Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
BIBI TITI MOHAMED NA LUCY LAMECK
Kushoto ni Bibi Titi Mohamed na kulia ni Lucy Lameck wakiwa China na Mao Tse Tung.
Hii picha kaniletea dada yangu mmoja ambae aliona nimeweka picha ya safari ya kwanza ya Nyerere UNO 1955 na katika picha hiyo yuko Bibi Titi na Lucy Lameck lakini nimesema sina jina la msichana mdogo aliyekuwa kasimama pembeni ya Nyerere.
Dada yangu akaniandikia akaniambia kuwa huyo ni Lucy Lameck.
Nikamuomba ithibati ya taarifa hii kuwa huyo msichana ni Lucy Lameck.
Jibu lake lilinisisimua sana.
Aliniandikia: "Ni Lucy Lameck nina uhakika bila kupepesa."
Kuna mtu alipata kuniandikia kunieleza hilo lakini sikumuamini.
Nikamuuliza dada yangu kutaka uhakika zaidi kipi kinachomthibitishia yeye kuwa huyo msichana ni Lucy Lameck?
Soma jibu aliloniandikia: "Ninamtambua sana.
Nilikuwa karibu nae toka 1967 na hata alivyokuwa anatibiwa London alipenda kufikia kwangu...
Tafuta picha zake zingine utaona kama kutakuwa na tofauti.
Hata style ya vazi lake ni yeye..."
Kwa miaka mingi nilikuwa katika picha hiyo ya pili natafuta majina ya wanawake hawa wawili - jina la huyu msichana na huyo mwanamke mwingine aliyesimama katikati ya Bibi Titi na Julius Nyerere.
Kwangu mimi kuwa huyu bint mdogo ni Lucy Lameck hii ni "Eureka."
Mwaka wa 1955 akina mama hawa wawili walipokuwa Uwanja wa Ndege wa Dar-es-Salaam wakimsindikiza Julius Nyerere safari yake ya kwanza UNO wakati huo wakipigania uhuru wa Tanganyika hawakujua historia ilikuwa imewawekea kitu kipi katika maisha yao.
Hawakujua kuwa wakiwa pamoja na viongozi wakubwa watakuja kupiga picha na Chairman Mao Peking na nchi wanayotoka haitakuwa Tanganyika bali Tanzania.