Bibi wa miaka 50 afariki akiwa kwenye foleni ya kupiga kura KENYA

Mimi namuona shujaa anayetambua umuhimu wa kutekeleza haki yake kikatiba.Mwenyezi Mungu amrehemu, amen
 

Mkuu kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sawa ni bibi wa miaka 70 na sio 50!
 

Mkuu hapo ndo ujue kwamba wakenya haki zao wanazijua
 
Wakuu vipi matokeo ya uchaguzi kenya nani anaonekana kupaa?
 
Tatizo la lugha.. Grandmother huko Kenya anaitwa "nyanya" tofauti na Tz ambapo huitwa "bibi". Matumizi ya neno "bibi" zaidi humaanisha mke wa mtu (mrs)..
RIP bibi!
 
Hivi unasema bibi ukimaanisha kikongwe, au ukimaanisha mwanamke ie bibi yangu ana mimba?
 

Alikuwa na miaka 72
 
Duh miaka 50 bibi? Hapana wakati kwa MA- CCM huyo ni Kijana.

Hicho ni kiswahili cha wenzetu wakenya, huwa wanaita wanawake bibi, na wanawake wazee wanawaita nyanya. ndio maana ukiwa kenya ukisikia mtu anakuambia bibi yangu mgonjwa usifikiri anamaanisha grandma, akimaanisha grandma atasema nyanya yangu mgonjwa.
 
Mimi nimesikia BBC swahili, ni bibi wa miaka 70 ndo amefariki katika hospitali ya wilaya, baada ya kukimbiziwa huko mara baada ya kuanguka akiwa kwenye foleni ya kwenye kituo cha kupigia kura.
 
5O ni mtu wa makamo ana uwezo wa kuzaa watoto hadi 3
 
miaka 50 bado binti si bibi huyo. miaka 50 siku hizi ndo umri wa kuolewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…