hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 13,628
- 20,992
Hivi Ulishawahi kujiuliza kwanini NCHI YA LEBANONI LEO KATIKA BENDERA YAO WANATUMIA NEMBO YA MWEREZI?
Basi Ni Kitabu kimoja tu kitakupa sababu ,Sio kingine Ni BIBLIA ,Hata Kama utanuna hakuna namna , Ni kupitia BIBLIA utaelezwa hata Mzizi wa neno ISRAELI.
Qurani itataja neno ISRAELI Lakini kamwe haiwezi kukupa Mzizi /origin ya Hilo neno, Itataja Neno ZABURI Lakini kamwe hakuna atakayekuambia Zaburi Ni nini.
Basi Leo nakuletea Historia ya Mti wa Mwerezi ,ulitajwa Sana katika BIBLIA ,na Hadi leo Taifa la LEBANON ndio nembo yao katika BENDERA NA TAIFA, Lakini umeelezewa na kutajwa na BIBLIA miaka Zaidi ya 2800 iliyopita .
UTAIELEZA NINI BIBLIA?
Ni kutokana na ubora na ufahari na uzuri wa mti huu Nchi ya Lebanon inayoongozwa na Rais Mkristo, na waziri mkuu muislamu, wa madhehebu ya Suni na spika wa bunge muislamu wa madhehebu ya shia kwa mujibu wa sheria na mikataba yao, utaweza kuona bendera ya taifa hili na nembo ya rais wa nchi hii ina alama ya mti wa mwerezi.
Mwerezi ni nini?
Mwerezi ni aina ya mti uliokuwa unapatikana maeneno ya nchi ya Lebanoni, Ulikuwa unastawi pia sehemu mbalimbali za dunia, lakini ulistawi zaidi katika nchi ya Lebanoni, iliyopo kaskazini mwa nchi ya Israeli.
Aina hii ya mti ilitumika kwa matumizi mengi, kutokakana ubora wake na uimara wake ukulinganisha na aina nyingine ya miti. Mti huu wa Mwerezi ulikuwa ni mgumu na usiooza kirahisi.
Nchi ya Lebanoni, ilijipatia utajiri kutokana na biashara ya miti hii, ambapo Mataifa mengi duniani kama Misri, Ashuru, Babeli na Israeli ilinunua miti hii kutoka huko Lebanoni, kwaajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi.
Mfalme Daudi alitumia miti hii ya Mierezi kutoka Lebanoni kuijenga nyumba yake
6 BASI UAMURU WANIKATIE MIEREZI YA LEBANONI; na watumishi wangu watafuatana na watumishi wako; na ujira wa watumishi wako nitakupa kama utakavyosema; kwa kuwa wajua ya kwamba hakuna kwetu mtu ajuaye kukata miti kama Wasidoni”.
Na hata baada ya Mfalme Nebukadneza kuliharibu hekalu hilo la Sulemani, hekalu la pili lilipokuja kujengwa na wakina Zerubabeli, lilijengwa sehemu kwa miti hiyo ya Mierezi.
Ezra 3:6 “Tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba walianza kumtolea Bwana sadaka za kuteketezwa, lakini msingi wa hekalu la Bwana ulikuwa haujawekwa bado.
7 Tena waliwapa waashi na maseremala fedha; wakawapa watu wa Sidoni, na watu wa Tiro, chakula, na vinywaji, na mafuta, ili walete MIEREZI KUTOKA LEBANONI mpaka Yafa kwa njia ya bahari, kwa kadiri walivyopewa ruhusa na Koreshi, mfalme wa Uajemi”.
Hivyo Mwerezi katika biblia imetumika kama ishara ya UTAJIRI. Kama vile DHAHABU.
Tunaona vitu vikuu viwili vilivyotajwa sana katika ujenzi wa nyumba ya Mungu ni MWEREZI pamoja na DHAHABU. Kutokana na uthamani wa vitu hivyo.
Na kama Mti wa Mwerezi ulivyojipatia sifa hivyo, Bwana Mungu anasema walio Haki wote watasitawi kama Mwerezi.
Zaburi 92:12 “Mwenye haki atasitawi kama mtende, Atakua kama MWEREZI WA LEBANONI.
13 Waliopandwa katika nyumba ya Bwana Watasitawi katika nyua za Mungu wetu.
14 Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi.
15 Watangaze ya kuwa Bwana ni mwenye adili, Mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu”.