Bible Mysteries: Q source iko wapi

Ushauri tu, tunapoangalia historia ya kale, detai ndogo kama hii tunaweza kuikosa ikatusababishia tukakosa, mbingu. Luka alijua anachoandika na ili asimchanganye Theofilo mtukufu, aliyekuwa mlengwa wa vitabu vyote viwili, ilibidi aweke bayana kwamba Yesu alizaliwa kwenye ile orodha (sensa) ya kwanza na si hii ya pili ambayo ilikuwa inakumbukwa zaidi na wayahudi (maana ilifanywa na warumi kutumia askari wao ambao walikuwa machikozo kwa wayahidi maana walimwabudu Kaisari na ngao zao na bendera zilikuwa na sanamu).
 
Kwa hiyo Yesu alizaliwa wakati wa sensa ya kwanza na Herode alikuwa hai, no contradictions!
 
UNABII WA DANIEL UNAONESHA VZR ATABATIZWA,KUUWAWA KATIKA MIAKA 27B.C NA 31B.C, HIVO UTAWEZA KUJUA PIA ALIZALIWA LINI

Danieli 9:25 “Basi ujue na kufahamu, ya kuwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake…”

Yerusalemu ulianza kujengwa upya katika mwaka 457 KK kwa amri ya mfalme Artashasta

Unabii unasema kutakuwa na wiki 7 kujumlisha wiki 62 jumla 69 kutoka kujengwa Yerusalemu mwaka 457K.K. hadi kuja kwa masihi. Katika unabii siku moja ni sawa na mwaka mmoja (angalia Ezekieli 4:6 na Hesabu 14:34), hivyo wiki 69 ambazo ni sawa na siku 483 zinamaanisha miaka 483 halisi; ambayo ingepita tangu kujengwa upya kwa Yerusalemu hadi kuja kwa Masihi.

Hivyo ukichukua miaka 483 ukaijumlisha katika mwaka -457 KK ambao Yerusalemu ulianza kujengwa, utapata mwaka 27 BK (-457 483 = 27); ambao Masihi angetiwa mafuta.



Je Mashi alitiwa mafuta mwaka 27 BK?

Matendo 10:38 “habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.”

Masihi = aliyetiwa mafuta.

Hivyo kulingana na unabii Yesu alibatizwa au kutiwa mafuta katika mwaka 27 BK mwishoni mwa wiki 69, na Luka anatuambia Yesu alikuwa na umri wa miaka 30 wakati anabatizwa 27 BK.

Luka 3:21, 23 “Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka; Roho Mtakatifu akashuka juu yake…Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,”

Hii ni kwa sababu Yesu hakuzaliwa 1 BK; kwani kalenda ilikosewa kama miaka 4.

Historia inasema Herode alikufa 4 KK, na tunajua Herode alitaka kumuua Yesu, hivyo Yesu alizaliwa 4 KK na katika 27 BK alipobatizwa alikuwa na umri wa miaka 30.

MWAKA -4 30 1 = Unapata hadi miaka 27 ya YESU anapobatizwa (Namba “1” ipo kwa ajiri ya mwaka “0”)

Hivyo Yesu alibatizwa mwaka 27BK. (majuma 69 au miaka 483) kutoka mwaka 457KK hadi 27BK. Hivyo unabii ulitimia kwa ukamilifu, kama ulivyotabiliwa kuwa tangu kujengwa Yerusalemu mwaka 457KK mpaka kuja kwake masihi kungekuwa na majuma 69 au miaka 483.

Kwa hakika Yesu mwenyewe alisema wazi kwamba unabii ulikuwa umetimia kikamilifu.

Marko 1:9, 14, 15 “Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani…Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu, akisema, Wakati umetimia…”

Yesu alijua kwamba mwaka 27BK. unabii wa Danieli ulikuwa umetimia.

JE YESU ALIKUFA LINI?

T
UMSIKILIZE TENA NABII DANIEL

Danieli 9:27 “Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja;…”

Yesu alipobatizwa ilikuwa ni wiki ya 69, hivyo katika wiki 70 zilizotolewa kwa ajili ya taifa la Israeli ilikuwa imebaki wiki moja tu muda wa rehema ya taifa lao uishe. Hivyo kwa muda wa juma hili moja lililobaki Yesu na wanafunzi wake waliitangaza Injili ya Mungu kwa Waisraeli pekee yao. Hawakutangaza Injili mahali pengine popote tofauti na Israeli. Yesu mwenyewe aliwaamru wanafunzi wake SOMA...
Mathayo 10:5, 6

Tumejua kwamba kwa juma moja Yesu angefanya agano na watu wengi, lakini Injili ingehubiriwa kwanza kwa Israeli pekee. Sasa Je juma moja linamaanisha nini?
Juma moja = siku 7. Katika unabii siku = mwaka, hivyo juma moja = miaka 7. Muda huu ulianzia mwaka 27BK alipobatizwa Yesu, na unaendelea mpaka 34BK (27+7 = 34).
Katikati ya juma.

Danieli 9:27 “…Na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu;…”

Juma zima = miaka 7, hivyo nusu ya juma ni miaka 3 na nusu (7 / 2 = 3.5). Ukihesabu miaka mitatu na nusu kutoka katika mwaka 27BK. aliobatizwa Yesu utapata mwaka 31BK. Hivyo Yesu angekomesha sadaka na dhabihu, au angesulubiwa msalabani, au “angekatiliwa mbali,” Dan. 9:26 katika mwaka 31BK. Kwa hiyo Yesu alifanya kazi yake ya utumishi kwa muda wa miaka 3 na nusu, tangu 27BK hadi 31BK aliposulubishwa msalabani.

Mathayo 27:50-51 “Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama pazia la hekalu lakapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;”
Pazia lilichanika kuonesha kwamba hatupaswi kutoa tena sadaka wala dhabihu kwa ajili ya msamaha wa dhambi na upatanisho; bali tunapaswa kumwangalia Yesu pekee kwa ajili ya vitu vyote hivyo.

Rehema kwa taifa la Israeli yaisha.

Juma moja la mwisho ambalo lilianza 27 BK lingeisha mwaka 34 BK, nusu ya juma ni miaka 3.5 ambayo Yesu alifanya kazi yake tangu 27 BK alipobatizwa hadi 31 BK aliposulubishwa. Hivyo katika juma la mwisho (la 70), ilikuwa imebaki nusu juma (miaka 3 na nusu) pekee ambayo ingeishia 34 BK; kwa ajili ya Wayahudi. Kama Wayahudi wangendelea kumkataa Mwana wa Mungu hadi 34 BK, ndipo Mungu angeuondoa ufalme kwao na kuwapa watu wa mataifa. Je Wayahudi walimkubali Yesu kabla ya mwaka 34 BK au waliendelea kuwa wakaidi? Wayahudi walithibitisha kuikataa kabisa rehema yao ya majuma 70 kwa kumwua Stefano katika 34 BK!

Matendo 7:56-59 “Akasema, Tazama? naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu. Wakapiga kelele kwa sauti kuu, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja, wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe…stefano, naye akiomba, akisema , Bwana Yesu, pokea roho yangu.”

Yesu alipopaa mbinguni wanafunzi wake waliendelea kuhubiri Injili kwa Wayahudi. Lakini majuma 70 yalipoisha katika mwaka 34BK, Wayahudi waliukataa wazi wazi ujumbe wa Injili kwa kitendo cha kumuua Stefano. Hivyo unabii wa Yesu ulitimia, Wakanyanganywa ufalme wa Mungu nao wakapewa watu wa mataifa.

Mathayo 21:43 “Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.”
Unabii ulitimia majuma 70 kwa ajili ya Wayahudi yalipoisha nao wakathibitisha kuikataa Injili, Mitume wakageukia kuhubiri kwa watu wa mataifa.

.

HITIMISHO;
YESU KAZALIWA MWAKA 4K.K, KABATIZWA MWAKA 27B.K AKIWA NA MIAKA 30,KAFA MSALABANI MWAKA 31B.K


Marejeo:
1. Kwa ushahidi kuhusu tarehe 457KK, ni mwaka wa saba wa kutawala kwake mfalme Artashasta, ambaye katika mwaka 457KK aliamuru mji wa Yerusalemu ujengwe; angalia, S.H. Horn na L.H. Wood, The Chronology of Ezra 7 (Washington, D.C.: Review and Herald association, 1953); na E.G.Kraeling, The Brooklyn Museum Aramaic Papyri (New Haven or London, 1953,) ukr. 191-193

 
Usipate shida sana. Biblia imeandikwa na wanadamu kuna historia, unabii,mashairi, n.k. msingi mkuu ukiwa ni ujumbe maalum.

Sijui ingekuwaje kama ingesemekana ilishushwa, halafu ukute kuna vitu humo havijakaa sawa.
Ingekuwa hatari kuu
 
: Brindle, Wayne, "The Census and Quirinius: Luke 2:2" (1984). SOR Faculty Publications and Presentations. 73. The Census and Quirinius: Luke 2:2.
Nimeisoma paper nzima na sijaona popote panapo na conclusive evidence ya Kulink Quirinius na ''census'' ya 5 BC na ndio maana conclusion yake ni hii hapa.

Lakini changamoto ni kwamba Luke 2:2 imefungamanisha sensa iliyofanyika na uwepo wa Quirinius kma Governor wa Syria (sio commander wa kijeshi as a secondment)



Luke is very clear (King James) kwamba Taxing was FIRST made when Cyrenius (Quirinius) alikua gavana wa syria ikimaanisha kama kuna sensa nyingine wakati wa Herode ni irrelevant maana haikufanyika hyu Quirinius akiwa gavana.

Alternative solutions za paper

Hapa muandishi anakiri Flavius Josephus (kumbuka hyu ndiye most credible historian enzi zile za Yesi ameondoka) kma Historical accurate zaidi hivyo kwa kudai kwake kuwa Quirinius ni governor kati ya 6-7 AD huko Syria haiwezi kuwa contested.

Sasa Basi huyi Flavius ambaye ndio most credible both kwa theologians na hii paper anasema kuna sensa ngapi?


So mpaka hapa Josephus anakubali sensa ni moja tu na sio vinginevyo.

Sasa basi conclusion ni kwamba paper imeshindwa kuonyesha kabisa relationship kati ya Sensa ya quirinius kufanyika wakati mmoja na Herode akiwa hai.

Lakini paper inakiri kwamba uwezekano wa sensa mbili kuwepo upo (Ambayo sijapinga)

Changamoto ni kwamba inashindwa kuthibitisha kwamba Quirinius alikuwepo Judaeah 5BC kma governor wa Syria!!

Hivyo paper haijajibu swali la msingi la co existence kati ya Herode, Sensa, na Quirinius.
 
Luka alijua anachoandika na ili asimchanganye Theofilo mtukufu, aliyekuwa mlengwa wa vitabu vyote viwili, ilibidi aweke bayana kwamba Yesu alizaliwa kwenye ile orodha (sensa) ya kwanza na si hii ya pili
Mkuu hakuna anayepinga uwepo wa sensa mbili nachopenda utufahamishe ni hiki
Je sensa ya kwanza/ pili Quirinius ali co exist na Herode?

Je sensa ya 5 BC ina maana Quirinius hakuwepo? na sensa ya 6 AD ina maana Herode hakuwepo?

Sasa basi hii sensa wakati Yesu anazaliwa ilikua ni ipi maana ukisema ya kwanza ilikua enzi za Quirinius ina maana ni 6 AD na kuendelea which renders Herodius irrelevant kwenye hii story and vice versa.

Karibu
 
Kwa hiyo Yesu alizaliwa wakati wa sensa ya kwanza na Herode alikuwa hai, no contradictions!
Paper uliyoweka inakiri kuwa sensa ya kwanza haikua documented popote. Can u adress this?

Pili luke 2:2 inadai Sensa ya kwanza Quirinius alikuwepo, ssa kivp tena sensa ya kwanza iwe enzi za Herode ilihali Krenio hakua governor?

Hii discrepancy ndio kiini cha debate
 
Hakuna tofauti kwa maana Kaisari ndio kiongozi mkuu na Herode alikuwa chini ya Kaisari.
 
Tukubaliane jambo moja kwamba Luka alikuwepo karne ya kwanza, aliandika kitabu chake wakati mashahidi wa haya yaliyotokea walikuwa hai, alichoandika kuhusu uwepo wa Kirenio kama "hégemoneuó" ambayo Strong ana define kama - "to command" na watafsiri wameitafsiri kama liwali au Gavana haitupi conclusion kwamba Luka alikosea au alichakachua kwa makusudi. Jambo la muhimu hapa ilikuwa kuonyesha uwezekano wa Kirenio kuwa na "comanding position" huko Syria wakati Herode akiwa mfalme. Kuhusu ushahidi ni kuwa very unfare ukitaka proff ya jambo ambalo witness ni watatu tu: Luka, Josephus, na Tacitus. Kukosekana ushahidi sio proof ya kutokuwepo tukio halisi. ni miaka 2020 na ushee imepita tangu hayo yatukie, kuna vitu sisi leo tunaweza kuviona ni muhimu ila kwa yule aliyeandika enzi zile wala hakuona ni kitu cha kufafanua maana kilikuwa wazi au trivial enzi hizo.

Labda nitoe mfano hai: tunajua Tanzania huwezi kuinfluence jambo kubwa kama katiba kama wewe ni raia binafsi, hata kama ni Rais mtaafu. fikiria baada ya miaka 2000 mtu anasoma historia ya Tanzania halafu amebakiza manuscript tatu tu zinazoelezea kuanza kwa vyama vingi halafu manuscript moja inasema Nyerere aliachia urais 1985, nyingine ikasema Mwinyi alikuwa Raisi kuanzia 1985 -1995. nyingine ikasema Nyerere alianzisha vyama vingi miaka ya 90 mwanzoni. Mtu akisoma haya wakati huo atakuwa na maswali kama unayouliza leo ila sisi hayo maswali hatuna kwa sababu tunajua power structure na political power aliyokuwa nayo Nyerere kwa hiyo tunaelewa.

Sasa tukija kwenye issue yetu ya Kirenio, Herode, sensa, na tarehe za hayo mambo hatuna rekodi zaidi ya hao mashahidi watatu ambao kila mmoja aliandika akikusudia yake. Kwa mfano Luka hakuwa na mpango wowote wa kutufafanulia kuhusu career ya Kirenio ila yeye alitaka Theofilo asichanganyikiwe kati ya hizo sensa tofauti. Na kwa mtu anayesoma anaelewa Luka asingeweza kuandika vitu ambavyo si kweli akimuandikia afisa wa kirumi (Theofilo) ambaye historia ya watawala wa kirumi wa Syria alikuwa anaijua vizuri.

Kwa hiyo sasa mimi, wewe na wengi wa wasomaji na wachangiaji wa hii mada humu JF sio wataalamu wa historia wala archeolojia. Ila wanasema kweli huwa na tabia ya kujifukua huko ilikojificha, sasa hivi hatujui - hilo halina maana kwamba Biblia inajichanganya ila ni kwamba historia imepotea. Lakini je imepotea kimoja? nadhani siyo, hao wataalam wanaendelea na utafiti wao, na jambo lililozuri sana kwa Biblia ni kwamba ina maadui wengi ambao wangependa kuthibitisha imepotoka. Hata hao tunawasubiri, mpaka sasa ngoma ni droo; huwezi kuthibitisha kwamba Kirenio alikuwa Liwali mara mbili lakini pia huwezi kuthibitisha kuwa hakuwa.
 
Shukrani kwa huu mchango wako uliopangiliwa wa hoja na maandiko.

Mungu akubariki sana
 
Mkuu

Naamini MUNGU yupo

Lakini kuna wajanja wachache Sana wakiamua kutuonyesha kwamba wao Ndio wanamjua vizuri KULIKO sisi wakaandaa Namna ya kutawala kupitia ujuzi wao wa elimu Hiyo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…