Biden akutana na viongozi wa NATO wa Mashariki mwa Ulaya

Biden akutana na viongozi wa NATO wa Mashariki mwa Ulaya

HERY HERNHO

Senior Member
Joined
Mar 4, 2022
Posts
110
Reaction score
458
Rais wa Marekani Joe Biden amekutana na viongozi wa nchi za upande wa mashariki mwa Ulaya, ambao ni wanachama wa jumuiya ya Kujihami ya NATO.

Kwenye mkutano huo wa Jumatano huko Warsaw Poland, Biden alikariri kujitolea kwa nchi yake kuhakikisha usalama wa washirika wake wa mashariki mwa Ulaya. Kauli yake imejiri baada ya Urusi kujitoa katika mkataba kati yake na Marekani wa kudhibiti silaha za nyuklia. Biden alitaja hatua hiyo ya Urusi kujiondoa kwenye makubaliano hayo kuwa kosa kubwa.

Rais wa Romania Klaus Lohannis alisema nchi za Magharibi zinapaswa kushirikiana katika kuisaidia Ukraine hadi mzozo huo utakapomalizika na ivishine vita hivyo.

Si wanachama wote wa kundi la Bucharest Tisa wamekuwa tayari kuisaidia Ukraine mfano Hungary ambayo imepuka ikipinga baadhi ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya kwa Urusi. Pamoja na Uturuki, Hungary haijaridhia maombi ya Sweden na Finland kuwa wanachama wa NATO.

Mnamo wakati kuna mvutano mkubwa zaidi kati ya Urusi na nchi za Magharibi Kuwahi shuhudiwa tangu enzi za vita Baridi miongo mitatu iliyopita, Biden aliwahutubia maelfu ya watu mjini Warsaw siku ya Jumanne ambapo alisema watawala wa kimabavu kama rais wa Urusi Vladimir Putin sharti wapingwe.

Urusi imekuwa ikisema inatizama jumuiya ya NATO kitisho kwake kiusalama.

64787216_803.jpg
 
hao jamaa watakuja kumtosa marekani kimyakimya. wataanzisha bilateral agreement na urusi kimyakimya kila mtu kivyake. Marekani atajikuta amebaki peke yake na Uingereza
 
Back
Top Bottom