Messenger RNA
JF-Expert Member
- Jul 24, 2022
- 1,411
- 3,712
Rais wa Marekani Joe Biden amesema kwa mara nyengine kwamba Marekani itailinda Taiwan endapo kutatokea "shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa" na China.
Akizungumza katika mahojiano ya chombo cha Habari cha CBS, Bw Biden alijibu "Ndiyo" alipoulizwa ikiwa hiyo inamaanisha majeshi ya Marekani yatailinda Taiwan.
Mahojiano hayo yalipeperushwa siku ya Jumapili, na kuifanya Ikulu ya White House kusisitiza kwamba sera ya Marekani haijabadilika.
Sera ya Washington daima imekuwa moja ya "utata wa kimkakati" - haijapinga kuitetea Taiwan, lakini pia haina njia mbadala.
Taiwan ni kisiwa kinachojitawala katika pwani ya mashariki mwa China ambacho Beijing inadai kuwa sehemu ya eneo lake. Washington kwa muda mrefu imekuwa na mvutano wa kidiplomasia juu ya suala hilo. Kwa upande mmoja inazingatia sera ya China Moja, msingi wa uhusiano yake na Beijing.
Chini ya sera hii, Taiwan ni sehemu ya Uchina na msimamo huo haupingiwi. Kwa hivyo Marekani haitambui kama nchi tofauti na haina uhusiano wa kidiplomasia na kisiwa hicho. Lakini inadumisha uhusiano wa karibu na kuiuzia Taiwan silaha chini ya Sheria ya Mahusiano ya Taiwan, ambayo inasema kwamba Marekani lazima ipatie kisiwa hicho njia ya kujilinda.
Bw Biden alisisitiza haya katika mahojiano na chombo cha Habari cha CBS kwa Dakika 60 siku ya Jumapili.
"Kuna sera ya Uchina moja na Taiwan hufanya maamuzi yao wenyewe juu ya uhuru wao. Hatujabadili msimamo, sio kuwahimiza wawe na uhuru wao - huo ni uamuzi wao," alisema.
Bw Biden alikuwa ametoa maoni kama hayo mwezi wa Mei, na kuapa kuingilia kijeshi kutetea Taiwan iwapo ingeshambuliwa. Ikulu ya White House ilifuatilia haraka kwa kusema harijabadilika kuhusu sera hiyo ya Muda mrefu ya Marekani .
Wakati huu pia Ikulu ya White House imetoa taarifa inayoonekana kupingana na Bw Biden: "Rais aliwahi kusema haya kabla, ikiwa ni pamoja na Tokyo mapema mwaka huu. Pia aliweka wazi wakati huo kwamba sera yetu ya Taiwan haijabadilika. Hiyo bado ni kweli. "
Lakini hii ni mara ya tatu katika mwaka mmoja ambapo Rais Biden ameenda mbali zaidi kuliko msimamo rasmi wa kuashiria ahadi ya kuchukua hatua za kijeshi - Oktoba 2021 na kisha tena Mei mwaka huu.
Mapema mwezi huu, Marekani ilikubali kuiuzia Taiwan silaha zenye thamani ya $1.1bn (£955m) sina makombora, na hivyo kusababisha hasira kutoka China.
Mvutano kati ya Marekani na China uliongezeka baada ya Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi kufanya ziara yenye utata katika kisiwa hicho mwezi Agosti - safari ambayo Bw Biden alisema "si wazo zuri".
Kujibu, Beijing iliweka kizuizi cha kijeshi cha siku tano kuzunguka Taiwan. Marekani inadai kuwa ilirusha makombora katika kisiwa hicho, lakini Beijing haikuthibitisha hilo na Taiwan ilisema makombora ambayo China ilirusha yaliruka juu angani na hayakuwa tishio lolote.
Kwingineko katika mahojiano yaliyorekodiwa mapema Jumapili, Bw Biden aliionya Urusi kutotumia silaha za nyuklia za kemikali au mbinu za matumizi ya silaha hizo katika vita vya Ukraine.
BBC Swahili