora za uvuvi. Hata haya matumizi ya makokoro na baruti hayatakuwepo kwani mhusika tayari anjua athari zake kimazingira. Upungufu wa mafuta ya Kula na sukari tungesikia redioni.
Kuwe na mtaala mmoja unaojumuisha mitaala midogo midogo. Mtaala mkuu ubebe masomo ya pamoja Mfano Uraia, sayansi na teknolojia pamoja na utamaduni wetu kama vile lugha. Mtaala mdogo uwalenge wanajamii mahsusi kulingana na Ukanda wao. Pia achague kusoma ama kutokusoma fani nyingine mfano ufundi, ubunifu na sanaa, biashara na michezo. Hii shida ya wasomi wanaoongezeka mtaani kila mwaka wakiwa wameacha shimo la umaskini kwa wazazi wao kwa kusomeshwa kwa kuuza meza, vijiko, viti na masufuria majumbani mwao halafu mwisho tunawakejeli kwa kutaka wajiajiri bila mtaji, isingekuwepo!
Watengeneza mitaala na waandaa sera wana wajibu wa kupunguza mzigo masomo mengi, Kufanya tafiti za kutosha juu ya elimu itakayomsaidia mnufaika kujitegemea. Kuandaa mtaala wa muda mrefu kwa kufuata sera na falsafa ya nchi. Aidha, kuhakikisha kinachofundishwa kihusiane na jamii inachotaka kwa wakati huo. Tufute vitu vilivyopitwa na wakati kama kumuuliza mwanafunzi uandishi wa Simu za maneno (Telegram) katika ulimwengu huu wa teknolojia ya kidigiti, badala yake ajifuze namna ya kutumia email, fax, na vifaa vya kisasa vya kielektroniki.
Kama tunataka kuifikia Kanaan, hatuna budi kugeuka na kufuata kasi ya dunia. La sivyo tutaendelea kuyumbishana kwa kubadili mitaala na mifumo ya elimu kwa kufuata hisia, mihemko na manufaa ya mtu binafsi kwa kutegemea ameamkaje siku hiyo. Hiyo ndiyo njia pekee ya kutengeneza mstakabari bora wa vijana na taifa letu lakini kwa sasa, hili DELA LAKO LINAN'PWAYA!

Attachments
Upvote
1