Sikumbuki ni Injili gani kati ya vitabu ambavyo havikuweka kwenye Biblia aliulizwa Yesu na watu wasioamini kuwa Mungu yupo.
Imeeandikwa humo kuwa Yesu alijibu swali hilo kwa mfano huu.
Kuwa katika mto fulani kulikuwa na samaki wasioamini kuwa kuna maji, wakamwendea samaki mmoja mzee wakamwuliza kama kuna maji, Yule samaki akawaambia kwa suala hili nendeni baharini mtamkuta samaki mmoja mwenye hekima huyo atawaeleza na kuwapa majibu yenu.
wale samaki wakaenda kama walivyoagizwa, walipofika kule wakamweleza yule samaki kuhusu mashaka yao kuhusu kuwepo kwa maji.
Yule samaki mwenye busara akawaambia hamuamini kuhusu kuwepo kwa maji, wakati ndani yake mnazaliwa, mnaishi, mnakula mnakwenda na ndani yake mnakufa.
Kuwepo kwa aliyeumbwa maana yake Muumba yupo, kuwepo kwa meza na viti maana yake seremala yupo. Kuwepo kwangu mimi maana yake yupo aliyeniumba, ukitaka kumuona Mungu angalia kazi zake mojawapo ni mimi.
Hao unaowataja kwa sasa hawapo, lakini kazi zao ndizo unazozisoma.
Hata akilini inatambulika kwa kazi zake haonekani kwa macho, sina hakika ulishawahi kukutana na akili macho kwa macho.
Ukitaka kumuona Mungu angalia kazi zake, amekupa utashi wa kuchagua kuamini au kutokuamini. Kutokuamini kwako hakumfanyi apungue wala kuamini kwako hakumfanyi aongezeke.
Mungu anatawala na kukaa na watu kwa njia ya imani na kuwafanya watu kuwa wema kama yeye alivyomwema na nimaamuzi ya mtu mwenyewe kuamini au kutokuamini. Hapa msistizo uko kwenye mtu zaidi ya mwili na vya mwilini. Mungu naye ana watu anaowaita watu wake. Nao hao wako kwenye jitihada za kuwaongeza watu waaminio Mungu na nguvu zake.
Shetani anatawala watu kwa njia ya hofu na kwafanya watu waovu kama yeye alivyomuovu. Hapa msisitizo uko kwenye mambo ya mwilini na vionjo vyake. Ndilo linapokuja swali la ulishawahi kumuona Mungu kwa macho msisitizo ni kwenye mambo ya mwilini. Shetani nae anawatu wake ambao wamejitoa kwa kujua au kutokujua kufanyakazi zake mojawapo ni kuasi tu mambo ya Mungu, ikiwezekana msisitizo uwe hayupo tu.
Kwa hiyo ninakuona wewe unapost humu ni uthibitisho tosha kuwa Mungu yupo na shetani yupo pia.
Yeremia kuna sehemu aliambiwa nenda kwa mfinyanzi na kule nitaongea na wewe, alipofika kule alimkuta mfinyanzi akifanya kazi yake ya kufinyanga na aliamua analotaka udongo huu akatengeneza kikombe huu sahani kadri ya maamuzi yake. Mungu akamuuliza yeremia je Mimi nisiwe na uamuamuzi wa kufanya mambo kadri nitakavyo kama afanyavyo mfinyanzi huyu?
Kuishi katika mwili huo ilionao milele sio mpango wa Mungu hata kama unaupenda sana huo mwili wako, siku ikifika utachomoka tu. Ni hekima yake Mwenyezi ambayo hata unayoyaona mapumbavu ni zaidi sana ya hekima ya mwanadamu. Na hao unaosema wapenzi wako katika mwili huu wataondoka na wewe utailia vilevile, shida hasa kwako kulia kwako ni kubaya kwa sababu huna tumaini baada ya kufa, tofauti na wenye tumaini baada ya kufa.
Bwana uinuke utende sawasawa na mapenzi yako, kwani ni nani atakuuliza unafanya nini hapo? Sikumbuki huu mstari unapatika wapi? Naona ni vyema kufunga na mstari huo kwa sasa