Biblia: Wanawake na Wanyamaze katika kanisa

Biblia: Wanawake na Wanyamaze katika kanisa

goswe

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2018
Posts
4,432
Reaction score
5,036
Nawasalimu katika jina pendwa la Bwana wetu Yesu Kristo .
Mfalme wa utukufu.

Nimewaandikia hili kuwakumbusha hila za ibilisi,na njia yake kuu anayoitumia yakugeuza maandiko.

Nakufanya watu waishi kinyume cha neno la Mungu.

Yeye amefanya hivyo mara zote, kufanya watu waone hamna shida.

Lakini hakuna kitu Mungu amejali kama neno lake.

Mambo ni mengi yakuzungumza jinsi kanisa lilivyodanganyika na ibilisi,hata kuliacha neno ambalo wamedai kuliamini.

Lakini kama yesu alivyosema mpinga kristo atakuwa ni mkristo haswa anaepinga neno la Mungu hata akiona yeye hataamini,isiokiwa ataamini kile ameambiwa ama fundisho la kanisa lake.

Kulingana na neno la Mungu si ruhusa kwa mwanamke kuhubiri,kusimama mimbarani, wala kuzungumza kanisani.

Haijalishi zama ni zipi lakini huo ndio utaratibu wa Mungu.

Biblia inasema mwanamke na anyamaze kanisani akitii kwa kula jambo,maana ni aibu mwanamke kunena katika kanisa.

Na kama Mungu alinena hili mbingu na nchi zitapita ila hili litadumu milele mbele zake.

1 Timotheo 2:11-15
[11]Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.

[12]Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.

[13]Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.

[14]Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.

[15]Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.

1 Wakorintho 14:34-38
[34]Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.

[35]Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.

[36]Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?

[37]Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana.

[38]Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga.

Tena biblia inasema
Mwanamke hapaswi awe mchungaji.

Ila mchungaji awe mume wa mke mmoja na anaeweza kuisimamia nyumba yake vizuri

Neno la Mungu likisema usiue ,usiue,usizini,inamaanisha usizini.
Halihitaji tafsiri za mawazo yako
Lipo wazi na direct.

Katika mawazo yumo ibilisi,na katika maswali ndipo ibilisi anapoingilia.

Kanisa linajua haya yote na bado limekaa katika hali ya kidanganyika.

Bwana Yesu kristo alisema je nitakaporudi nitaikuta injili niliyowaachiaaa?
Kisha akasikitika sana

Biblia inasema si utaratibu wa kanisa la Mungu mwanamke kuhubiri wala kunena, ila akae kwa utulivu akitii kwa kila jambo,
Mungu kwakuwafahamu kwake tangu mwanzo wanawake aliwaweka nje ya huduma yake kuu,.

Adam hakudanganyika siku zote eden isipokuwa mwanamke ndani ya muda mfupi tu,alipoenda nje ya uangalizi wa mumewe dakika chache tuu alidanganyika.

Hakuna kiumbe kipo karibu na Mungu sana kama mwanamke kama akiwa ndani ya neno.
Ila hakuna kitu kipo karibu na ibilisi kama mwanamke.
Na njia kuu ya kumwangusha mwanaume ni kupitia mwanamke.

Bwana wetu Yesu kristo aliwaona wanawake wengi lakini hakuchagua mmoja kuambatana.

Mungu hapingani na neno lake.
Ni nini?

Ibilisi akiwa kanisani.
Usishiriki kitu kinyume na neno la Mungu.

Biblia inasema wapo watu wanaojisumbua kuniabudu.
Wananiabudu bure .

Huyu paulo ambae watuwatasema ni mawazo yake
Ndie yule alitokewa na Bwana yesu kristo,alipokuwa akienda kuua wakristo.

Akapelekwa jangwani miaka mitatu

Kisha akarudi ili azungumze na mitume

Aone kuwa aliyoambiwa ni sawa na wao.

Biblia inasema alipozungumza nao hakuona kimoja cha kuongezewa kutoka kwao.

Anasema haya ni maagizo ya Bwana ila mtu akitaka kuwa mjinga na awe mjinga ila sisi wala makanisa ya Mungu hatuna utaratibu huo.

Kisha anasema hata malaika kutoka mbinguni ama yeye mwenyewe aje ahubiri injili nyingine tofauti na hii alaaniwe

Wagalatia 1:6-10
[6]Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine.

[7]Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo.

[8]Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.

[9]Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.

[10]Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.

Mithali 14:12
[12]Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu,
Lakini mwisho wake ni njia za mauti.

Mathayo 7:13-15
[13]Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.

[14]Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

[15]Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
 
Tuanze na nabii mkuu Elen G. White; una maoni gani?
Tangu dunia kuanza
Mungu hajawahi kumtuma nabii mkuu mwanamke
Wlaikuwepo wenye karama za unabii ila si manabii wa kuleta ujumbe kwa kizazi
Miriam na wenzake wote,wlaikuwa na karama za kinabii anaweza akakuota ama akaona Ono kwako ilansi unabii.
 
Humjui vizuri; amepasishwa na mabingwa wengi duniani; wasomi wazamivu wa theology. She one of the most influential person of all times amekuwa rated hivyo. Msome kidogo hapo kisha utafakari tena!

Humjui vizuri; amepasishwa na mabingwa wengi duniani; wasomi wazamivu wa theology. She one of the most influential person of all times amekuwa rated hivyo. Msome kidogo hapo kisha utafakari tena!

Haijalishi amepasishwa na watu wenye elimu kiasi gani,wala amesoma kiasi gani maadamu yupo nje ya neno la Mungu huyo sie

Mafarisayo na masadukayo walikuwa wasomi sana,walipasishwa na shule mashuhuri hata wakati fulani walimkejeli yesu kuwa amesoma chuo gani.
Lakini ndio waliomkataa yesu

Biblia inasema akili za wanadam kwa Mungu ni upumbavu.

Paulo alifundishwa elimu ya dini akafikia kiwango kikubwa mnoo na walimtarajia awe kuhani,
Lakini alipoitwa Mungu alimtoa elimu yoote na vikira zoote alizokuwa nazo alafu akampa neno halisi.

Musa alifundishwa miaka 40 mapambano na elimu za kidini wakitarajia aje awe FARAO,
Mungu alipomuita alimpeleka porini miaka 40 akamfuta akili zoote za kibinadam na pambo alizo pewa ndipo akamtumia.

Hivyo basi hata kama upambwe na maua kiasi gani na watu wakupe vyeti na heshima.
Maadam haupo sawa na neno la Mungu wewe kwakuanzia tu sie
 
Amosi 3:7
[7]Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.
Surely the Lord GOD will do nothing, but he revealeth his secret unto his servants the prophets.

Sio mtu mwingine yoyote.sio mwanatheolojia
Neno huja kwa nabii.
Na nabii huletwa mmoja kwa kila kizazi.
Sio kama hawa kila mtu anaejiita nabii
 
Haijalishi amepasishwa na watu wenye elimu kiasi gani,wala amesoma kiasi gani maadamu yupo nje ya neno la Mungu huyo sie

Mafarisayo na masadukayo walikuwa wasomi sana,walipasishwa na shule mashuhuri hata wakati fulani walimkejeli yesu kuwa amesoma chuo gani.
Lakini ndio waliomkataa yesu

Biblia inasema akili za wanadam kwa Mungu ni upumbavu.

Paulo alifundishwa elimu ya dini akafikia kiwango kikubwa mnoo na walimtarajia awe kuhani,
Lakini alipoitwa Mungu alimtoa elimu yoote na vikira zoote alizokuwa nazo alafu akampa neno halisi.

Musa alifundishwa miaka 40 mapambano na elimu za kidini wakitarajia aje awe FARAO,
Mungu alipomuita alimpeleka porini miaka 40 akamfuta akili zoote za kibinadam na pambo alizo pewa ndipo akamtumia.

Hivyo basi hata kama upambwe na maua kiasi gani na watu wakupe vyeti na heshima.
Maadam haupo sawa na neno la Mungu wewe kwakuanzia tu sie
Tukuamini wewe ni mzamivu wa neno la Mungu kuzidi maprofesa waliompasisha Bi. Ellen? Inanipa shida sana.
 
Humjui vizuri; amepasishwa na mabingwa wengi duniani; wasomi wazamivu wa theology. She one of the most influential person of all times amekuwa rated hivyo. Msome kidogo hapo kisha utafakari tena!

Kuna uongo mwingi tu kwenye baadhi ya historia alizokuwa anajaribu Kuandika kwenye vitabu vyake na pia alikuwa ni mentally ill (alikuwa na shida ya akili huyo mama fatilia)
 
Tukuamini wewe ni mzamivu wa neno la Mungu kuzidi maprofesa waliompasisha Bi. Ellen? Inanipa shida sana.
Kama huniamini Yaamini maandiko ya Mungu.
Hata hivyo Mungu hana ushirika na maprofesa wa kidini.
Hakuna msomi aliewahi kumtumia bila kumbadili akili zake za chuo.

Sasa kama mimi huniamini ungemuamini vipi petro ambae hakuwa anajua kusoma wala kuandika.
 
Back
Top Bottom