Biden invited 110 Countries - Summit for Democracy, Tanzania mpya haimo!

Ndiyo mnavyodanganyana kwenye vijiwe vyenu hapo mbogamboga [
Is DRC Congo a democratic or resource center??

Nani anapima demokrasia??
Nini kipimo cha demokrasia?
Wakati gani tuseme hii ni democratic na lini tuseme hii siyo??
 
Burundi, Rwanda, Uganda na Tanzania nje, aibu sn na hongera kwa wakenya
Wakishatoka kwa biden huko wakenya shida zitaisha au watabi vilevile?
Ingekuwa na maana kama wangekua wanaenda kuonana na Mungu.
 
IDEA report haina nguvu ukilinganisha na mchango wa US in democratic world,ndio maana inaita nchi zaidi ya 100 duniani na inaitikiwa vema.

Ndio maana Russia au U.A.E hawawezi kusikilizwa kama US. maana hawana democracy,democracy ina nguvu ya utu mwema.

Kwa yanayofanywa na Tanzania kwa sasa tunapoteza credibility ata ya kusikilizwa na waafrika wenzety achilia mbali convincing power ya kuita nusu tu ya nchi za Afrika! Tunanuka dhulma na damu kwa sasa!

US itabaki kuwa ndie msimamizi mkuu wa demokrasia duniani kwa karne nyingi zijazo.
 
Wakishatoka kwa biden huko wakenya shida zitaisha au watabi vilevile?
Ingekuwa na maana kama wangekua wanaenda kuonana na Mungu.
Ujinga wenu ndiyo huu, bibi ushungi akitoka Uganda anakuja na nini? pia mbona anasema anafungua nchi ana maanisha nini? wakenya walipata fedha za covid 2.6T mapema sababu ya ujinga wenu tulichelewa matokeo yake tumepata 1.5T, wenzako wanachungulia fursa mapema, unashitaki watu kwa kesi za kubumba ugaidi unategemea nini? wawekezaji utawasikia kwenye redio
 
Marekani anajifunza kwetu demokrasia, yaani Mama Samia ndio mwalimu wa demokrasia, sasa haiwezekani watualike, hawana cha kutufunza sisi.
 
Tanzania tayari tunademokrasia karibu sawa na Marekani,

Unataka atualike tujafanye nini?

Mwenye Afya hahitaji Tabibu mkuu
Ila tunahitajika tuvae barakoa kwa kujilazimisha na kupata chanjo ili tuweze kupewa pesa za COVID 19 ili tujenge madarasa na vyoo vya wanafunzi! Viva Awamu ya Sita. Viva Tanzania!!!!!
 
Xi Jinping naye amealika Mkutano wa wakuu wa nchi duniani kujadili uchumi na demokrasia. Tanzania mbele kama tai. USA haimo kwa hiyo ngoma droo.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje wa Bunge la ulaya akataa ripoti iliyoonesha matumaini ya mabadiliko ktk utawala wa awamu ya sita


David James McAllister MEP ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge la Ulaya ametoa hotuba nzito na kuwalaumu wataalum wa Umoja wa Ulaya waliotoa ripoti mbele ya kamati hiyo ya Bunge yenye ushawishi mkubwa pamoja na kuaminika kusimamia values / desturi na makubaliano ya kuheshimu haki za binadamu na utawala bora .

Mwenyekiti David James McAllister MEP akakumbushia barua yake aliyoandika kuwaonya wataalamu wa Umoja wa Ulaya EEAS mwaka jana mwezi November 2020 kuhusu "kuubeba" utawala dhalimu usiofuata haki za msingi za kibinadamu. Ripoti hiyo ilisema kuna maendeleo 'makubwa' nchini Tanzania mbali ya changamoto ndogo ndogo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya akakumbushia hicho kinachoitwa 'changamoto ndogo ndogo' kwa hakika ni kikubwa na hakipaswi kutupiliwa mbali ikiwa watu wanakamatwa ovyo, kutupwa mahabusu, kufunguliwa mashtaka, kutishiwa haki ya kuishi n.k mambo ambayo ndiyo msingi mkubwa wanaousimamia Umoja wa Ulaya wakati wa kutoa msaada kwa nchi yoyote ulimwenguni
EEAS - European External Action Service - European Union External Action
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge la Ulaya amesema mfano wataalamu hao je wameweza kukutana ndani ya Tanzania na mwenyekiti wa CHADEMA au makamu mwenyekiti wa CHADEMA? Ambao ni viongozi wa chama kikuu cha upinzani, mmoja akiwa rumande kwa kesi ya kutunga huku mwingine akiwa uhamishoni Belgium halafu wataalamu hao wanasema ni changamoto ndogo ndogo?

Pia kuna raia wanaoshiriki siasa Tanzania wenye mtizamo mbadala walio wanachama, wapenzi na wafadhili wazalendo wa KiTanzania wanabaguliwa kushiriki ktk vyombo vya maamuzi ngazi zote, wanaoozea ktk jela mbalimbali Tanzania au biashara zao kuhujumiwa je hayo ni mambo madogo ? Amehoji David James McAllister mwenyekiti huyo makini wa kamati ya Bunge la ulaya.

Hivyo amewataka wataalamu hao waliotumwa na bunge la Umoja wa Ulaya kuwabebeleza watawala wa Tanzania kuacha ukandamizaji, kujitathmini kama wanataka kulimwa barua nyingine kali ya karipio kuhusu ripoti yao iliyozua maswali mengi ndani ya Bunge la Ulaya na miongoni mwa wabunge wa Bunge hilo la Ulaya mwaka 2020 na vivyo hivyo pia mwaka huu mwezi November 2021 inayojadiliwa na Kamati hiyo ya Bunge la Ulaya.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge la ulaya amewataka wataalamu hao kuja na majibu mujarabu ya kuibana serikali ya Tanzania kwa kuwa inatumia misaada ya Umoja wa Ulaya itokanayo na kodi za raia wa nchi wanachama zinazoamini katika utawala bora, haki za binadamu kulindwa na demokrasia hivyo haiwezekani nchi viongozi wa nchi walio wakandamizaji kama wa Tanzania kufaidi jasho na nguvu wa walipa kodi wa Ulaya wanaoamini katika uhuru, haki na Maendeleo ya kweli ya watu ktk demokrasia inayozingatia utu.

amesema yeye na wajumbe wabunge wa kamati ya mambo ya nje wanajiandaa kupendekeza hatua "kali" dhidi ya utawala unaoendekeza udhalimu waziwazi na kwa kificho.

David James McAllister mwenyekiti wa Kamati Ya Bunge la Ulaya ya Mambo ya Nje anasema mbali na ripoti hiyo ya wataalamu wake pia wanapata habari kupitia balozi za Marekani, Canada , Uingereza na balozi wa nchi wanachama wanaohudhuria kesi namba 16 ya mwaka 2021 ya tuhuma nzito za kupikwa dhidi ya Mbowe na wenzie 3, na kesi hiyo ni kichekesho dhidi ya Umoja wa Ulaya na raia wa wa Umoja wa Ulaya ambao wote wanaamini ktk haki mbele ya sheria, demokrasia na kutokuwepo ugandamizaji wa haki za kibinadamu za aina yoyote.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge anataka kuona wataalamu hao wanakuja na mkakati gani wa kuibana serikali ya Tanzania inapotaka misaada na mikopo, kwani sasa siyo muda tena wa maongezi / dialogue yasiyo na kikomo kuhusu hali hii mbaya ya kisiasa nchini Tanzania, bali ni wakati wa Umoja wa Ulaya kufanya matendo kwani muda wa maneno umekwisha, ili ujumbe uwaingie watawala dhalimu.

 
Ipo Kenya tu.Rwanda, Burundi, Uganda na Tanzania zimefyekelewa mbali
 
Nchi yoyote inayojitambua na kukemea mali zake zisiibiwe - hasa nchi na Kiafrika, hazipendwi na mataifa ya magharibi.
Utakuta nchi ambazo wazungu wamejimilikisha ardhi kubwa na waafrika wanaswaga duhu, nchi hiyo inakumbatiwa na mabeberu!
 


09 December 2021

Why is the US President hosting a global summit on democracy? | Inside Story


The United States portrays itself as one of the world's greatest democracies. But President Joe Biden says democracy is under siege from authoritarian regimes, so he is holding a virtual summit to give democracy a boost. Some countries including Russia, China, Iran and Hungary were not invited. And critics say the US has no moral authority while continuing to support autocratic rulers abroad and restricting voting rights at home. So what will the meeting achieve?

Source : Al Jazeera English
 
Hivi Ni Nani alipiga mabomu Nagasaki na Hiroshima?Ni Nani amepeleka demokrasia yake Kule Libya,Iraq, Afghanistan,Syria na hali ikoje Kule kwa Sasa?
Kote huko marekani wameshindwa vibaya, hakuna che demokrasia wala jama yake na demokrasia, kinachoendelea ni domoghasia tu!
Huwezi kueneza demokrasia kwa kutumia mtutu wa bunduki.
Wanachofanya wamarekani ni kujitengenezea wateja wa kuwauzia silaha tu, na kuwananga Russia na China wasiuze.
 
Marekani wameiweka Tanzania kundi Moja na China na Urusi.Tofauti iliyopo China wana Uchumi bora kabisa ,Urusi ni superpower inashindana na marekani kwa silaha .Swali,Je, Tanzania inashindana na Marekani Kwa kitu gani?
 
Marekani wameiweka Tanzania kundi Moja na China na Urusi.Tofauti iliyopo China wana Uchumi bora kabisa ,Urusi ni superpower inashindana na marekani kwa silaha .Swali,Je, Tanzania inashindana na Marekani Kwa kitu gani?
Coca Cola yetu ya pilipili ni nzuri sana kuliko ya Marekani.
Dunia ijayo si ya viongozi katili na wakandamiza haki za binaadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…