Mkuu wa Mkoa wa Arusha , ameahidi kutoa Bajaji mpya na runinga kwa Bi. Arafa Yusuph Matoke (74),ambaye ni miongoni mwa maelfu ya wanawake wanaoshiriki shamrashamra za kuelekea Kilele cha siku ya wanawake Machi 08, 2025.
Kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha leo Machi 02, 2025 kunapofanyika shamrashamra hizo pamoja na msaada wa kisheria wa Mama Samia, Bi. Arafa amekuwa miongoni mwa walioshiriki michezo mbalimbali kwa wanawake ikiwa ni pamoja na kukimbia na gunia.