Bibi yangu alipoenda Hospitali ya Amana Dar, alilazimishwa kuchanjwa

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2016
Posts
1,281
Reaction score
1,251
Wadau naomba kujua Kama Hospitali za serikali kwenye maeneo yenu zina huu Utaratibu. Bibi yangu Alikuwa hajisikii vzr, wajukuu zake wawili wakampeleka AMANI HOSPITALI.

Walimuuliza Bibi ushachanjwa? Akawaambia Bado, wakamwambia hadi achanjwe ndo wamtibu. Ilibidi achanjwe hapohapo. Kumbe hii kitu ni kulazimishana kiac hii. Makwenu huko kukoje?
 
Tulisema sisi hiyo hangaya alisema hiyari ni hiyari ya kulazimisha yaani tutauzwa muda sio mrefu.
 
Kwa nini alikubali ikiwa hataki kuchanja?
 
Wengi wanasema ukichanja unadhurika/ kufa. Je hali ya bibi vipi? MKACHANJE
 
Anti yangu alichoma hiyo chanjo bila kulazimishwa, alijipeleka mwenyewe, yeye ni kiongozi alitaka kuonesha mfano, sasa hivi anajuta kwanza siku hiyo mkono ukavimba

Baada ya siku tatu kengele zinapiga kichwani yaani kila siku kuna jipya anajuta sana.

Binti mwingine kaenda kutoa jino kaambiwa hawezi pata huduma kwanza apate chanjo.

Nyie chanjo ni lazima sio utashi wako.
 
Wadau naomba kujua Kama Hospitali za serikali kwenye maeneo yenu zina huu Utaratibu. Bibi yangu Alikuwa hajisikii vzr, wajukuu zake wawili wakampeleka AMANI HOSPITALI. walimuuliza Bibi ushachanjwa? Akawaambia Bado, wakamwambia hadi achanjwe ndo wamtibu. Ilibidi achanjwe hapohapo. Kumbe hii kitu ni kulazimishana kiac hii. Makwenu huko kukoje?
Ulitaka asichanje ili wasimpe matibabu?
 
Wadau naomba kujua Kama Hospitali za serikali kwenye maeneo yenu zina huu Utaratibu. Bibi yangu Alikuwa hajisikii vzr, wajukuu zake wawili wakampeleka AMANI HOSPITALI. walimuuliza Bibi ushachanjwa? Akawaambia Bado, wakamwambia hadi achanjwe ndo wamtibu. Ilibidi achanjwe hapohapo. Kumbe hii kitu ni kulazimishana kiac hii. Makwenu huko kukoje?
Kwenye vituo vyote vya kutoa huduma za matibabu za umma kwa sasa kabla ya kupewa huduma habari ya chanjo ndiyo inayotangulia sasa sijui ukikataa unapewa tu matibabu au unakataliwa
 
Chanjo ni sehemu ya matibabu
 
Kwenye vituo vyote vya kutoa huduma za matibabu za umma kwa sasa kabla ya kupewa huduma habari ya chanjo ndiyo inayotangulia sasa sijui ukikataa unapewa tu matibabu au unakataliwa
Duh. Kumbe. Hali tete
 
Chanja ili uungizwe kwenye system ya ...
 
Back
Top Bottom