SimbaMpole123
JF-Expert Member
- Apr 23, 2023
- 5,501
- 4,956
Wanahistoria wa Misri na Israel kutokana na kuchimbua mabaki na kufuatilia michoro na vinginevyo wamekuta kwamba hamna uhalisia wowote kuhusu story za waisraeli kuwa watumwa Misri, kutembea jangwani miaka 40 na kupigana Vita dhidi ya miji 30 na zaidi. Ina maanisha kuwa hizi story hazina ukweli kwa sababu haziendani na tafiti za kihistoria. Pia kipindi hicho Canaan ilikuwa koloni la Misri kwa hiyo kulikuwa hamna maana ya kwenda Huko na Biblia inashindwa kumtaja jina huyo farao wakati hata Yale majaribu yaliyowakuta misri sio ya kweli kihistoria. Story zingine Kama Joshua kusimamisha jua na kushinda Vita kisa mvua ya mawe inaonekana kabisa hizi story ziliandikwa na watu wa kale wasio na uelewa wa sayansi. Mimi Kama Simba mpole sijui watu mnaaminije story Kama hizi na kuzichukulia Kama ukweli na historia.