Biblia ina makosa? Nachanganyikiwa!

Uzzuri ni kwamba biblia imeandikwa kwa lugha nyingi kwa lengo la kuwafikia watu wengi.
Na wewe imekufikia....ENJOY!!

Tatizo dogo, unaisma kama unasoma gazeti la Mzalendo,,hakika utachanganyikiwa tena utakuwa kichaa kabisa.
Ushauri:
Tafuta mkristo yeyote utakayevutiwa naye kiimani akushike mkono ili msafiri salama kwenye hayo maandiko.
 
Punguza munkar sheikh 😅

Biblia inasema hakuna aliyemwona Mungu akaishi.
Hivyo kama unataka kumwona ujue ukishamtia machoni anaondoka na wewe😎
 
Waamini ndio huwa mnasoma Biblia kama kitabu cha simulizi(novels) au gazeti kwa mtiririko bila kufanya ulinganisho/comparison/uchambuzi. Ukivisoma vitabu vya injili kwa kulinganisha kila tukio katika injili zote nne mkanganyiko (contradictions) imejaa tele.
 
Ukiisoma biblia, huku roho yako ukiwa umeifanya nyumba ya shetani, kamwe huwezi kuelewa chochote, kwa sababu shetani anayefanya kazi ndani yako, ni kutaka uwe wake milele. Kila utakachokisoma, shetani atataka kisaidie kukupoteza zaidi, ndiyo maana anakunyima ufahamu.

Hata makuhani wa nyakati za kale, shetani aluwaingia kiasi cha kuanya maagizo ya Mungu kupitia manabii wake wayatafsiri vibaya ili kutimiza matakwa ya shetani. Na kwa sababu makuhani na mafarisayo walitumika na shetani, ndiyo sababu Mungu akaamua kuwafikia wanadamu kwa kuitengeneza nafsi katika umbile la mwanadamu ili wanadamu wapate mafundisho ya kweli moja kwa moja kutoka kwake. Na ndiyo maana Yesu Kristo alisema, Hakuna amjuaye Baba isupokuwa Mwana, Hakuna atakayemfikia Baba isipokuwa kupitia mimi. Na muda wote aliokaa na wanadamu alifuta mafundisho na tafsiri zote potofu za makuhani na mafarisayo. Ndiyo maana Paulo aliyekywa mshika mafundisho ya makuhani na mafarisayo, mafundisho yaliyopotoshwa, anasema kuwa AGANO JIPYA, NI UTIMILIFU WA AGANO LA KALE. Tena akaongeza kuwa AGANO LA KALE NI KIVULI CHA AGANO JIPYA.

Omba sana rehema ya Mungu, maana humjui Mungu aliye Mmoja katika nafsi zake tatu, kwa utashi na werevu wako, bali kwa msaada wa Mungu mwenyewe, na hiyo ni kwa sababu shetani anafanya kazi usiku na mchana kukupotosha ili uwe wake milele.
 
Kweli nimeamini mti wenye matunda ndio unaotupiwa mawe.

Yohana 15:18 — Yesu anawaambia wanafunzi wake kwamba ulimwengu ukiwachukia, ujue ulimchukia yeye kwanza.
2 Timotheo 3:12 — Biblia inasema kwamba wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.
 
Biblia ni kitabu cha utamaduni wa watu wa ulaya unatumiaga ugoro au bangi???????????
biblia na ulaya wapi na wapi????????????????????????
kilicholetwa kuutoa utamaduni wa kiafrika na kuuingiza wa kizungu uzungu gani upo kwenye biblia????????
hujui weazungu wenyewe walipelekewa biblia???????????????????
 
sio mbaya niko mbioni kuanzisha dini yangu
 
nikupongeze mtoa mada kwa kuamua kusoma biblia na kufika siku ya 33 hongera sana . Pia kuwa na maswali juu ya unachokisoma ni jambo la kawaida sana tena ni la kibinadamu kabisa kwa yeyote mwenye akili. nikushauri kila unaposoma biblia andika unachoelewa na pia andika maswali unayokutana nayo. Yaandike na usiyatafutie majibu kutoka kwenye ufahamu wako wewe endelea kusoma biblia na ukiomba mwambie Mungu vile unajisikia au vile biblia inavyokuchanganya, mwambie exactly kama uliotuandikia hapa na ongea nae kuwa akufunulie majibu ya maswali maana unasoma biblia ili kukutana na sauti ya Mungu mwambie basi ninavyosoma nikutane na sauti yako kwenye haya yaliyonichanganya.

Maadam umeamua mwenyewe kusoma biblia(naamini ni roho yako na nafsi yako vimetii mwaliko wa roho mtakatifu) usiulize kila mtu swali unalokiutana nalo. utapewa majibu milioni utashika lipi sasa. hili nalo unaweza kumwambia Mungu nahitaji mtu au mahali nitakaposaidiwa namna ya kukujua na kuyajua maneno yako katika biblia.. Cha msingi endelea kusoma biblia na wakati mwingine sikiliza mahubiri ama bible studies. endelea kusoma biblia na usiache kuandika maswali. majibu ya maswali yako yatajifunua unavyoendelea kusoma biblia na unavyoendelea kusikiliza mahubiri na wakati mwingine unaweza kumuuliza mchungaji wako pia ila endelea kusoma biblia. na hata ukiimaliza anza tena upya kusoma maana ufunuo ulioupata leo kwenye mstari utakaousoma ni tifauti na ufunuo utakaoupata ukisoma mstari uleule kwa wakati mwingine. so endelea kusoma.
 
Unaelewa nini kuhusu papal states?
 
Unaelewa nini kuhusu papal states?
biblia mostly imeandikwa middle east asilimia kubwa na visiwa vya patmo na paulo
papal state ya italy ni kipindi papa ananguvu na kumiliki maeneo aliyoyapoteza na kukupaliwa vatican iwe nchi na mussolin
 
biblia mostly imeandikwa middle east asilimia kubwa na visiwa vya patmo na paulo
papal state ya italy ni kipindi papa ananguvu na kumiliki maeneo aliyoyapoteza na kukupaliwa vatican iwe nchi na mussolin
Nani aliileta biblia afrika ya mashariki? Na kuwafundisha watu neno na kuitafsiri kwa lugha za asili na kwa dhumuni gani?
 
Kama mtu akijaribiwa, asiseme: “Ninajaribiwa na Mungu.” Maana Mungu hawezi kujaribiwa na uovu, wala yeye hamjaribu mtu yeyote .YAKOBO 1:13
 
Punguza munkar sheikh 😅

Biblia inasema hakuna aliyemwona Mungu akaishi.
Hivyo kama unataka kumwona ujue ukishamtia machoni anaondoka na wewe😎
Kama hakuna aliyemuona, mlijuaje yupo?

Au mmejitungia tu dhana ya kufikirika mkaamua kuiita Mungu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…