Bibi harusi ajifungua kanisani

Hata hivyo, kutokana na hali hiyo bwana harusi alilazimika kufunga ndoa na msichana mwingine wa pembeni kwa niaba ya bibi harusi, ili kuhalalisha sherehe hiyo huku bibi harusi mwenyewe akiwa hospitali analea.
[/QUOTE]
sasa itakuwaje kama huyo aliye funga nae ndoa aking'ang'ania kuwa yeye ni mke halali maana kuolewa tabu sana siku hizi
 
Makanisa sasa yaanzishe utaratibu wa kutofungisha ndoa kwa wenye ujauzito
 
hiii NIKAWAIDA YA WACHAGA MIMBA HALAFU NDOA!
JAMAA WANAOGOPA KWELI KULISK!
 
Dini za kweli zimebaki rohoni, uwezi kwa maadili ya kikristo ukafungisha ndoa watu wameshapeana ujauzito, maana yake wamesha zini na kuvunja amri ya saba ( nasisitiza ya saba na siyo ya sita kama wengi tulivyokariri), so! Makosa ni ya makanisa na viongozi ambao wameacha the reality of the holy bible..shame on them
 
niliwahi kusikia kuwa gauni jeupe linamaanisha bibi harusi ni bikira lol
 
Katika hali isiyo ya kawaida bibi harusi alishikwa na utungu wa kuzaa wakati akifungishwa ndoa kanisani huko tanga baadae alikimbizwa hospitali ambapo alijifungua njiti wa miezi 7 wa kike. Hoja yangu ni Je, Kwanini siku hizi wote wanaonda kanisani kufunga ndoa tayari mwanamke anakuwa na mimba, pili je dhumuni la ndoa ni kuzaa watoto peke yake? Naomba mawazo yenu.
 
Hii si sawa na thread ya Fidel mwingine tena Tanga??? Makubwa haya
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Bibi harusi ashikwa uchungu, ajifungua kanisani Muheza [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Thursday, 11 August 2011 21:16 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg

Mwandishi Wetu, Muheza
BIBI harusi aliyefahamika kwa jina la Mariam Shabani, ameshikwa na uchungu wa kujifungua kanisani wakati akifungishwa ndoa na mchumba wake, aliyefahamika kwa jina la Deo Massawe.Tukio hilo lilitokea juzi Kanisa Katoliki lililopo maeneo ya Majengo Shimoni, wilayani Muheza, huku umati wa watu ukiwa umejaa ndani ya kanisa hilo ukiisubiri kufungwa kwa ndoa hiyo.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia tukio hilo ndani ya kanisa hilo, wakati Padri Martin Kihiyo, akiendelea na misa ya kufungisha ndoa hiyo, ghafla bibi harusi akiwa amevaa vazi rasmi la harusi, alianza kupiga kelele akidai anasikia uchungu wa kujifungua.

Hata hivyo, baada ya bibi harusi huyo kupiga kelele, Padri Kihiyo alisitisha misa hiyo na Mariamu kuchukuliwa haraka na kuwekwa kwenye gari huku akiwa hajiwezi hadi Hospitali Teule Muheza.Pia, Mariamu anafahamika kwa jina la Sada Shabani, baada ya kufikishwa hospitali alipelekwa chumba cha kujifungulia huku akiwa na vazi lake la harusi.

Baada ya kuhudumiwa Mariamu, alijifungua mtoto wa kike na kulazwa wodi ya Azimio wanakolazwa wazazi.
Mmoja wa muuguzi hospitalini hapo aliyeomba asitajwe, alisema bibi harusi huyo alijifungua njiti akiwa na miezi saba.Kwa upande mwingine, kwenye ukumbi ambao ulikuwa umeandaliwa kwa sherehe ya harusi hiyo, watu walikuwa wamekaa ndani wakisubiri maharusi bila kufahamu kilichokuwa kikiendelea.

Hata hivyo, kutokana na hali hiyo bwana harusi alilazimika kufunga ndoa na msichana mwingine wa pembeni kwa niaba ya bibi harusi, ili kuhalalisha sherehe hiyo huku bibi harusi mwenyewe akiwa hospitali analea.

Inasemekana Mariamu alianza kusikia uchungu akiwa saluni na aliwaeleza baadhi ya watu, lakini walimjibu kuwa huo ni woga wa harusi.Katika hatua nyingine, mbuzi wa ndafu aliyekuwa ameandaliwa alianguka chini kwenye mchanga.

Baadhi ya Wakristo walisikitishwa na tabia ya viongozi wa dini kuendelea kuwafungisha ndoa watu ambao wake zao wana mimba kwamba, ni aibu.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 

hao wanaojifungulia makanisani hawajui au hawajazisikia busara zilizomo kwenye hayo maandiko mekundu............
 
Yaani hii staili ya siku hizi inashangaza kwa kweli....
 
ndoa za siku hizi bana mpaka wa2 wa.ch.ak.a.ch.u.e wahakikishe wanafunga ndoa bibi akiwa ni mjamzito, hii ni dhambi,
 
niliwahi kusikia kuwa gauni jeupe linamaanisha bibi harusi ni bikira lol
Na mpaka sasa ndivyo ilivyo......

mambo ya offside trick haya
Hebu nawe hebu tuondolee sihasa kwenye jukwaa letu pendwa....

Ndo nini hiki hapa chini na kinahusiana nini na mautamu?

Chama Cha Mapinduzi...Hakitodumu,
Wala hakina sababu ya kudumu!
 
Na mpaka sasa ndivyo ilivyo......

Hebu nawe hebu tuondolee sihasa kwenye jukwaa letu pendwa....

Ndo nini hiki hapa chini na kinahusiana nini na mautamu?

Chama Cha Mapinduzi...Hakitodumu,
Wala hakina sababu ya kudumu!



ha ha ha haaaa.. babu hicho kihisishi tu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…