Hii ni kamba, mwongo mkubwa!
Kwanza, Bibi Titi hakumleta Nyerere TAA, na wala si Kawawa. Pia, Waislam na Wakristo ni wote walishiri kwenye harakati za Uhuru.
Bibi Titi hakuwepo kwenye picha wakati wa TAA, wala TANU ya mwanzo. Bibi Titi ndio aliletwa kukutana na Nyerere, 1955, na dereva Taxi aliyejuana na shemeji wa Bibi Titi. Baadae, shemeji wa Bibi Titi akawa anamsukuma Bibi Tibi ahudhurie mikutano ya Nyerere, na baadae akavutiwa nae, akapewa kadi namba 16. Nyerere alikuwa na kadi namba moja.
Na Kawawa alikuja TANU akitokea vyama vya wafanyakazi mwaka 1958, four years behind the curve!
Na madai yako mengine ya Wakristo vs Waislam ni uwongo wa kuchomwa moto. Wakristo na Waislam walishiri bega kwa bega katika harakati. Walionzisha TANU wako 17, wa dini zote:
(1)Mwalimu J.K. Nyerere Mwenyekiti
(2)Geremano Pacha
(3)Joseph Kimalando
(4)Japhet Kirilo
(5)C.O. Milinga
(6)Abubakari llanga
(7)L.B. Makaranga
(Saadani A. Kandoro
(9)Suleman M. Kitwara
(10)Kisunguta Gabara
(11)Tewa Said Tewa
(12)Dossa A. Aziz
(13)Abdu Sykes
(14)Patrick Kunambi
(15)Joseph K. Bantu
(16)Ally Sykes
(17)John Rupia
Na ukienda nyumba zaidi, hata viongozi wa Kitaifa wa TAA walioanza kutuma madai ya kimaandishi ikulu ya Sir Edward Twinning kudai chama kitambulike kwa uwakilishi Bungeni walikuwa ni Mwenyekiti na Katibu Mkuu, TAA Taifa, Abdulwahid Sykes na Vedastus Kyaruzi respectively.
Hiyo ni kabla na wakati wa uundwaji wa TANU. Baada ya kuundwa, TANU ili recruit viongozi wa harakati kutoka viongozi wa vyama vya ushirika, Nsilo Swai, Sir George Kahama, Jeremiah Kasambala, Paul Bomani, John Mhavile, na wengine.
Kwa hiyo, kusema TANU ilikuwa ya Waislam waliokaribisha Wakristo ( or vice versa ) ni urongo, uzandiki.