Mkazi wa Kitongoji cha Ganana A, Kata ya Ganana, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, Yasinta Amnaay (68), anadai eneo lake lenye ukubwa wa ekari moja na robo lilipimwa na kuuzwa bila kushirikishwa.
Kwa mujibu wa Bibi Yasinta, amekuwa akimiliki eneo hilo tangu mwaka 1975 wakati wa Operesheni Vijiji, baada ya kupewa na Baltazary Buhai, ambaye sasa ni marehemu. Amesema hajui kusoma wala kuandika, hali inayompa ugumu wa kufuatilia haki yake.
Soma zaidi:Wananchi walalamika kuchangishwa fedha ununuzi wa picha ya Rais na Bendera ya Taifa,Hanang
Bibi huyo amesema mazao yake, yakiwemo ngwara na mbaazi, yaliharibiwa baada ya eneo hilo kuchukuliwa. Anadai amefikisha malalamiko yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Almishi Hazali, Mkurugenzi wa Halmashauri na baadaye kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
Kwa mujibu wake, tarehe 18 Desemba 2025, Mkuu wa Mkoa wa Manyara alielekeza eneo hilo lifanyiwe tathmini, alipwe fidia kwa mazao yaliyoharibiwa na apatiwe eneo lake au eneo mbadala, lakini anadai maelekezo hayo hayajatekelezwa hadi sasa.
Walalamikaji pia wanadai kuwa baadhi ya viongozi wa ngazi ya wilaya pamoja na watu wenye uwezo mkubwa kifedha wamenufaika na viwanja vilivyopimwa katika eneo hilo. Aidha, wanadai Mkuu wa Wilaya alimwonya Bibi Yasinta kuwa akirudishiwa eneo hilo halafu akaliuza angechukuliwa hatua za kisheria. Pia wanadai Afisa Ardhi wa Wilaya ya Hanang, Erick Mbeya, hakutoa ushirikiano katika kushughulikia malalamiko yake.
Source:KUSAGA TV