Bichwa Komwe, Black and Beautiful; The Epitome of Beauty

Bichwa Komwe, Black and Beautiful; The Epitome of Beauty

Kuna watu wanasubiri ufe ndio wakusifie. Hii si haki.

Mimi sisubiri kusifiwa, au sisubiri nife ndio nisifiwe. Najisifia mwenyewe, tena sasa hivi.

Mimi ni binti wa kimanyema, nimezaliwa mkoani Mtwara mnamo mwaka 1982.

Nina sifa zote za mwanamke mzuri. Mimi ni mrefu, shupavu, makebo makubwa na mweusi TIIIII. Hata hivyo sura yangu ni ya baba. Najiamini sana.

Mwaka 2013 niliajiriwa kama askari wa jeshi la akiba. Ndio kazi inayonipatia kipato hadi sasa.

Kuna mtu mmoja jana alikuja mbio mbio ananishauri nijichubue ati ndio nipendwe. Sijui nani alimwambia nahitaji kuwa mweupe ili nipendwe?

Sisi wanawake wenye sura mbaya ndio tunaoongoza kwa mapenzi ya dhati. Tunaangalia moyo zaidi.

Nitoe rai kwa akina mama wote wenye sura za baba zetu, tujikaze na tusonge mbele. Maneno yasiturudishe nyuma.

Tuna sifa zote za kukubaliwa na kupendwa.

Ahsanteni sana. Naomba kuwasilisha.
ulishirik mauaji ya Oct 29 ukiwa wapi?
 
Back
Top Bottom