Biblia kwa Jicho Jingine

Biblia kwa Jicho Jingine

Huyu jamaa hawezi kuiendeleza hii maada coz ameicopy toka sehemu na alipoishia ndio hata kule ilipoishia nishaona sehemu kipindi nasoma sana so naona wengi mnaomba mwendelezo ambao yeye hawezi kuendeleza coz alicopy the whole story so hapo ndio mwisho wa kucopy coz story haikuendelea zaidi cha msingi na nyinyi endeleeni kutafuta other sources may be tutapata story nyingine..ni hayo tu wakuu msichoke kutafuta maarifa na kweli tuliyoagizwa kuitafuta,kuna vitabu vingi sana vya kusoma kufill gap iliyoachwa hapo kati..
Unampiga na kitu kizito muhaya wa watu aiseee.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ni ndefu ila haichoshi kusoma Safi sana nimesoma yote nimepata muunganiko mkubwa sana kwenye maandiko ya BIBLIA ambayo mengine nilikuwa nashindwa kuelewa. Nasubiri uchambuzi mwingine.
 
...haya maelezo yameegemea zaidi zile ngano za kwenye biblia ,sidhani kama Quran na vitabu vya iman zingine vina story hizi mkuu
...my point is_una uhakika gani kama hizi story za biblia ndio sahihi kumuelezea Mungu wa kweli na kuona story za tamaduni zingine kama ni za Miungu,Mizimu,Mapepo etc

......sidhani kama wasio wakristo wataelewa hizi mambo unazoeleza hapa mkuu....nafikiri hizi zilifaa zaidi kuelezea kanisani coz uhakika wake pia ni questionable kwa watu wasio amini biblia ambao ni wengi tu
Ila ndio maana Mwandishi kasema amerejea vitabu vingi ila kitabu Kikuu ni Biblia. Kwahiyo hapa anajenga dhana hasa kwa upande wa wanaoamini Biblia. Ila kwa imani zingine ni Vizuri pia kujifunza.
 
Duh sitaki kuamininkuwa huu Uzi ni wa zamani na sijawahi kuuona[emoji848][emoji119][emoji87]
Makubwa haya!

Sijamaliza kusoma,bado kidogo,ila nimependa ulivyoelezea na kufafanua ,'I wish' ungekuwa unaweka na mistari ya kusapot maana ipo kabisa,kila nikisoma naona kabisa ilipoandikwa!
Kudos[emoji106]
Km sehemu yaa uumbaji na kitabu cha mwanzo ...sehemu ya kiti cha enzi naona kabisa isaya,Daniel...
 
Mkuu Mashahidi wa Yehova wamechakachua mambo mengi sana.

Kwanza wanaamini Roho Mtakatifu si nafsi hai, bali ni nguvu ya Uungu inayotenda kazi ambayo kimsingi ni nguvu mfu.
Kama ambavyo gravitational force ni nguvu inayotenda kazi japo ni mfu, gravitational force hapa duniani huvuta vitu vyote kuelekea kwenye centre ya dunia, japo haina utashi wa kuamua wala hisia wala chochote ni just nguvu tu.
Hivyo hivyo kwa Roho Mtakatifu kwao ni nguvu tu ya kiroho, na wao wanamuita Roho huyu kuwa ni Roho Takatifu.

Pili hawaamini katika Mbingu mpya na dunia mpya baada ya Kiama, wanaamini katika Mungu kufagia tu uovu duniani na kubakiza wema, kwa msingi huo wanaamini hata majumba yaliyojengwa na wanadamu kama yale ya Posta pale Dar es Salaam yatabakizwa mara baada ya kiama kwa kuwa Mungu "si mjinga kihiivyo" kuivuruga dunia, na ndio maana makanisa yao yanaitwa JUMBA LA UFALME wakiamini kuwa yatadumu milele na milele.

Yapo mambo mengi sana nyuma ya pazia kwa kuwa Shetani amebuni mbinu mpya ya kuwadanganya wanadamu ambayo ni kuuchanganya uongo na ukweli, anachukua nusu uongo anamiksi na nusu ukweli, hapo ndipo upotofu mzito sana unatokea.

Lakini Ukisoma Biblia kwa mapana yake utaona kuna mapungufu mengi sana.
Fact!
 
Unachokisema ni kweli kabisa mkuu.

Hata Malaika wanayeishi na Mungu huko juu hawamuelewi huyu Mungu ni nani.
Katika kozi ambazo haziishi mbinguni ni kozi inayoitwa "Kumuelewa Mungu".

Hii ni kozi inayosomwa milele na milele na milele yote na kila kiumbe alichokiumba Mungu, si Malaika wala si wanadamu wala si kiumbe chochote cha kiroo kinaweza ku-graduate katika kozi hii.

Huko mbele nitaelezea concept moja makini sana ambayo kwa kifupi ni kuwa Mungu hujifunua kwa kila kiumbe chake kwa Level ya kiroho waliyo nao hao viumbe wake kwa kuwa yeye ni mkuu mno huwezi kumuelewa akija kama alivyo.

Na ni kweli kuwa Mungu ana mfumo wa utawala kama ulioko huku duniani, lakini yuko accessible kwa kila kiumbe chake, hakuna protocol ngumu ya kumuona kama ilivyo huku duniani, ila angalizo ni moja tu kuwa Mungu huyo unayemuona wewe si Mungu yule anayemuona Serafi au Kerubi, ndio maana wenye uhai wanne wale husihi tu kuimba mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu milele yote.

Si kwa sababu wanapenda kumsifu sana ila ni kwa sababu Kila siku wanamuona katika version mpya ambayo walikuwa hawajawahi kuiona, na katika hili kazi yao kuu ni kuitaja sifa kuu waiyoiona kwa wakati huo.
Na kwa kuwa daima anapanda katika viwango kwao kulingana na ufahamu wao, wao huishia tu kusema Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu maana hata wao wanashindwa kumuelewa.

Kwa hiyo ukienda Mbinguni leo ukataka kuonana na Mungu utapelekwa moja kwa moja na utakaa karibu naye kabisa, ila perception yako kwake italingana na uwezo wako wa ku conceive mambo ya Kiroho kwani wakati unadhani unamfahamu kumbe hata bado hujaanza kumfahamu.
Hata sioni cha kuongeza!uko sawa dude!

Na ndo maana hata level za watumishi wa Mungu (kwa maana ya nguvu za Mungu walizonazo ) zimetofautiana!
 
Mkuu nilichokielewa pia nikumegee kidogo .Mimi kama Mimi nimegundua pia uelewa Wa kila binadamu mmoja pia ndio uelewa wake wakumjua Mungu. na hiyo ni sana Kwa sbb Mungu anajifunua Kwa yeyote na Kwa njia mbali mbali. Mungu hana umbo halisi wala tabia iliyo moja .na kila mmoja anampa ufahamu kadri atakavyo yeye.
Ndio kwa sbb Mungu ni Roho!
 
SEHEMU YA PILI

Kwa miaka trilioni na trilioni mambo yalikwenda vizuri kabisa katika ulimwengu wa roho na spheres zake.
Kila kitu kiliishi kwa kufuata mifumo na mipaka aliyoiweka Mungu kuruhusu baadhi ya viumbe vilivyokuwa na juhudi ya kukua kiroho kuendelea kukua na kuimarika.

Kwa muktadha huo Uliwengu wa roho ulikuwa ni kama mmoja usio na matabaka matabaka zaidi ya ile miundo aliyoiumba Mungu kwa design yake.

Kwa ujumla wake ulimwengu wa kroho na kimwili uligawanyika katika maeneo makuu matatu.

Eneo la kwanza lilijulikana kama Pristine Universe, eneo la pili lilijulikana kama Boundary Universe na eneo la tatu lilijulikana kama Raw Universe.

Pristine Universe lilikuwa hasa ni eneo ambalo uumbaji ulikuwa umeshafanyika na kugawanyika kwa kadiri Mungu alivyoona inafaa kwa kufuata dimensions mbalimbali za kiuumbaji.

Boundary Universe hili lilikuwa ni eneo "tupu" au vacuum ambalo halikuwa na roho wa mwili wowote unaoishi huko, ni eneo ambalo lilikuwa kama uwanja usiojengwa au shamba lisilolimwa linalotegemea soon kulimwa pindi mwenye shamba atakapoamua kupanua mashamba yake.
Katika Boundary Universe hakuna kiumbe chochote kingeweza kuishi iwe ni maaika au viumbe vingine vya kiwmili au kiroho isipokuwa Mungu pekee na baadhi ya malaika waliopewa kulitunza eneo hilo na kuliandaa kwa ajili ya uumbaji utakao tokea, kila aliyejaribu kuingia eneo hili alipoteza uhai mora moja.

Raw Univese hili lilikuwa ni eneo a uumbaji ambapo Mungu alikuwa analitumia kama karakana au kiwanda cha ya uumbaji, eneo hili lilitawaliwa na giza na kila kilichoumbwa na kikasubiri kuzinduliwa rasmi kwa nyakati zilizoamuliwa na Mungu mwenyewe kiliwekwa huko.
Ni Mungu pekee na wasaidizi wake maalumu wa sekta ya uumbaji waliokuwa na access na eneo hilo.

Sasa basi Mungu alipoanza kuumba aliumba viumbe mbali mbali na vingi sana vya rohoni kwa mapana yake wa kwanza kwanza wakiwa wazee ishirini na nne na baadaye wakafuatia malaika wa ibada(worshiping angels), kwa kuwa jukumu la kila kiumbe lilikuwa kumuabudu Mungu.

Baadaye wakafuata malaika wengine na viumbe vingine vingi.
Ikumbukwe kuwa si kila kiumbe cha kiroho alichoumba Mungu kina Muundo kama wa binadamu, vingine vina muundo wa ajabu ajabu kama fimbo, ukienda huko mbinguni unaweza kukutana na fimbo ina macho au kiumbe kina sura ya ng'ombe na kinatimiza majukumu yake kama kawaida.

Katika malaika hao akaumba malaika wasimamizi wa galaxy mbali mbali akiwemo malaika maarufu sana kwa jina la Uryaluzzael ambaye ndiye alikuwa muangalizi wa dunia kabla Mungu hajaweka viumbe hai kuishi humu ndani.

Pia akaumba malaika wa hekima ambao walikuwa wamejaa maarifa na uwezo wa ajabu sana wa akili na ufahamu mpana sana kutoka kwa Mungu moja kwa moja wakisimamia kweli za Mungu.
Mbinguni malaika wanaoheshimika sana ni malaika wa Hekima na malaika wa Upendo na malaika wa Sifa na Ibada na malaika wa Hukumu za Mungu kwa kuwa hao ndio wanaougusa moyo wa Mungu moja kwa moja.

Pia Mungu akaumba maserafi na makerubi na walioko chini yao.
Katika hilo kundi hilo la Makerubi akamuumba kiumbe mmoja mzuri sana akampamba kwa kila aina ya nakshi na kila nguvu ya kiroho lakini pia akmpa kitengo nyeti sana cha kuzikusanya sifa zote za Mungu kutoka Spheres zote za kiroho na kimwili na kuzipeleka kwa Mungu moja kwa moja.
Kiumbe huyu aliitwa Lucifer, liyekuwa kerubi mzuri mwenye kupendeza kweli kweli anayejua kumsifu Mungu mpaka akafurahi, lakini pia anayejua kuzichambua sifa zinazoletwa kwa Mungu kutoka kila angle ya uumbaji ili zimfikie Mungu kwa mpangilio mzuri kabisa.
Chini yake akampa malaika wengi sana wa kumsaidia kazi yake hiyo.

Katika Kundi hili la makerubi pia akamuumba malaika muhimu sana anayeitwa Melkizedeki ambaye naye alikuwa rafiki mkuu sana wa Adam, akimsaidia katika ukuaji wake wa kiroho lakini pia katika kuitawala na kuisimamia dunia kama Mungu alivyotaka.
Melkizedeki huyu ndiye aliyepewa jukumu la kuilinda njia ya kwenda Bistani ya Edeni Adam alipoanguka.

Na kwa kuwa alikuwa kama guardina angel wa Adam, hata mara baada ya anguko la Adm ndiye aliyeishi naye duniani akiendelea kumsaidia mambo mbali mbali, na mara baada ya Adam Kufa akaruhusiwa kuuvaa mwili wa kawaida akawa kama mwanadamu akiishi na wanadamu kwa ruhusa ya Mungu mpaka pale Ibrahimu alipokutana naye kama Biblia inavyosema kwenye kitabu cha mwanzo.


Lucifer alikuwa malaika mwenye ngazi ya kerubi, tofauti yake na wengine ni kuwa yeye alikuwa kwenye kitengo muhimu sana cha sifa kwa Mungu, kitengo kilichompa access ya kuingia kwa Mungu moja kwa moja bila kufata protocol yoyoye.

Watu wengi hudhani mbinguni kuna Mungu na malaika tu, lakini kuna viumbe wengi sana zaidi ya malaika na generally wanajulikana huku kwetu kama “viumbe vya kiroho” lakini jina lao hasa hatujafunuliwa.

Wapo malaika waliokuwa na nguvu kubwa sana zaidi ya Lucifer hata kabla ya uasi wake, kilichompa charti shetani ni majukumu aliyokuwa nayo maana alikuwa center ya sifa kwa Mungu, na hapo ndipo hasa kwenye “moyo” wa Uungu wa Mungu wetu.

Kutokana na majukumu aliyokabidhiwa Lucifer ya kuzikusanya sifa zote na utukufu kutoka angle mbali mbali na kuzipeleka kwa Mungu na pia akapewa uwezo wa kusifu lakini alianza taratibu kuzitamani sifa zile akaziona ni zake na ana haki nazo yeye.

Tararibu moyo wake ukaanza kujiinua akaanza kujiona ni mkubwa kuliko malaika wote, miaka ilivyokwenda akajiona ni mkubwa kuliko makerubi wenzake wote, baadaye akajiona ni mkubwa kuliko malaika wote wa kitengo cha hekima baadaye kuliko wazee ishirini na nne.
Miaka ilivyozidi kwenda akajiona ni mkubwa kuliko maserafi wote.

Baadaye akajiona ni mkubwa kuliko Roho wa Mungu baadaye akajiona ni mkubwa kuliko Neno na akaanza kuutamani Uungu.
Mara baada ya tamaa ya Uuungu kumuingia mwanzoni akataka kuchukua nafasi ya Neno, akidhani ataweza kuwa muumbaji kama Neno.

Ni kama Mkurugenzi mkuu wa TRA akabidhiwe jukumu la kukusanya kodi zote za nchi na kuziwasilisha serikalini huku akiwa analipwa mshahara mzuri na ulinzi wa serikali na marupu rupu ya kutosha lakini taratiibu akaanza udokozi wa kodi za wananchi na kuziona kodi zote ni zake yeye kama Mkurugenzi, si za wananchi wala si za serikali, na kwa msingi huo aanze kuandaa plot ya kutaka kuchukua kiti cha Ikulu awe Rais yeye huku akisahau kuwa yeye ni mteuliwa tu wa Rais na sifa na marupurupu aliyonayo ni kwa sababu ya nafasi aliyo nayo kama mkurugenzi na yamepangwa na Rais wake.


Akaanzisha uasi akapata baadhi ya malaika na kuwatoa katika Pristine Universe kwenda kuvuka kwenye Boundary Unverse ili ajitegemee na aanishe mbingu yake na utawala wake.
Kikosi kile cha jwanza kabisa cha malaika kilipovuka tu mipaka ya Boundary Universe kikateketea chote kwa kuwa huko hakuna aliyeweza kuishi zaidi ya Mungu pekee maana ndiye chanzo cha uhai wote na yeye ndiye uhai wenyewe.

Mara baada ya Lucifer kuona imeshindikana kuvuka akajipanga upya kutaka kuja na mpangowa wa pili, yaani Plan B.

Plani B ilikuwa kumpindua Mungu hapo hapo alipo kwa kiburi kuwa naye anafaa kuwa kama Mungu.
Akaja na therty moja kuwa Mungu si chanzo cha nguvu zote kama wengi wanavyodhani ila amewazidi ujanja wenzio kwa kukaa mahali ambapo uhai wote unatokea yaani kiti cha enzi na kwa msingi huo yoyote yule ambaye ataweza kumtoa hapo atakuwa na uwezo kama wake.

Lakini pia akaja na wazo kuwa Mungu si kwamba ni muumbaji wa kila kitu kwa amri yake, ila ni kwa kuwa ni mambo yote yanatokea kwa sababu ya "evolution process" ambayo ni natural na Mungu ameihodhi na kujifanya kuwa yeye ndiye chanzo cha yote.

Hivyo kama malaika wakimuunga mkono akaweza kumpindua Mungu pale alipo na kuchukua nafasi yake, basi anao uwezo wa kuunda mfumo mpya kabisa wa maisha ambao hautakuwa unamtukuza "mtu" mmoja tu ambaye ni Mungu ila kila mtu atakuwa na portion ya utukufu wake, jambo ambalo lilikubalika sana kwa wenye uchu wa ukuu huko mbinguni.

Tangu kuanza kwa tamaa ya Lucifer mpaka uasi wake ilichukua miaka milioni moja ya kimbingu sawa na miaka Bilioni moja ya kidunia.

Hatimaye siku ya siku ikafika ya kufanya mapinduzi haswa haswa.
Hapo ndipo kikosi maalumu kambacho hakikutarajiwa kabla kikaundwa na malaika Mikaeli ambaye mwanzoni hakuwa malaika wa vita, mwanzo alikuwa malaika anayesimamia kuwakuza viumbe vya kiroho katika spheres zote kukua katika tabia za Kimungu kama Upendo, haki, huruma na tabia nyingine za "Utu mwema" maana kila kiumbe kina dimension yake ya tabia hizi na hukua hatua kwa hatua mpaka kufika kabisa kiwango ambacho Mungu anakiona kinafaa kwa kiumbe hicho kuingia katika sphere nyingine kwa ajili ya maisha ya dimension nyingine.

Katika kuuzima uasi hule ili kuhakikisha kuwa maeneo nyeti ya ibada za kimbingu hayatiwi unajisi na Lucifer na kundi lake maaika Phanuel ambaye jukuma lake la kwanza kabla ya uasi ule lilikuwa kuutunza na kusimamia Uwepo wa Mungu na Utakatifu wake hasa maeneo ya Ibada akashirikiana na Gabriel kuhakikisha kuwa maeneo nyeti ya ibada hayanajisiwi huku Mikael akipambana moja kwa moja na Lucifer.

Vita ikapangwa Mbinguni Lucifer na malaika zake na Mikaeli na malaika zake, vita ile ilihusisha mapigano ya moja kwa moja, mapigano ya ushawishi kuhakikisha viumbe vinavutiwa kila kimoja upande mmoja lakini pia vita ya panga pangua ya Ulimwengu wa roho maana Lucifer alifanikiwa kumega theluthi moja ya ulimwengu wa roho wa Pristine Universe na kuziweka upande wake, huku Mungu akibaki na theluthi 2 ya ulimwengu huo kwa wakati huo.

Mwisho wa siku Mikaeli aliibuka mshindi akafanikiwa pia kufanya tukio la ajabu sana lililoushangaza ulimwengu wa kiroho, tukio la kukata ulimwengu wa roho wa Lucifer na kuutenga pembeni kabisa na kutengeneza mkusanyiko uliojulikana kama War Universe.
Bahati mbaya sana dunia yetu na Sola Sstem yetu na Galaxy hii ikaangukia katika hio War Galaxy.

Na sababu kuu ni kuwa kulikuwa na race ya viumbe kabla ya Adam kuumbwa vilivyoishi hakika ulimwengu huu ambavyo vilikubali kushirikiana na Lucifer na kumuasi Mungu, hivyo vikajikabidhi kwa Lucifer japo si kwa kiwango kikubwa kama kile cha malaika na sehemu Nyingine.

Vita ikaisha Mungu akapanga na kupangua safu yake upya na kuweka mfumo mpya wa majukumu kwa kila kiumbe kilichobaki ikiwemo kuwapandisha baadhi ya malaika ngazi na kuwapangia majukumu mengine, na hapo ndipo malaika Mikaeli akapewa jukumu la kuwa mkuu na mwangalizi wa hii War Universe na akajulikana kama malaika mkuu.


Katika ulimwengu war oho kuna viumbe vya roho vikubwa sana na pia vyenye nguvu sana na vitiifu kwa Mungu kweli kweli ambavyo vimepewa usimamizi wa galaxies zote vingine vikiwa ni malaika na vingine vikiwa si malaika ila vinajulikana tu kama viumbe vya rohoni.

Lucifer alipoasi aliweka makao makuu yake nje ya Solar System yetu hii katika War Sphere japo Solar System yetu nayo ilikuwemo katika War Sphere hiyo ila haikuwa makao makuu ya Lucifer.

Tayari dunia na Solar System yetu hii ilikuwa inakaliwa na uzao mwingine ambao haukuwa uzao wetu huu wa Adam, katika uasi ule wao waliamua kujiunga na Lucifer lakini si kwa kiwango cha Ushetani ule maana viumbe waliokuwa wanakaa katika dunia hii hawakuwa wa kiroho ila wa kimwili.

Mungu akaamua kuwafutilia mbali na kuwanyang’anya mwili na kuwabakiza kuwa wa kiroho tu huku akiwaacha baadhi kukaa katika dunia hii hii ila katika dimension ya kiroho, lakini mpaka leo wanapambana kutafuta miili kwa kuwapagaa wanadamu kwa kuwa kwa maoni yao Mungu aliwadhulumu dunia yao na kuwanyang’anya miili yao, wengi wa wanadamu huwaita viumbe hawa kama mapepo, lakini ni roho zenye ubinadamu ndani yake zinazosihi katika ulimwengu wa roho.

Ikumbukwe kuwa si kila Shetani ni mapepo, kwenye ushetani kuna Majoka(hawa wengi wao huwa wakuu wa giza na mamlaka za giza), kuna mizimu(haya huwa ni mashetani yanayosimamia koo fulani na huku Afrika ni maarufu sana) kuna Miungu(hawa huwa ni wafalme wa giza) na kuna majini ambayo huwa ni mashetani yaneyoendana na mila za kiarabu.

Chini hapo kuna majeshi ya wafu, kuna viumbe vya rohoni vya giza ambavyo ni hybrid ya wanadamu na mashetani ambavyo huumbwa hasa kwa matendo ya zinaa za kishetani kama zinaa za majini mahaba, kuna vikaragosi, vinyamkera, vinwengo na madudu kibao.

Pia kuna mapepo

Roho zote hizi zinafanya kazi katika kambi ya Lucifer kwa sasa.

Mungu wetu ni Mungu wa mipango ambaye huwa ratiba yake na mapenzi yake hayavurugwi na yeyote, kwa hiyo baada ya vita ile akaamua kuendelea na zoezi lake la uumbaji kama hapo awali, zoezi ambalo linaendelea na litaendelea milele na milele kwa kuwa hana mwisho.

Hivyo Mungu akawatuma badhi ya Malaika zake wenye nguvu kuja kuangalia maeneo ambayo hayakuthiriwa sana na ushetani ili aendelee na uumbaji wake au kuyarekebisha marekebisho ya hapa na pale kuyarudhisha katika kusudi lake la awali.

Mmoja wa malaika wenye nguvu ambao Mungu aliwatuma hapa dunia kwa ajili ya kuisafisha dunia na solar Sstem hii kwa ajili ya Mungu kuendelea na mipango yake kama Muumbaji alikuwa anaitwa malaika Uryaluzzael.

Uryaluzzael huyu alikuwa mmoja wa malaika wenye nguvu sana wa kuweza kusimamia “Solar System” yote peke yake.
Kitendo cha Mungu kumtuma aje hapa duniani kilimshtua sana Lucifer na kumpa picha kuwa Dunia hii ni sehemu muhimu sana kwa Mungu na huenda anataka kufanya jambo zito sana, kwa hiyo akapambana na yeye akaja hapa hapa duniani kuanzisha empire yake.

Kitendo kile cha Lucifer kuhamishia makao hapa duniani kilifanya kuongezeka kwa giza katika Solar System na hivyo kumfanya Mungu kutoa hukumu ya haki ambapo dunia ilikuwa awali na miezi mitatu, miwili ikaharibiwa na kubakiza mmoja tu ambao tunao kwa sasa..

Malaika Uryaluzzael alikuja haa duniani kwa ajili ya kuianda dunia kwa ajili ya kuifinyanga upya ili kuumba uzao mpya kuikalia Galaxy yetu hii huku makao makuu yake yakiwa katika Solar System hii tuliyopo.
Yalikuwa ni maandalizi ya awali kabisa ya kuumbwa kwa Adam na uzao wake.

Maandaizi ya kuleta uzao mpya na kuufungua ukurasa mpya wa maisha mapya ambao sisi kwetu tunauita mwanzo.
Na hapo ndipo Mungu alipoichukua dunia na mbingu zake na kuirudisha katika Creation Sphere au Raw Sphere ambayo kimsingi huwa imefunikwa na giza na maji huku Roho wa Mungu akiendelea na hatua za kwanza kabisa za uwezeshaji wa uumbaji ili pale Neno tu atakapofika kuanza kazi yake, uumbaji uanze mara moja.

Na ndipo maandiko yanapoanza kwa kusema hapo Mwanzo Mungu aliziumba Mbingu na nchi, nayo nchi likuwa giza tena utupu, na Roho wa Mungu akatulia juu ya uso wa maji.

Kabla ya kuanza kusimulia mchakato wa uumbaji nitaanza kuuchambua ulimwengu wa roho wa Mbingu za Mungu na malaika zake halafu nitaenda kuichambua kuzimu ya Shetani na malaika zake na mifumo yao ya maisha jinsi walivyo.

Itaendelea.....
Sehemu ya kwanza tuko sawa!
Ila hii sehemu ya pili natofautiana na wewe hapa uliposema Melkzedeki alikuwa malaika!
Melkizedeki sio malaika,soma vzr kitabu cha Mwanzo kisha nenda Waebrania utajua alikuwa nani!
 
Huyu jamaa hawezi kuiendeleza hii maada coz ameicopy toka sehemu na alipoishia ndio hata kule ilipoishia nishaona sehemu kipindi nasoma sana so naona wengi mnaomba mwendelezo ambao yeye hawezi kuendeleza coz alicopy the whole story so hapo ndio mwisho wa kucopy coz story haikuendelea zaidi cha msingi na nyinyi endeleeni kutafuta other sources may be tutapata story nyingine..ni hayo tu wakuu msichoke kutafuta maarifa na kweli tuliyoagizwa kuitafuta,kuna vitabu vingi sana vya kusoma kufill gap iliyoachwa hapo kati..
[emoji87][emoji848][emoji16]duh kumbe?!!
Sasa si angesema tu kuwa kuna mahali kaicopy kwani kuna tatizo?

Ndo maana tangu 2018 mpk leo hakuna muendelezo[emoji23][emoji119]
Wabongo jamani!
Anyway,kwa sie wanaosoma biblia nankufuatilianmambo ya rohoni hawapati shida kuelewa!
 
[emoji87][emoji848][emoji16]duh kumbe?!!
Sasa si angesema tu kuwa kuna mahali kaicopy kwani kuna tatizo?

Ndo maana tangu 2018 mpk leo hakuna muendelezo[emoji23][emoji119]
Wabongo jamani!
Anyway,kwa sie wanaosoma biblia nankufuatilianmambo ya rohoni hawapati shida kuelewa!
@Christine1 nashukuru umesoma yote, achana na comment negative, kama kuna sehemu ipo hoi mada basi ashukuriwe aliye ileta hapa, hata kama haijatoa funzo lakini imeleta kitu fulani katika vingi vimhusuvyo Mungu .
 
Kumbe tabia ya kukimbia uzi ni toka kitambo sana.

Ila mkuu umeelezea vema sana.
 
[emoji87][emoji848][emoji16]duh kumbe?!!
Sasa si angesema tu kuwa kuna mahali kaicopy kwani kuna tatizo?

Ndo maana tangu 2018 mpk leo hakuna muendelezo[emoji23][emoji119]
Wabongo jamani!
Anyway,kwa sie wanaosoma biblia nankufuatilianmambo ya rohoni hawapati shida kuelewa!
Mi mwenyewe nilikuwa kama nyinyi baada ya kusoma huu uzi ulinishika sana so nikawa ni miongoni mwa waliokuwa wanasubiri mwendelezo..basi ikawa ni kila siku tunamtag kuulizia mwendelezo lakini jamaa alikuwa kimya, tukazama PM lakini jamaa kimya ndio mpaka leo, lakini mm sikukata tamaa nikaendelea kuchimba vitabu mbalimbali mpaka nilipokuja kukutana na hii story yake ndio nikagundua aliicopy kule na kuileta hapa ila ni uzi mzuri sana na una maarifa mengi mapya ya kujifunza, Big up kwake mleta uzi ameamsha watu wengi.
 
Mi mwenyewe nilikuwa kama nyinyi baada ya kusoma huu uzi ulinishika sana so nikawa ni miongoni mwa waliokuwa wanasubiri mwendelezo..basi ikawa ni kila siku tunamtag kuulizia mwendelezo lakini jamaa alikuwa kimya, tukazama PM lakini jamaa kimya ndio mpaka leo, lakini mm sikukata tamaa nikaendelea kuchimba vitabu mbalimbali mpaka nilipokuja kukutana na hii story yake ndio nikagundua aliicopy kule na kuileta hapa ila ni uzi mzuri sana na una maarifa mengi mapya ya kujifunza, Big up kwake mleta uzi ameamsha watu wengi.
Mkuu natamani kupata hiyo link alikoitoa hiyo habari ili na mm nikasome
 
Mi mwenyewe nilikuwa kama nyinyi baada ya kusoma huu uzi ulinishika sana so nikawa ni miongoni mwa waliokuwa wanasubiri mwendelezo..basi ikawa ni kila siku tunamtag kuulizia mwendelezo lakini jamaa alikuwa kimya, tukazama PM lakini jamaa kimya ndio mpaka leo, lakini mm sikukata tamaa nikaendelea kuchimba vitabu mbalimbali mpaka nilipokuja kukutana na hii story yake ndio nikagundua aliicopy kule na kuileta hapa ila ni uzi mzuri sana na una maarifa mengi mapya ya kujifunza, Big up kwake mleta uzi ameamsha watu wengi.
Tunaomba link na sisi tupitie pitie
 
Mi mwenyewe nilikuwa kama nyinyi baada ya kusoma huu uzi ulinishika sana so nikawa ni miongoni mwa waliokuwa wanasubiri mwendelezo..basi ikawa ni kila siku tunamtag kuulizia mwendelezo lakini jamaa alikuwa kimya, tukazama PM lakini jamaa kimya ndio mpaka leo, lakini mm sikukata tamaa nikaendelea kuchimba vitabu mbalimbali mpaka nilipokuja kukutana na hii story yake ndio nikagundua aliicopy kule na kuileta hapa ila ni uzi mzuri sana na una maarifa mengi mapya ya kujifunza, Big up kwake mleta uzi ameamsha watu wengi.

KWELI
 
Back
Top Bottom