Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
BIBI TITI MWANAMKE SHUJAA
Labda kama ingekuwa si Bibi Titi Mohamed nisingefahamiana na Mh. Mohamed Mchengerwa.
Mh. Mchengerwa ndiye muasisi wa Tamasha la Bibi Titi.
Labda kama isingekuwa Tamasha la Bibi Titi Mohamed nisingefahamiana na Mh. Mchengerwa na pengine wengi tusingefika Ikwiriri hadi leo.
Inahitaji kuona kwa macho yako mwenyewe Tamasha la Bibi Titi katika Uwanja wa Ujamaa ndiyo utaelewa ushawishi wa Bibi Titi kwa watu wa Rufiji.
Hili ni tamasha langu la tatu mimi kuhudhuria na kila tamasha linazidi lililotangulia.
Wakati wa Tamasha Ikwiriri yote inasimama.
Wafanyabiashara zote wanakuwa wamesimama wima kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora na wao wananufaika na ugeni unaoingia mjini.
Huu unakuwa wakati wa nema kubwa Ikwiriri na Rufiji yote.
Haijatokea kiongozi mpigania uhuru wa Tanganyika akaenziwa namna leo Bibi Titi anavyoenziwa Rufiji.
Hakika hii ni kumbukumbu ya pekee na inayomtendea haki kiongozi huyu mwanamke aliyeingiza katika TANU jeshi kubwa la wake kwa waume kwa namna yake ya hotuba zake za kuwahamasisha ujasiri Watanganyika wasimame katika umoja wao hadi Mwingereza arudi kwao.
Naam Mwingereza alirejea kwao kwa amani na salama.
Bibi Titi aliinufaisha TANU katika uhai wake.
Bibi Titi ameinufaisha pakubwa historia ya uhuru wa Tanganyika leo wakati hatunae tena duniani.
Historia ya Bibi Titi huwezi kuihadithia bila kueleza historia yenyewe kama ilivyokuwa TANU ilipoanza kudai uhuru wa Tanganyika.
Ukipenda unaweza ukarudi hadi mwaka wa 1950 wakati vijana wa wakati ule walipofanya mapinduzi ya kutoa katika uongozi kizazi cha Wajerumani na kuingiza kizazi kipya cha utawala wa Waingereza.
Bibi Titi ni sehemu ya viongozi vijana walioingia katika siasa za kudai uhuru wa Tanganyika kuanzia kipindi hicho.
Inastaajabisha kuwa aliyesimamia mabadiliko haya Schneider Abdillah Plantan hajatajwa popote katika historia ya uhuru ingawa yeye ndiye aliyewaleta katika TANU Bibi Titi Mohamed na shoga yake kipenzi Tatu bint Mzee.
Kabla yake ni huyu Schneider Plantan aliyewapigania Dr. Vedasto Kyaruzi na Abdulwahid Sykes kuingia katika uongozi wa TAA mwaka wa 1950 kuchukua nafasi ya uongozi wa Thomas Saudtz Plantan na Clement Mohamed Mtamila.
Kupitia maisha ya Bibi Titi ndipo inapopatikana historia ya kweli ya TANU na historia ya Julius Kambarage Nyerere.
Wangapi wanajua kuwa Bibi Titi alipanda jukwaani kuhutubia mkutano wa TANU Mnazi Mmoja sura ya Nyerere haijui inafananaje?
Huyu ndiye Bibi Titi ambae anaeanziwa Ikwiriri kila mwaka.
View: https://youtu.be/I6TFC3QIeWQ?si=ez3cHccJaMgzoEgV