UrbanGentleman
JF-Expert Member
- Jun 19, 2016
- 2,584
- 1,885
Sio kweli....prove thatAsili ya biblia ni mashariki ya kati na kitovu ni Jerusalem au nchi ya Israel
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio kweli....prove thatAsili ya biblia ni mashariki ya kati na kitovu ni Jerusalem au nchi ya Israel
lowasa mbon kazaliwa juzi tu bhana weweYote haya yanasababishwa na fisadi Lowasa!
Wazungu wenyewe wanakataa habari za kuchanganya dini na serikali.Wazungu wameendelea na wana utamaduni ambao wote leo hii tunauiga au tunataka kuuiga lkn kama ulikuwa haufahamu Wazungu wameendelea kwa sababu ya UKRISTO, yaani mfumo wa Kizungu ni kwamba uliongozwa na mafundisho ya Biblia na ndiyo maana wamefikia hapo walipofikia, ukisikia wakisema Western Civilization maana yake ni kwamba ni Ukristo na Biblia!
Hata Ubepari au Capitalism kama ujulikanavyo kwa Kizungu umetokana na Biblia, bila ya Ukristo na Biblia hakuna Capitalism!
Sheria zote za Kizungu ambazo leo hii tunaziiga kama Common law ya Uingereza, French law, German law ambayo ndiyo inatumika Ujapani, Uchina na kwingineko imetokana Biblia na Ukristo, hivyo tukitaka kuendelea kwenye Dunia inayaofuata na kuongozwa na mfumo wa Kizungu ni lazima tuiishi Biblia au tuchanganye lkn ni lazima tuielewe Biblia na mafundisho yake na kuyaishi na siyo kuishia kukariri vifungu tu, bila ya hivyo tutabakia kuwa wa mwisho siku zote labda mpaka Kimondo kishuke Duniani na kuua sehemu kubwa ya Dunia na kutoa nafasi kwa Ustaarabu mwingine kunyanyuka lkn mpaka hiyo siku ifike Ukristo na Biblia ndiyo way to go!
" Mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi, mkikataa mtaangamia kwa upanga".... Bible
"Ukinisujudu ntakupa milki yote ya dunia"...shetani
"Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa"....Bible
Wazungu wenyewe wanakataa habari za kuchanganya dini na serikali.
Soma French Revolution, soma Enlightenment, soma Rousseau, soma Nietsche.
Angalia makanisa yanavyokosa watu Ulaya.
yeah ukristo umesaidia kuifikisha ulaya mahali ilipo leo hii ingawa nchi zingne kama japan na china zilikuwa na civilizations zao zilizowafikisha hapo walipo pia but kwa ulaya ukristo umechangia pakubwa sana
vipi kuhusu ushoga ambao ni ustaarabu wa ulayayeah ukristo umesaidia kuifikisha ulaya mahali ilipo leo hii ingawa nchi zingne kama japan na china zilikuwa na civilizations zao zilizowafikisha hapo walipo pia but kwa ulaya ukristo umechangia pakubwa sana
mkuu inawezekana haujaemuelewa vizuri mleta maada alichomaanishavipi kuhusu ushoga ambao ni ustaarabu wa ulaya
Unaongelea Ukristo kama vile Ukristo ni kitu kimoja kinachoeleweka wakati Ukristo ni vitu tofauti kwa watu tofauti.Kuukataa Ukristo leo hii au sijui kupinga Serikali kuwa na Dini haimaanishi au hakuondoi ukweli kwamba hii inayojulikana kama Western Civilization ni zao Ukristo wa Kizungu au unaweza hata kuuita Christian Civilization kwa kifupi bila Ukristo na Biblia hakuna Western civilization na bila Western civilization hakuna Ubepari au Capitalism kama wanavyouita ni sawa tu na kusema hakuna Arab/Persia Civilization bila Uislamu na Kurani!!
Unaongelea Ukristo kama vile Ukristo ni kitu kimoja kinachoeleweka wakati Ukristo ni vitu tofauti kwa watu tofauti.
Katika Ukristo humo humo kuna Ukatoliki na Uprotestanti.
Umesoma kitabu cha Max Weber "The Protestant Ethic and The Spirit of Capitalism".
Kwa mujibu wa Weber, Ukatoliki hauna spirit of Capitalism. Na Ukatoliki ni Ukristo bado. Utasemaje Ukristo ndio umeleta Capitalism wakati imekuwa argued successfully kwamba Ukatoliki hauna spirit of Capitalism?
Halafu kama vile unavyosema "kukataa Ukristo leo hii...hakuondoi ukweli kwamba hii inayojulikana kama Western Civilization ni zao la Ukristo wa kizungu" na mimi ninaweza kukwambia mchango wa Ukristo katika Western Civilization kwa sasa umepitwa na mchango wa European Enlightenment.
Unachosema wewe hapa ni kwamba "Bila Kinjeketile Ngwale kusingekuwa na Tanzania kwa sababu Kinjekitile ndiye alianza kuhamasisha watu wa iliyokuwa Tanzania waungane kupinga Wajerumani" wakati humtaji Nyerere na Karume na juhudi za TANU/ ASP zilizokuja kufanyika more immediately before Tanzania kuwapo.
Ukristo una sehemu muhimu katika Western Civilization. Kabla ya Ukristo kulikuwa na Greece na Rome. Baadaye yakaja mambo ya European Enlightenment. Kwa nini katika yote hayo umeona Ukristo tu wakati nafasi ya Ukristo kwa sasa ishapitwa na nafasi ya Enlightenment?
Kwa nini unaongelea Ukristo na wala si Roman Empire au Greece civilization zilizokuwa kabla?
Kwa nini unaongelea Ukristo na si Enlightenment iliyokuja baada ya Ukristo?
Unafahamu kwamba unaweza kutumia biblia kuhalalisha au kuharamisha chochote?
Enlightenment imetoka kwenye ukristo, imejikita kwenye secularism.Kwanza nimesisitiza kwa kusema ,,Ukristo wa Kizungu" nikifahamu kwamba Ukristo siyo Ukristo tu, na ninaposema Ukristo wa Kizungu namaanisha wote Ukatoliki na Uprotestanti kwani Uprotestanti ni zao la Ukatoliki, Max Weber nimemsoma sana na ndiyo chanzo cha ufahamu wangu juu ya nilichoandika!
Unachanganya mambo, Ukristo ndiyo chanzo cha kila kitu Ulaya hata hiyo enlightment unayoiongelea pia ni zao la Ukristo, hata Wanasayansi wanaoikataa Dini ya Ukristo leo hii Elimu yao yenyewe kuanzia akina Galileo mpaka hawa wa leo ni zao la Ukristo wa Ulaya hivyo huwezi kutenganisha western Civilization na Ukristo!
Enlightenment imetoka kwenye ukristo, imejikita kwenye secularism.
Ukristo Ulaya kwa sehemu kubwa ni historia, kitu kilicho influence Western Civilization Zaidi ya Ukristo ni Enlightenment.
Unaposema Enlightenment ni zao la Ukristo, ni kwamba hujui au unadharau tu ukweli kwamba Enlightenment pia ni zao la tamaduni za Rome na Greece zilizokuwepo kabla ya Ukristo?
Kwa nini unaona Enlightenment ni zao la Ukristo wakati watu kama kina Rosseau, Nietzsche, John Stuart Mill etc wamechangia Enlightenment kwa kukataa Ukristo?
the definition of enlightenment
The Enlightenment, a philosophical movement of the 18th century, characterized by belief in the power of human reason and by innovations in political, religious, and educational doctrine
Sasa mbona Ukristo nao umetoka kwenye Uyahudi ambao ulitoka kwenye tamaduni mbalimbali za kale?Kwa sababu hao wote akina Nitsche, Schiler &Co. pia ni zao la Ukristo, ninachomaanisha Elimu yao ya Falsafa imetokana au ina misingi ya Ukristo/Biblia kwa maana vyuo Vikuu walivyosoma vilikuwa vya Kikristo, sasa baada ya kuelimika ndiyo wakaanza kuiangalia Dunia kwa jicho lingine lkn misingi ya elimu yao ni Ukristo, kwa kuwa Vyuo vikuu vya Ulaya ambavyo ndivyo wamesoma vilijengwa na Kanisa na isitoshe zamani Ulaya kulikuwa hakuna utengenisho kati ya State na religion, na papa alikuwa ni Mkuu kama wa kisiasa pia ana aliongoza kwa kufuata Ukristo hivyo ilikuwa haiwezekani kukwepa influence ya ukristo!
Na yoyote aliyesoma alisoma kuhusu Ukristo na hivyo hata michango yao waliyoitoa ingawaje baadhi ilipingana na Ukristo lkn walikuwa wanazunguka hapo hapo tu, Nitsche ukisoma kazi zake nyingi amemuhusisha Mungu kama Human, All too human ingawaje alikuwa anakosoa uwepo wa Mungu lkn utaona chanzo cha uelewa wake ni huo huo ukristo, hivyo unaweza kusema bila Ukristo kusingekuwa na Nitsche ...
Asante kwa marekebisho bibie nilidhani ni GenghisNaunga mkono hoja. Ni Chengis Khan
Kwan ww hujioni km umeandika upumbavKwa nini unauita upumbavu? Fafanua kama ukipenda!