Anaefuatilia mambo ataona makosa yaliofanyika kutokana na kutafisiri biblia kutoka lugha yake ya asili kwenda lugha nyingine. Sababu za makosa hayo ziko wazi.
Ukiacha makosa ya kutafisiri pia sio maneno yote yaliyomo katika biblia ni maneno ya Mungu. Mengine ni maneno ya mwandishi mwenyewe.
Kwa hiyo ni muhimu unaposoma vitabu vya biblia kujua mwandishi wa hicho kitabu ni nani: historia yake. Kitabu kiliandikwa wakati gani na aliwaandikia kina nani, ujumbe wake ni nini.
Wayahudi ndio watu pekee duniani wenye utalaamu wa dini. Ndio wanaojua dini. Hatahivyo, katika historia yao ya dini mpaka leo wayahudi hawataji jina la Mungu.
Kitabu cha Kutoka kinaeleza kuwa Musa alipewa consonant "YHWH" - kama jina la Mungu. Matamshi hayo kwa yenyewe hayatamkiki kama neno lenye maana.
Kwa sababu wayahudi hawaruhusiwi kutaja jina la Mungu (YHWH), ili kuepuka kutaja jina hilo wanataja maneno Adonai, Elohim, kueleza sifa na ukuu; uwezo na matendo ya Mungu.
Kitabu cha Mwanzo 1:1, pamoja na kwamba kinaeleza tokeo la ulimwengu lakini fundisho lake kuu ni kuanguka kwa mtu. Kitabu hiki kinaeleza mambo msingi ili kuweza kujua si tu biblia, lakini pia uumbaji kwa ujumla.
Kumbe katika msingi huo ni muhimu kujua muhusika mkuu, ambaye biblia inamtaja kuwa muumbaji wa vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana, yaani Mungu.
Mungu maana yake ni nini?
Pili ni vitu vilivyoumbwa:-
Dunia ni nini?
Mbinguni ni nini?
Mtu ni nini?
Ulimwengu ni nini?
Maswali haya yatatuwezesha sio tu kuacha kushughulika na mambo madogo badala yake kushughulikia mambo ya juu na kuwa na maarifa ya vitu na ushahidi wao wa ndani.